Thursday, December 13, 2012

Mafunzo ya OPRAS kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara yaanza

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano, Mhe. Balozi Rajab Gamaha (aliyesimama) akifungua Mafunzo ya Upimaji wa Utendaji Kazi kwa Uwazi (OPRAS) kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara yaliyoendeshwa na Wakufunzi kutoka Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Wengine katika picha kutoka kushoto ni Bw. Dushhood Mndeme, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Neema, Mkufunzi kutoka Utumishi na Bi. Elizabeth Makyao kutoka Utumishi.
Bi. Elizabeth kutoka Utumishi akiwasilisha mada kuhusu mfumo huo wa upimaji kazi kwa njia ya uwazi (OPRAS) kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara (hawapo pichani) huku Bal. Gamaha, Bw. Mndeme na Bi. Neema wakimsikiliza.
Bi. Neema kutoka Utumishi akisisitiza jambo kuhusu mafunzo hayo kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Wizara (hawapo pichani) huku Balozi Gamaha akisikiliza.


Baadhi ya Wakurugenzi na Wakurugenzi Wasaidizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo.
Baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo  na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mafunzo hayo.
Sehemu nyingine ya Watendaji Wakuu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia mafunzo hayo.
Baadhi ya Wakuu wa Vitengo na Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki mafunzo hayo.
Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakiendelea na mafunzo ya OPRAS.

Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo ya OPRAS.
Maafisa wengine wa Mambo ya Nje wakiendelea na mafunzo ya OPRAS.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.