Friday, March 2, 2018

Tanzania yashiriki Mkutano wa Kwanza wa Global Dryland Alliance

Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma M. Rajab (wa kwanza kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe walioshiriki mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance. Balozi Rajab alimwakilisha  Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja iliyopo Doha, Qatar hivi karibuni. Umoja huo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2017  unaangalia namna ya kutatua majanga ya njaa yanayosababishwa na ukame, upungufu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa.
Kikao hicho kilizinduliwa rasmi na mwenyewe wa mkutano huo Mhe. Mohammed bin Abdullah Al Rumaihi Waziri wa Manispa na Mazingira wa Qatar. Na baadae kuendeshwa na Mwenyekiti mpya wa Umoja huo ambae pia ni Waziri wa Kilimo wa Benin.
Balozi Fatma M. Rajab akifuatilia  mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance Tanzania ambapo alimwakilisha, Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo umefanyika Kwenye Makao Makuu ya Umoja huo yaliyopo Doha, Qatar. 
Mkutano ukiendelea.
Wajumbe wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembelea jengo jipya la Makao Makuu ya Global Dryland Alliance mjini Doha.




Ubalozi wa Tanzania, The Hague wawapokea Wanafunzi wa Al Muntazir

Balozi wa Tanzania uliopo The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akizungumza na wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir ya Jijini Dar es Salaam walipomtembelea Ofisi kwake wakati wa ziara yao nchini humo ya kushirki Kongamano la Wanafunzi linalojulikana kama Farel Model United Nations-FAMUN 2018 lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Mwalimu Getrude Mtenga kwa ushiriki na uwakilishi mzuri wa Tanzania katika Kongamano la FAMUN 2018
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Bi. Zainab Sumar ambaye ni Mwanafunzi aliyepokea Tuzo ya "Best Delegate Award in ECOSOC at FAMUN 2018".
Mhe. Balozi Kasyanju akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi na Walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir waliotembelea Ubalozi hivi karibuni.
========================================================================
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTAZIR WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA THE HAGUE, UHOLANZI

Ubalozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi umewapokea Wanafunzi 10 na Walimu wawili (2) kutoka Shule ya Sekondari ya Almuntazir ya Jijini Dar es Salaam waliofika nchini Uholanzi kuhudhuria Kongamamo la Wanafunzi, linalojulikana kama Farel Model United Nations –FAMUN 2018, lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.

Wakiwa nchini Uholanzi, wanafunzi hao Fatima Jiwan, Zeinab Mehboob Pyarali Sumar, Saleha Munavarali Virani, Jeet Kirti Hirwania, Waqaas Mahsen Mahdi, Saloha Said Aboud, Sakina Mohamed Akhtar Walji, Kadhim Mahmood Kara, Zahra Imtiyaz Gulamhussein, Neha Dharmendra Makwana pamoja na walimu; Bibi Getrude Mtenga na Bi. Zainab Muslim Dharsee walipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo The Hague Uholanzi.

Kongamano la FAMUN hutoa fursa nzuri kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuongeza ujuzi wa kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa yanayoendelea ulimwenguni katika lugha ya Kiingereza, kujenga uwezo katika kufanya tafiti pamoja na kuunda urafiki mpya miongoni mwao. Ushiriki wa wanafunzi hao pia umeitangaza vizuri Tanzania kwenye Kongamano hilo.

PRESS RELEASE





Thursday, March 1, 2018

Waziri Mahiga akutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt Augustine Mahiga akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe alipomtembelea Wizarani, tarehe 1 Machi,2018, Dar es Salaam.

 Mhe. Waziri Mahiga,(Kulia) akizungumza jambo na Mhe. Waziri Nyamitwe katika mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine walizungumzia jinsi ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na nchi ya Burundi.
Balozi wa Burundi nchini Mhe. Balozi Gervais Abayeho (wa kwanza kushoto), akifuatilia mazungumzo hayo, wengine wanaofuatilia mazungumzo, kutoka kulia  ni , Bw. Suleiman Saleh, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Afrika. Bw. Wilbroad Kayombo na Bw. Erick Ngilangwa, Maafisa Mambo ya Nje,  na mwisho ni Katibu wa Waziri, Bw. Magabilo Murobi wakifuatilia mazungumzo hayo

Waziri Mahiga akiagana na mgeni wake Waziri Nyamitwe  baada ya kumaliza mazungumzo

