Wednesday, February 8, 2017

Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho kutoka Mabalozi wa Burundi, Iran,Cuba, Zambia, Morocco na Saudi Arabia

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Burundi Mhe.Gervais Abayeho Ikulu Jijini Dar es Salaam


Rais Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Burundi nchini Tanzania Mhe. Gervais Abayeho. Wapili kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Mahiga na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Aziz P. Mlima (wakwanza kulia) wakifuatilia mazungumzo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania Mhe. Mousa Farhang Ikulu Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Mousa Farhang mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Mousa Farhang

Picha ya pamoja
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania Mhe. Lucas Domingo Harnandez Polledo Ikulu Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Tanzania Mhe. Lucas Domingo Harnandez Polledo  mara baada ya kuwasilisha Uati za Utambulisho

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Balozi Joseph Sokoine akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Cuba nchini Mhe. Lucas Domingo Harnandez Polledo mara baada ya kuwasilisha Uati za Utambulisho

Picha ya pamoja
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Zambia nchini Tanzania Mhe. Benson Keith Chali Ikulu Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kisiga akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Zambia nchini Tanzania Mhe. Chali mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho

Picha ya pamoja

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhiwa Hati za Utambulisho na  Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Abdelilah Benryane Ikulu Jijini Dar es Salaam

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kisiga akisalimiana na Balozi Ufalme wa Morocco Mhe. Benryane  mara baada ya kukabidhi Hati za Utambulisho

Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Morocco nchini Tanzania Mhe. Abdelilah Benryane mara baada ya kuwasilisha Hati za Utambulisho
Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek (katika) mwenye makazi yake Jijini Dar es Salaam akiwa amesimama wakati wimbo wa Taifa ukipigwa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Salaam kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martin

Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia Mhe. Al Malek akisaini kitabu cha wageni Ikulu Jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia Mhe. Mohamed Ben Monsour Al Malek Ikulu Jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi wa Ufalme wa Saud Arabia Mhe. Al Malek mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Aziz Mlima akisalimiana na Balozi wa Ufalme wa Saud Arabia Mhe. Al Malek mara baada ya kukabidhi hati za utambulisho

Picha ya pamoja

Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Ufalme wa Saudi Arabia nchini  Mhe. Al Malek mara baada ya kuwasilisha hati za utambulisho Ikuli Jijini Dar es Salaam


Tuesday, February 7, 2017

Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho wa Balozi Mteule wa Burundi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akipokea nakala ya hati za utambulisho kutoka kwa Balozi mteule wa Burundi Mhe. Gervais Abayeho




 Dkt. Mahiga akizungumza na Balozi Mhe. Abayeho mara baada ya kumaliza kupokea nakala za utambulisho.
Balozi mteule Mhe. Abayeho naye akielezea jambo kwa Dkt. Mahiga
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mteule kutoka Burundi Mhe. Abayeho (wa pili kutoka kushoto), Mkurugenzi Mkuu Idara ya Itifaki Balozi Grace Martine (Wa pili kutoka kulia) Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bwa. Suleiman Salehe (wa kwanza kushoto) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bwa. Eric Ngilangwa

Waziri Mahiga apokea nakala za hati za utambulisho za Mabalozi wateule wa Zambia na Cuba


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi mteule wa Zambia nchini Tanzania Mhe.Benson Keith Chali alipowasili Wizarani Jijini Dar es Salaam kukabidhi nakala za hati za utambulisho

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akipokea hati za utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Zambia nchini Tanzania Mhe. Chali

Waziri Mhe.Balozi Dkt. Mahiga na Balozi Mteule wa Zambia nchini Mhe. Chali wakiwa katika picha ya pamoja. Wa pili kulia ni Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Grace Martin, wa kwanza kulia ni Afisa kutoka Wizarani na kushoto ni Maafisa kutoka Ofisi za Ubalozi wa Zambia nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Balozi Mteule wa Cuba nchini Tanzania Mhe.Lucas Domingo Harnandez Pelledo mara baada ya kuwasili Wizarani kuwasilisha nakala za hati za utambulisho

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea nakala za hati za utambulisho kutoka Balozi Mteule wa Cuba nchini Tanzania Mhe.Lucas Domingo Harnandez Pelledo

Picha ya pamoja


Aidha, Waziri Mhe.Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na  Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Wizarani Jijini Dar es Salaam mapema leo asubuhi.Katika mazungumzo hayo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kidiplomasia, uchumi na kijamii baina ya nchi hizi mbili Tanzania na Burundi


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe walipokutana kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam



Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akizungumza


Waziri  Mhe. Mahiga akimsiliza Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe walipokuna kwa mazungumzo Wizarani Jijini Dar es Salaam

