TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Watanzania 70 wahitimu Chuo Kikuu
cha Galgotias nchini India
Watanzania
zaidi ya 70 wakiwemo wawili wa shahada ya uzamivu wamehitumu masomo yao katika
Chuo Kikuu cha Galgotias nchini India katika
fani mbalimbali tarehe 14 Januari
2019.
Balozi
wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika
mahafali ya nne ya chuo hicho aliwatunuku vyeti wanafunzi hao na wengine kutoka
nchi mbalimbali duniani na kuwasihi kutumia
ujuzi walioupata kuchangia kikamilifu maendeleo ya nchi walizotoka.
‘Ulimwengu
unasubiri uongozi mpya na mawazo mapya na kanuni na miiko madhubuti kutoka
kwenu. Hivyo, kifanyeni chuo kijivune kupitia kwenu kwa kutoa michango yenye
tija katika mataifa na jamii zenu, hususan kwa kufanya kazi kwa bidii, ubunifu
na uadilifu mkubwa katika kutimiza majukumu yenu', Balozi Luvanda alisema.
Balozi
Luvanda alisema kuwa wanafunzi hao wanahitimu huku dunia ikishuhudia mapinduzi
ya teknolojia mbalimbali zikiwemo za kidigitali, teknolojia ya matumizi ya
sarafu za kidigitali (block chain), matumizi ya kiwango kikubwa cha data katika kufanya
maamuzi (big data revolution), usalama wa mitandao (cybersecurity) na matumzi ya teknolojia katika kutekeleza kazi
ambazo awali zilikuwa zinafanywa na mwanadamu (artificial intelligence). Alielezea matumaini yake kuwa
chuo hicho kitakuwa kimewandaa vyema wahitimu hao kukabiliana na changamoto za mapinduzi ya
teknolojia katika kutekeleza majukumu yao.
Mhe.
Balozi alihitimisha hotuba yake kwa kuwasihi wahitimu hao kuwa, kutunukiwa vyeti
sio mwisho wa kujifunza. Wanatakiwa waendelee kusoma vitabu kwa kuwa kusoma vitabu ni sawa na kuufanyia matengenzo ubungo. ‘Akili ya mwanadamu
ni kama bustani, bustani isipomwagiwa maji na kupaliliwa itaota magugu na kufa
kabisa. Mhe. Balozi alimaliza.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
16 Januari
2019
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.