Friday, November 30, 2012

Hafla ya Kufungua Jengo Jipya la Makao Makuu ya EAC

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Serikali na wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika hafla ya ufunguzi wa jengo la Makao Makuu ya EAC mjini Arusha tarehe 28 Novemba, 2012

Mhe. Mwai Kibaki, Rais wa Kenya na Mwenyekiti wa EAC akiwasilisha hotuba yake wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Makao Makuu ya EAC mjini Arusha

Mhe. Rais Kibaki akitoa cheti kwa mmoja wa Wahandisi waliofanikisha ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya EAC mjini Arusha

Mwakilishi wa Serikali ya Ujerumani naye akitoa hotuba fupi katika hafla hiyo. Serikali ya Ujerumani ndiyo iliyodhamini ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya EAC

Mhe. Rais Kikwete wa kwanza kushoto akiwa na baadhi ya viongozi wenziwe wa EAC wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa jengo jipya la Makao Makuu ya EAC.

Mhe. Rais Kikwete (katikati) na Viongozi wenziwe wa EAC wakiwa katika moja ya vyumba vya jengo la Makao Makuu ya EAC mjini Arusha

Mhe. Rais Kikwete wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa EAC mjini Arusha.

Mwakilishi wa Serikali ya Ujerumani na wa EAC wakiweka saini Mkataba wa kushirikiana kiuchumi kati ya Ujerumani na EAC

Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akibadilishana mawazo na Bw. Richard Sezibera, Katibu Mkuu wa EAC wakati wa hafla ya kufungua Jengo la Makao Makuu ya EAC mjini Arusha

Wanafunzi wa Shule ya Msingi wakitoa burdani wakati wa hafla ya kufungua jengo la Makao Makuu ya EAC mjini Arusha

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.