Monday, December 3, 2012

Naibu Katibu Mkuu akutana na Msajili wa MICT

Mhe. Balozi Rajabu Gamaha, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kushoto) akiwa katika picha na Bw. John Hocking, (wa tatu kutoka kulia) Msajili wa Mahakama iliyorithi shughuli za ICTR (United Nation Mechanism for International Criminal Tribunals (MICT). Bw. Hocking alikuja Wizarani kwa madhumuni ya kufanya mazungumzo na uongozi wa Wizara kuhusu utendaji kazi wa Mahakama hiyo. Wengine katika picha ni watendaji wa Mahakama hiyo.

Mhe. Balozi Gamaha akifafanua jambo wakati alipofanya mazungumzo na Bw. Hocking (hayupo katika picha)

Bw. Hocking (kulia) pamoja na ujumbe wake wakimsikiliza kwa makini Naibu Katibu Mkuu wakati wa mazungumzo yao.

Msajili wa MICT akitoa maelezo kwa Naibu Katibu Mkuu (hayupo pichani) wakati alipomtembelea ofisini kwake.

Naibu Katibu Mkuu, Mhe. Gamaha akimsikiliza kwa makini Bw. Hocking. (hayupo katika picha)

Balozi Irene Kasyanju, (kulia) Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa naye akifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Naibu Katibu Mkuu na Msajili wa MICT huku Afisa kutoka Kitengo chake, Bw. Benedict Msuya akinukuu mambo muhimu ya mazungumzo hayo.

Wajumbe wakimsikiliza kwa makini Mhe. Balozi Gamaha aliye katikati.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.