Monday, February 6, 2017

Rais Magufuli awaapisha Mabalozi wa Tanzania nchini Ufaransa na DRC

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimwapisha Balozi wa Tanzania Ufaransa Mhe.Samuel W. Shelukindo.
Sherehe za uapisho huo zimefanyika leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mhe. Rais Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Shelukindo.
Mhe. Rais Magufuli akimuapisha Luteni mstaafu Paul Ignace Mella kuwa Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mhe. Rais Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Mella.
Kutoka kulia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Kaimu Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Hamis Juma na Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Janeth Magufuli wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa Mabalozi na baadhi Wakuu wa Majeshi ya Ulinzi akiwemo Mkuu wa Jeshi ya Ulinzi nchini.
Kutoka kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba, Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Angella Kairuki pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Ussi Gavu wakifuatilia hafla ya uapisho. 
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima (wa pili kulia) akifuatilia sherehe za kuapishwa kwa Mabalozi na baadhi ya viongozi wa majeshi ya ulinzi. Pembeni yake  ni wageni waalikwa kutoka katika vyombo vya ulinzi wakifuatilia pia hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Idara ya  Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega (wa kwanza kulia) akifuatiwa na  Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Bw. Stephen Mbundi nao wakiwa Ikulu kwenye hafla ya kuapishwa Mabalozi
Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hafla ya uapisho. Kutoka  kushoto ni Balozi Abdallah Kilima, Balozi Baraka Luvanda na Balozi Innocent Shio.
Sehemu ya viongozi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wakifuatilia hafla ya kuapishwa kwa viongozi na Mabalozi
Mhe. Rais Magufuli akimpongeza Balozi Shelukindo mara baada ya kumalizika kwa tukio la kuapishwa.
Kushoto ni Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Grace Martin pamoja na Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Geofrey Pinda wakiratibu shughuli za Itifaki.
Picha ya pamoja Mhe. Rais Magufuli na Mabalozi mara baada ya kuwaapisha.

Picha ya pamoja Mhe. Rais Magufuli, Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Shein, Mawaziri, viongozi waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Viongozi wa majeshi na Mabalozi walioapishwa, 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Naibu Katibu Mkuu awatembelea Watanzania wanaoshikiliwa nchini Malawi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi amewasihi Watanzaniawananewanaoshikiliwa katika Gereza Kuu la Mzuzu nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani wa Kayerekera kuwa  wavumilivu wakati Serikali ikitafutaufumbuzi wa suala lao.

Balozi Mwinyi aliyasema hayo alipowatembelea gerezani ambapo katika ziara hiyo alifuatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma, Bw. Hassan Bendeyeko pamoja na maafisa wengine kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi.

Balozi Mwinyi aliwaeleza Watanzania hao kuwa mazungumzo katika ngazi mbalimbali kati ya Tanzania na Malawi yanaendelea na kuna matumaini makubwa kuwa hivi karibuni ufumbuzi wa suala lao unaweza kupatikana.
Balozi Mwinyi aliendekea kuekeza kuwa yeye na wenzake wamekuja Lilongwe kushiriki kikao cha Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi,   lakini wameamua kusafari  takriban kilomita 400 kutoka Lilongwe  hadi Mzuzu kuja kuwaona na kuwafikishia ujumbe kuwa Serikali inafanya jitihada kuhakikisha kuwa suala hili linapatiwa ufumbuzi kwa haraka.

"Nikufahamisheni kuwa jitihada katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo lenu zinaendelea na hata Mhe.  Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokutana na Rais wa Malawi, Mhe. Prof. Peter Mutharika pembezoni mwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika nchini Ethiopia jambo lenu lilikuwa moja ya masuala  waliyoyajadili.

Naibu Katibu Mkuu alisema kuwa alifarijika kuwakuta watu hao wote wapo salama na wenye afya nzuri na kuwajulisha kuwa ziara hiyo ya kuwatembelea na nyingine zilizofanyika siku za nyuma ni ushahidi dhahiri kwao na kwa Watanzania kwa  ujumla kuwa Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. Magufuli imedhamiria kuwahudumia Watanzania wote wa kada mbalimbali popote pale wanapoishi.

Watanzania hao wanane walikamatwa mwishoni mwa mwezi Desemba, 2016 na hadi sasa wanashikiliwa katika gereza kuu la Mzuzu. Watanzania hao ambao kati yao wawili ni wanawake  wamejitambulisha ni wakulima na wachimbaji wadogo wa madini wanatoka katika mkoa wa Ruvuma na walikwenda Malawi chini ya Taasisi ya CARiTAS kujifunza athari za migodi ya urani katika jamii.


Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe 05 Februari 2017

Tanzania na Malawi zasaini kushrikiana katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga akisoma hotuba ya kufunga kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi kilichofanyika Liolongwe. kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Ramadhan Mwinyi

Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Francis Kasaila akiwasilisha hotuba katika kikao cha JPCC kati ya Tanzania na Malawi

Wajumbe wa kikao cha JPCC wakifuatilia kwa makina hotuba za Mawaziri wa Mambo ya Nje zilipokuwa zinawasilishwa

Sehemu nyingine ya ujumbe ikifuatilia hotuba za Mawaziri

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Malawi na Tanzania wakiweka saini mikataba ya kushirikiana katika Mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga. Nyuma ya Waheshimiwa Mawaziri, kulia ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Bw. Mustafa Usi na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Malawi.

Waheshimiwa Mawaziri wakibadilishana mikataba baada ya kuisaini

Waziri Mahiga akisalimiana na wajumbe mbalimbali. Anayeshikana naye mkono ni Bi. Elizabeth Rweitunga, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje.

Picha ya pamoja kati ya Waheshimiwa Mawaziri na wajumbe walioshiriki kikao cha JPCC.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Malawi zasaini kushrikiana katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga

 Kikao cha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kimeweka mazingira mazuri ya kushughulikia mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa ambapo juhudi za kutafuta suluhu zilisimama kutokana na mabadiliko ya uongozi nchini Malawi.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt, Augustine Mahiga (Mb) wakati alipokuwa anasoma hotuba ya kufunga kikao hicho jijini Lilongwe siku ya Jumapili tarehe 05 Februari 2017.

Mhe. Waziri alieleza kuwa kikao hicho kimefanyika kufuatia maelekezo ya Waheshimiwa Marais wa Tanzania na Malawi ambao walifanya mazungumzo walipokuwa Ethiopia katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika na kutoa wito kwa jopo la viongozi wa zamani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuongeza kasi ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Jopo la viongozi wa zamani wa SADC lililopewa dhamana ya kushughulikia suala hilo linaundwa na Mhe. Joachim Chissano, Rais wa zamani wa Msumbiji; Mhe. Thabo Mbeki, Rais wa zamani wa Afrika Kusini  na Mhe. Festus Mogae, Rais wa zamani wa Botswana.

Waziri Mahiga alieleza kuwa japo Tanzania na Malawi zinatofautiana katika mpaka wa Ziwa Nyasa lakini tofauti hizo sio kikwazo kwa nchi hizo kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya faida ya wananchi wa pande zote mbili.
 Alisema kikao hicho cha JPCC kinatoa fursa kwa pande mbili kujadili na kukubaliana maeneo mbalimbali ya ushirikiano na kuweka utaratibu wa utekelezaji.

Aidha, katika kikao cha JPCC, wajumbe wanakitumia kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa maeneo ya ushirikiano yaliyoafikiwa.

 “Nafurahi kusikia mmejadili na kukubaliana maeneo mengi ya ushirikiano ikiwemo biashara, kilimo, utalii, tehama, utangazaji, utunzaji wa mazingira na usafiri wa anga”. “Ni jambo la kupongezwa katika majadiliano yenu pia mmependekeza iundwe Kamati ya Makatibu Wakuu ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi sita ili kutathmini utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa kwa mujibu wa muda uliokadiriwa”.  

Mhe. Mahiga alitoa maelezo namna Serikali ya Awamu ya Tano inavyoboresha miuondombinu ya Bandari ya Dar Es Salaam, barabara na mipango ya kuboresha Reli ya TAZARA kwa kushirikiana na China ili Malawi iweze kusafirisha bidhaa zake kwa urahisi.

“Ni jukumu letu na pia ni wajibu wa kimataifa kuzihudumia nchi zisizokuwa na bandari. Hivyo, Tanzania ambayo imezungukwa na nchi nane zisizokuwa na bandari itaboresha miundombinu ili nchi hizo ziweze kusafirisha bidhaa zao bila usumbufu wowote.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Francis Kasaila alisisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya bandari, barabra na reli ili Serikali ya Malawi na wafanyabiashara waweze kusafirisha bidhaa kwa urahisi. Alisema ili vituo vya mizigo vya Malawi vilivyopo Dar es Salaam na Mbeya vifanye kazi kwa ufanisi hakuna budi kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, Reli ya TAZARA, barabara ya Dar es Salaam hadi Mbeya na kujenga Kituo cha Pamoja cha kutoa Huduma mpakani.

Kikao hicho kilimalizika kwa kushuhudiwa uwekaji saini wa mikataba ya makubaliano katika Mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga.

Mhe. Waziri kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu amepangiwa miadi ya kuonana na Rais wa nchi hiyo, Mhe. Prof. Peter Mutharika ambapo amepanga pamoja na mambo mengine kujadili suala la Watanzania wanane wanaoshikiliwa katika gereza kuu la Mzuzu kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani wa Kayerekera.



Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe 06 Februari 2017