Wajumbe wengine wa Tanzania ====================================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
KUHUSU MKUTANO MAALUM WA 38 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA JUMUIYA YA AFRIKA
MASHARIKI
Mkutano Maalum wa 38 wa Baraza la
Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unafanyika jijini Arusha kwa lengo la
kujadili na kukubabaliana na agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye
Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo utakaofanyika tarehe 1 Februari,
2019.
Mkutano
huo ambao unaongozwa na Mwenyekiti kutoka Jamhuri ya Uganda ambaye pia ni
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Kirunda Kivejinja utajadili agenda
mbalimbali muhimu ambazo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa maamuzi mbalimbali
yaliyofikiwa na Baraza hilo kwenye vikao vilivyopita; taarifa kutoka Ofisi ya
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, taarifa kuhusu masuala ya
miundombinu, forodha na biashara na ripoti ya kamati ya utawala na fedha.
Agenda zingine ni taarifa ya Baraza kwa Wakuu wa Nchi kuhusu utekelezaji wa maamuzi
mbalimbali yanayofiwa kwenye mikutano ya Wakuu hao wa Nchi na Kalenda ya
Matukio ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa
kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Juni 2019.
Mkutano
huo wa Mawaziri ulitanguliwa na vikao vya Maafisa Waandamizi kutoka nchi wanachama
kilichofanyika tarehe 28 Januari kikifuatiwa na kikao cha Kamati ya Uratibu
chini ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 29 Januri
2019.
Ujumbe
wa Tanzania kwenye mkutano huo unaongozwa na Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki na kuwahusisha pia Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb), Waziri wa , Katiba
na Sheria, Mhe. Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri Fedha na Mipango, Mhe. Kapt.
Mstaafu George Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma, Mhe. Joseph Kakunda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara na Mhe.
Innocent Bashungwa, Naibu Waziri wa Kilimo.
Jumuiya
ya Afrika Mashariki ambayo inaundwa na nchi sita za Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi,
Rwanda na Sudan Kusini imeendelea kuhakikisha wananchi katika nchi hizo
wananufaika na Jumuiya hiyo hususan katika nyanja za biashara, ulinzi na
usalama, viwanda, kilimo, miundombinu na huduma za kijamii.
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Arusha.
30 Januari 2019
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.