Thursday, November 8, 2012

Ushirikiano kati ya Tanzania na China wazidi kukua; Rais Kikwete azinduzia bomba la gesi asilia



Rais Kikwete azindua Ujenzi wa Bomba la Gesi Asilia kutoka Mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi ujenzi wa bomba la gesi asilia linalotoka Mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam katika maeneo ya Kinyerezi, leo jijini Dar es Salaam.  Akishuhudia uzinduzi huo (kushoto) ni Makamu wa Rais, Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal.  


Rais Kikwete, Makamu wa Rais Dkt. Bilal na viongozi wengine wakimsikiliza Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb), Waziri wa Nishati na Madini ambaye alikuwa akielezea kuhusu miundombinu ya bomba la gesi la asilia. 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kampuni inayojenga bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, Benki ya Exim ya China na viongozi waandamizi wa Serikali akiwemo Balozi Dkt. Philip S. Marmo (wa pili kulia - mstari wa mbele), Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini China.  Rais Kikwete aliwakaribisha Ikulu kwa mazungumzo baada ya uzinduzi rasmi wa ujenzi wa bomba hilo maeneo ya Kinyerezi, jijini Dar es Salaam.



Picha zote kwa hisani ya      www.issamichuzi.blogspot.com







No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.