Wednesday, November 28, 2012

Rais Kikwete ahutubia Mkutano wa Tatu wa Bunge la Afrika Mashariki

m

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Margaret B. Ziwa akimkaribisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipowasili kwenye Makao Makuu ya Jumuiya hiyo kwa ajili ya kuwahutubia Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki mjini Arusha tarehe 27 Novemba, 2012.

Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Margaret Ziwa akitoa salamu za kumkaribisha Mhe. Rais Kikwete kuhutubia Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki. Anayeoneka pembeni mwa Mhe. Ziwa ni Mhe. Anne Makinda, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe.  Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisisitiza jambo wakati alipokuwa anawahutubia Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki mijini Arusha tarehe 27 Novemba,2012
Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki na wageni waalikwa wakimsikiliza Mhe. Rais Kikwete alipowahutubia.

Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhe. Ziwa mbele ya Jengo Jipya la Makao Makuu ya EAC.

Bw. David Mwakanjuk (katikati), Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akifafanua jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha (kushoto) Mhe. Magesa Mulongo kabla ya kikao cha Bunge la EAC kuanza tarehe 27 Novemba, 2012. Mwingine katika picha ni Afisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.