Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Misri hapa nchini Mhe. Mohamed Gaber Abouelwafa. Katika mazungumzo yao Balozi Abouelwafa alimweleza Dkt. Mahiga kuwa wanafurahishwa na mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Misri, ambapo kwa sasa Misri wanatekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la kuzalisha Umeme Nchini, vilevile Misri itaendelea kuboresha miundombinu ya uzalishaji wa maji kwa kuchimba visima vingine vya maji Nchini. Pamoja na Mambo mengine Dkt. Mahiga alimweleza Balozi Abouelwafa kuwa Tanzania itaendelea kumpa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini. Aidha, Dkt. Mahiga alimweleza Balozi kuwa Tanzania inatambua mchango wa Misri kwenye sekta mbalimbali zikiwemo Afya, Elimu na Biashara. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, zilizopo jijini Dar Es Salaam |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.