Friday, June 3, 2016

Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za Ghuba

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akimkaribisha leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi alipokuja kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini.

 Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimshukuru Balozi kwa kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Oman, vilevile aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano hata kwa Balozi atakaye teuliwa kuja kuiwakilisha nchi ya Oman. kwa upande wa Balozi Al-raqaishi alitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mahiga na uongozi wote wa Wizara kwa ujumla kwa ushirikiano aliokuwa akipewa kwa kipindi chote cha uwakilishi wa Taifa lake hapa nchini. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Tahir Bakari, kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Al-ruqaishi.
Waziri Mahiga na Balozi Al-ruqaishi wakiwa katika picha ya pamoja.
       ===Wakati huo huo Waziri Mahiga alizungumza na Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu===

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Falme za Kiarabu (U.A.E) nchini Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Al suwaidi alipokuja kumtembelea wizarani, na kufanya naye mazungumzo  yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu katika nyanja mbalimbali zikiwemo:  Afya, Elimu, Biashara na Uchumi, pia Balozi wa Al suwaidi alimpongeza Waziri Mahiga kwa Hotuba ya Bajeti ya 2016/2017 iliyopitishwa na Bunge. 
Waziri Mahiga na Balozi Al suwaidi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo
                      === Pia Dkt. Mahiga alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kuwait  ====

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisaliamiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipomtembelea Wizarani mapema leo asubuhi na kufanya naye mazungumzo yaliyojikita katika kuboresha na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Kuwait.
Dkt. Mahiga akimweleza jambo Balozi Al Najem
Balozi Al Najem akimwelezea jambo Waziri Mahiga mara baada ya kuzindua Tovuti ya Ubalozi wao, huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya kati Balozi Abdallah Kilima (wa Tatu kutoka kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje wakishuhudia.  
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Al Najem mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

==== Vilevile Balozi  Mahiga alikutana kwa mazungumzo na  Balozi wa Qatar ====
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Mhe. Abdulla Jassim Al Maadad alipokuja kumtembelea Wizarani, mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Qatar katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Biashara na Uchumi.
Balozi Al Maadadi naye pia alimweleza Waziri Mahiga atahakikisha kuwa anaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na nchi yake, sambamba na kuhakikisha Serikali nchini Qatar inaisaidia Tanzania hasa katika sekta ya elimu, biashara na uchumi ambazo Qatar imekuwa ikifanya vizuri.
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga akiagana na Balozi Al maadadi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

==== Mwisho Mhe. Waziri alikutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia  ====

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Wajih Alotaabi alipokuja kumtembelea katika ofisi za Wizara  na kufanya naye  mazungumzo, ambapo katika mazungumzo yao Dkt. Mahiga ameshukuru Taifa la Saudi Arabia kwa kuwa na Mahusiano Mazuri na nchi ya Tanzania, pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Alotaabi, kwa kufanikisha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Ade Al Jubair alipokuja kwa ziara ya kikazi nchini na kuweka saini ya Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi na Uwekezaji.  
Mhe. Wajih Alotaabi naye alitoa shukrani kwa ushirikiano ambao amekuwa akipewa na Wizara na Serikali kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Tahiri Bakari, kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia Mhe. Wajih Alotaabi
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Mhe. Wajih Alotaabi mara baada ya kumaliza mazungumzo 
Waziri mahiga katika Picha ya pamoja na Mhe. Alotaabi
Picha ya Pamoja


Wanachuo wa Royal Diffence College watembelea Wizara ya Mambo ya Nje.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Edward Sokoine, akitoa maelezo ya awali wakati wa kuanza kwa mkutano na wanafunzi wa chuo cha Ulinzi cha Royal College of Diffence Studies kilichopo nchini Uingereza (hawapo pichani), ambao wapo kwenye ziara ya mafunzo katika nchi za Tanzania, Ethiopia na Malawi kwa ajili ya kubadilishana mawazo namna masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yanayoibuka hivi sasa yanavyoathiri utulivu, usalama na ustawi wa nchi, kanda na dunia kwa ujumla. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Samuel Shelukindo.
Baadhi ya wanachuo hao wakisikiliza maelezo kutoka kwa mzungumzaji meza kuu (hayupo pichani). Masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na hali ya usalama katika eneo la nchi za maziwa makuu, nafasi ya wakuu wa nchi za Afrika katika utatuzi wa migogoro, uhusiano wa Tanzania na nchi jirani na mikakati ya kukabiliana na ugaidi katika kanda na dunia kwa ujumla.
Baadhi ya wanachuo pamoja na Askari wa JWTZ (waliovaa sare), wakisikiliza maelezo kutoka kwa mzungumzaji meza kuu (hayupo pichani).
 
Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mazungumzo.Wa kwanza kutoka kulia ni Bi. Olivia Maboko, Bi. Lilian Kimaro na Bi. Mona Mahecha
Mmoja wa wanachuo hao akiuliza swali.

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo akiendelea kufafanua jambo katika mkutano huo.
 
Kikao kikiendelea...
 Balozi Sokoine, akifafanua jambo.
Kikao kikiendelea.
======================
PICHA NA: REUBEN MCHOME.

Press Release



PRESS RELEASE

VACANCY ANNOUNCEMENT FROM THE WORLD METEOROLOGICAL ORGANIZATION (WMO)

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received Vacancy Notice No. 1962 for the post of Chief Human Resources Division from the World Meteorological Organization (WMO) for qualified individuals to apply. 

The deadline for application is 14th June, 2016. The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply.


Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation, Dar es Salaam.
03th June, 2016

Thursday, June 2, 2016

Waziri Mahiga ahitimisha Mkutano kuhusu Utawala wa Sheria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akitoa hotuba wakati wa kufunga rasmi Mkutano wa Kimataifa kuhusu masuala ya Utawala wa Sheria uliofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 1 na 2 Juni, 2016 na kuwahusisha Mawaziri kutoka nchi za Afrika. Katika hotuba yake Mhe. Mahiga alisisitiza kuwa Tanzania itaendelea kupambana na rushwa ambaye ni adui mkubwa wa haki na usawa ili kuimarisha utawala wa sheria
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Baraka Luvanda akifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Mahiga (hayupo pichani)
Bi. Irene Khan, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Sheria (IDLO) ambao ndio waandaaji wa mkutano huo kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania nae akichangia jambo wakati wa kumalizika kwa mkutano huo.
Waziri Mahiga akiwa na Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Luigi Scotto (katikati) pamoja na Afisa katika Ubalozi huo
Mhe. Waziri Mahiga akisalimiana na Afisa Mwandamizi kutoka Ubalozi wa Burundi hapa nchini
Waziri Mahiga akizungumza na waandishi wa habari
Picha na Reginald Philip

Mhe. Kairuki afungua Mkutano kuhusu Utawala wa Sheria

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mhe. Angella Kairuki (Mb), akitoa hotuba wakati wa ufunguzi rasmi wa Mkutano wa ngazi ya Mawaziri wa nchi za Afrika kuhusu Utawala wa Sheria ulioandaliwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Sheria ya Kimataifa  (IDLO) na Serikali ya Tanzania na kufanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 01 na 02 Juni 2016.  Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Bi. Irene Khan. Waziri Kairuki alikuwa Mgeni Rasmi katika  Mkutano huo unaojadili nafasi ya Sheria katika kufikia Agenda ya Maendeleo Endelevu ya mwaka 2030 na Agenda ya AU ya mwaka 2063

Mhe.  Kairuki (Mb), wa pili kutoka kulia akiwa pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wa kwanza kulia, Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin William Mkapa wa kwanza kushoto na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kimataifa ya Sheria (International Development Law Organization - IDLO), Bi. Irene Khan. Mhe. Mkapa na Mhe. Kikwete walikuwa wazungumzaji wakuu kwenye mkutano huo.     
Rais Mstaafu, Mhe. Benjamin Mkapa akiongea kwenye mkutano huo.
Rais Mstaafu, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete naye akiongea katika mkutano huo
Sehemu ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia mkutano
Mhe. Rais Mstaafu Kikwete akifuatilia mkutano, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi  wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elisha Suku.
Wajumbe wa mkutano wakisikiliza hotuba  za ufunguzi wa Mkutano wa IDLO 
Sehemu nyingine ya ujumbe wa mkutano ambao ni Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini
Mhe. Mkapa akibadilishana mawazo na baadhi ya wajumbe wa mkutano mara baada ya shughuli ya ufunguzi kukamilika
Kutoka kulia ni Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Bi. Irene Khan na Mhe. Benjamin Mkapa wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukamilika kwa shughuli za ufunguzi
Rais Mstaafu Jakaya Kikwete wa pili kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Elizabeth wa kwanza kulia, Bi. Hamida Makame na Bw. Gerlad Mbwafu.


Picha ya pamoja kati ya Mgeni Rasmi, Mhe. Kairuki na wajumbe wa mkutano
Mhe. Kairuki akifafanua masuala mbalimbali kuhusu mkutano wa IDLO mbele ya waandishi wa habari.

Picha na Reginald Philip

Waziri Mahiga apokea Ujumbe Maalumu kutoka kwa Rais wa Angola.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt, Augustine Mahiga (Mb), akimpokea Mjumbe Maalumu wa Rais wa Angola, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mhe. Manuel Domingos Augusto leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam.
Waziri Mahiga akisalimiana na Balozi wa Angola nchini Tanzania, Mhe.Ambrosio Lukoki.
 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt, Augustine Mahiga (Mb), akiangalia bahasha iliyofungwa ujumbe maalumu kutoka kwa Rais wa Angola Mhe. Jose Eduardo Dos Santos, baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mhe. Manuel Domingos Augusto
 Waziri Mahiga akisisitiza jambo katika mazungumzo hayo ambayo yalijikita zaidi kwenye masuala mbalimbali kuhusu Jumuiya ya Nchi za Maziwa Makuu.
Sehemu ya Ujumbe wa Angola ulioambatana na Mhe. Manuel Domingos Augusto, kulia ni Balozi wa Angola nchini Tanzania Mhe.Ambrosio Lukoki.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo (kushoto), akifuatilia kwa makini mazungumzo hayo, pamoja na maofisa wa Wizara hiyo, Bi. Zulekha Tambwe (katikati) na Bw. Ally Kondo nao wakiendelea kurekodi kile kinachozungumzwa katika mazungumzo hayo.
                                                ==========================
Picha na Reuben Mchome.

Balozi Dora Msechu akutana na wafanyabiashara wa Sweden kuhamasisha biashara na uwekezaji.

Balozi wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu amefanya mkutano na wafanyabiashara wa Sweden ulioandaliwa na Baraza la Biashara la Sweden na Afrika Mashariki(SWEACC). 
 Mhe.Balozi Dora Msechu amewahamasisha Wafanyabiashara wa Sweden kuwekeza nchini Tanzania kwa kuwaeleza kwa kina fursa zilizopo pamoja na juhudi mahsusi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi ikiwa ni pamoja na mikakati kabambe ya kuimarisha sekta ya viwanda na kuboresha miundombinu.