Bw. Stephen Mbundi, Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiongoza Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa majadiliano kwa ngazi ya Watalaam wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwa maandalizi ya Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika tarehe 30 Januari 2019 jijini Arusha. Mkutano huu utafuatiwa na ule wa Makatibu Wakuu tarehe 29 Januari 2019. Pamoja na mambo mengine mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri utapitia na kujadili agenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na taarifa ya utekelezaji wa maazimio yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo; taarifa kuhusu masuala ya miundombinu, forodha na biashara na masuala ya utawala na fedha. Mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika jijini Arusha tarehe 1 Februari 2019. Kulia ni Bw. Eliabi Chodota, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Kijamii na kushoto ni Bw. Bernard Haule, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.