Monday, November 5, 2012

Sherehe za Mwenge za Kuadhimisha Miaka 100 ya ANC



Mhe. Balozi Radhia Msuya, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini akisema machache wakati wa Sherehe za Mwenge za kuadhimisha Miaka 100 ya Chama Cha African National Congress (ANC) zilizofanyika hivi karibuni tarehe 30 Oktoba, 2012 kwenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania mjini Pretoria, Afrika Kusini.


 
Wanachama wa ANC wakisikiliza hotuba ya Mhe. Balozi Msuya.


Mjumbe wa Chama cha ANC, Bw. Sochayile Khanyile, naye akiongea machache wakati wa Sherehe hizo.


Wanajeshi wakiwa wamejipanga kabla ya Sherehe rasmi za kuwasha Mwenge kuanza.  Kushoto ni Bw. Robert Kahendaguza, Mtawala Mkuu kwenye Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchi Afrika Kusini.


Mhe. Balozi Radhia Msuya, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Afrika Kusini, akiwasha Mwenge, ikiwa ni ishara ya kuadhimisha Sherehe za Kitaifa za Kutimiza Miaka Mia Moja ya kuanzishwa kwa Chama Cha ANC cha Afrika Kusini.  

Sherehe hizo zilianza katika vitongoji na miji kadhaa nchini Afrika Kusini tangu mwezi Januari 2012, ambapo viongozi mbalimbali wa Kitaifa walihudhuria, wakiwemo Mhe. Rais Jacob Zuma ambaye alikuwa mgeni rasmi, Rais mstaafu Mhe. Benjamin W. Mkapa, pamoja na marais na viongozi wa nchi mbali mbali.

Wakati huo huo, matamasha mbali mbali, mijadala, maonyesho na mbio za Mwenge zimekuwa zikiendelea nchini Afrika Kusini katika muendelezo wa Maadhimisho hayo ya Miaka 100 ya Chama Tawala.   Aidha, tarehe 31 Oktoba, 2012 Mbio za Mwenge za Maadhimisho hayo zilifanyika katika Balozi zaidi ya kumi za nchi marafiki, ikiwa ni sehemu ya kutoa ushirikiano katika harakati za Ukombozi wa Afrika Kusini. Nchi hizo zinaijumuisha Tanzania, Zimbabwe, Botswana, Namibia, Zambia, Angola, Palestina, Urusi, China, Cuba na nyingine nyingi. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.