Friday, December 7, 2012

Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi wa SADC waanza kwa kikao cha Troika

Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisalimiana na Mhe. Jacob Zuma (katikati), Rais wa Afrika Kusini mara baada ya Mhe. Zuma  kuwasili Ikulu, Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Troika). Mwingine katika picha ni Dkt. Tomaz Augusto Salomao, Katibu Mtendaji wa Jumuiya hiyo.Kikao hicho ni maandalizi ya Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaotarajiwa kufanyika katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam tarehe 8 Desmba, 2012.
Mhe. Rais Kikwete (wa pili kutoka kulia) akifurahia jambo na Marais wenzake Mhe. Zuma (wa tatu kutoka kushoto) na Mhe. Hifikepunye Pohamba (kulia), Rais wa Namibia walipokuwa Ikulu, Dar es Salaam kabla ya Mkutano wa Troika kuanza.Wengine katika picha ni Mhe. Joaquim Chissano (wa pili kutoka kushoto), Rais Mstaafu wa Msumbiji na Msuluhishi wa Mgogoro wa kisiasa nchini Madagascar na Dkt. Salomao, Katibu Mtendaji wa SADC.
Mhe. Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) akiongoza kikao kujadili masuala mbalimbali ya kikanda. Kikao hicho kilifanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Kikwete akizungumza na Mabalozi kabla ya mkutano wa Troika kuanza. Kutoka kushoto ni Balozi Liberata Mulamula, Msaidizi Mwandamizi wa Rais katika masuala ya Diplomasia, Balozi Shamim Nyanduga (wa tatu kutoka kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji na Balozi Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.
Balozi Naimi Aziz (katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na baadhi ya wajumbe waliofika kuhudhuria mkutano wa Troika uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.