Tuesday, April 24, 2012

Balozi Mteule wa Rwanda awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho


Balozi Mteule wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi, akimkabidhi nakala za hati za utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB), leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. (Picha na Tagie Daisy Mwakawago).


Mhe. Membe akiongea na Mhe. Dkt. Rugangazi, Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini.


Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi, Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini akizungumza jambo baada ya kuwakilisha nakala za hati za utambulisho kwa Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.




 
Na ROSEMARY MALALE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb) amemhakikishia ushirikiano Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini, Dkt. Benjamin Rugangazi alipofika ofisini kwake kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho leo.

Akizungumza na Balozi huyo, Mhe. Membe alimkaribisha nchini na kusema kuwa Tanzania na Rwanda zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na kwamba anafurahi na anamkaribisha wakati wowote ofisini kwake kwa majadiliano kuhusu kuimarisha na kukuza ushirikiano huo.

“Nimefurahi Balozi upo hapa nchini tayari, Tanzania ni nchi nzuri ya kirafiki na utafurahia kuwa Tanzania. Ninakukaribisha wakati wowote utakapohitaji kuwasiliana na na mimi kwa mashauriano,” alisema Mhe. Membe.

Kwa upande wake Balozi huyo Mteule alimshukuru Mhe. Membe na kueleza kuwa Rwanda na Tanzania zimeendelea kushirikiana kama ndugu kwa muda mrefu na kwamba atashirikiana na Wizara na Watumishi kwa ujumla kwa karibu.






No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.