Monday, December 17, 2012

Tanzania na Burundi zasaini Barua ya Kuomba Msaada wa Kuimarisha Mpaka

 
Mhe.Balozi  Rajabu Gamaha, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (kulia) na Balozi Albert Shingiro, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Burundi wakiweka saini barua ya pamoja kwa niaba ya Serikali ya Nchi zao ambayo itawasilishwa kwenye Shirika la Kijerumani la GIZ ili kuomba msaada wa kuimarisha mpaka kati ya Tanzania na Burundi.
Balozi Gamaha kulia akibadilishana mawazo na Balozi Shingiro mara baada ya zoezi la uwekaji saini barua kukamilika.
Ujumbe wa Serikali ya Burundi uliofuatana na Balozi Shingiro ukifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Gamaha na Balozi Shingiro ambao hawapo pichani.

Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Lilian Kimaro na Afisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nao wakifuatilia mazungumzo hayo.

Ujumbe wa Tanzania na ule wa Burundi wakisikiliza mazungumzo kati ya Balozi Gamaha na Balozi Shingiro.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.