Wednesday, December 5, 2012

Mhe. Membe azungumza na Waandishi wa Habari kuhusu Mkutano wa SADC na Meli za Iran

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipokutana nao Wizarani jana. Mhe. Waziri alizungumza na Waandishi hao kuhusu Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) unotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam tarehe 7 na 8 Desemba, 2012 na pia alijibu tuhuma kuhusu Meli za Iran kusajaliwa na kupeperusha Bendera ya Tanzania. Wengine katika picha ni Balozi Rajab Gamaha (kulia), Kaimu Katibu Mkuu na Balozi Dora Msechu, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifurahia jambo wakati wakimsikiliza Mhe. Waziri Membe (hayupo pichani) alipozungumza nao.
Mhe. Membe akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
Mhe. Membe akiendelea na mkutano na Waandishi wa Habari (hawapo pichani) huku Balozi Gamaha akimsikiliza kwa makini.
Mhe. Waziri Membe akisisitiza jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) huku Balozi Msechu akitafakari.


Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) wakati wa mkutano na waandishi wa habari. Kutoka kushoto ni Balozi Vincent Kibwana, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Irene Kasyanju, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria.
Baadhi ya Watendaji wengine wa Wizara ya Mambo ya Nje waliohudhuria mkutano huo wa Mhe. Membe na Waandishi wa Habari. Kutoka kushoto ni Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Bw.Joachim Otaru, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango na Bw. Gabriel Mwero, Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.