Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan, Mhe. Shinichi Goto aliyeambatana na washiriki kutoka Tanzania wanao kwenda Nchini Japan kwa ajili ya kupata mafunzo ya Uongozi katika sekta mbalimbali. Mafunzo hayo yatadumu kwa muda wa siku 50. Aidha, Dkt. Ndumbaro amemshukuru Balozi Goto kwa kuendelea kuiwakilisha vyema nchi ya Japan hapa nchini ambapo aliahidi kuwa Japan itaendelea kuchangia maendeleo katika sekta mbalimbali. Dkt. Ndumbaro amewaasa Washiriki wanaokwenda katika mafunzo hayo kuitumia fursa hiyo vyema kwa kujifunza mambo mampya kutoka Taifa hilo.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Bw. Caesar Waitara (hayupo pichani) yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar Es Salaam. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.