Wednesday, February 28, 2018

Waziri Mahiga akutana na Mabalozi wa Vietnam na Japan waliopo nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Vietnam nchini, Mhe. Kim Nguyen Doanh. Katika mazungumzo yao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika masuala ya biashara na uwekezaji.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto) pamoja na Bw. Emmanuel Luangisa (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Mhe. Kim Nguyen Doanh (hawapo pichani)

.....Mkutano wa Waziri Mahiga na Balozi wa Japan

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Masaharu Yoshida. Mazungumzo yao yalijikita kwenye kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ya manufaa kwa nchi hizi mbili. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Celestine Mushy akifafanua jambo wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Mahiga na Balozi wa Japan nchini, Mhe. Yoshida (hawapo pichani). Wengine katika picha ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Justa Nyange (kushoto)  Bw. Abdallah Kirungu (katikati), Afisa Mambo ya Nje na Bw. Magabilo Murobi (kulia), Katibu wa Waziri.


Mhe. Balozi Simba afunga mafunzo kwa Maafisa wa polisi



Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, ambaye pia alikuwa mgeni rasmi, Mhe. Balozi Hassan Y. Simba akisoma hotuba ya kufunga mafunzo ya siku tatu ya Maafisa wa Polisi, Mafunzo hayo yemetolewa na chuo cha mambo ya usalama cha Naif Arab University for Security Science, hafla hiyo imefanyika tarehe 28 Februari,2018, katika Hotel ya Hyatt Regency, Dar es Salaam.
 Balozi wa Tanzania nchini Saud Arabia, Mhe. Balozi Hemed Mgaza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje katika hafla hiyo.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Balozi Hassan Y. Simba (katikati), Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia , Mhe. Balozi Hemed Mgaza (kulia), anayefuata ni Kamishna wa Operesheni na Mafunzo Jeshi la Polisi, Commandor Nsato Marijani. wa pili kutoka mwisho kushoto ni Balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek wakifuatilia shughuli hiyo.
Sehemu ya wageni wakifuatilia ufunguzi huo.
    
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo Bw. Hangi Mgaka akipokea cheti katika hafla hiyo
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Ramadhani M. Mwinyi akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek 
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Mhe. Balozi Hassan Y. Simba akipokea zawadi kutoka kwa Balozi wa Saudi Arabia nchini, Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek 



Picha ya pamoja

Tuesday, February 27, 2018

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana kwa mazungumzo na Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya MICT

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiwa kwenye mazungumzo na Mhe. Olufemi Elias, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Msajili wa Mahakama ya Kimataifa ya Masalia ya kesi za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (Mechanism for International Criminal Tribunals-(MICT) iliyopo Jijini Arusha. Pamoja na mambo mengine Mhe. Elias aliipongeza Serikali ya Tanzania kwa kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Mahakama hiyo pia walizungumzia umuhimu wa Mahakama hiyo hapa nchini.
Mkutano ukiendelea.


Monday, February 26, 2018

Wizara ya Mambo ya Nje yaahidi kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa vitendo

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akitoa taarifa ya ufunguzi katika kikao cha Wizara na wadau kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam tarehe 26 Februari 2016.

 Lengo la kikao hicho ni kujadili maandalizi ya maonesho ya bidhaa za viwanda vya Tanzania yanayotarajia kufanyika Nairobi, Kenya kuanzia tarehe 25 hadi 28 Aprili 2018 ambayo yanatarajiwa kwenda sambamba na sherehe za Siku ya Tanzania (Tanzania day) ambayo husherehekewa tarehe 26 Aprili 2018 siku ya Muungano. Maonesho hayo ni njia mojawapo za kutekeleza Diplomasia ya Uchumi inayosisitiza katika kukuza biashara, utalii na uwekezaji.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana akizungumza. Balozi Chana alieleza kuwa Ofisi za Ubalozi zimejidhatiti kuhakikisha zinasimamia fursa zote za Watanzania hususan masuala ya biashara ili kuweza kuleta mageuzi ya kiuchumi kwa Taifa na Watanzania kwa ujumla.
Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi kuhusiana na maonyesho iliyokuwa ikiwasilishwa na Prof. Adolf Mkenda (hayupo pichani). Kutoka kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bw. Juma Ali Juma, Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Mhe. Pindi Chana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo  ya Biashara (TANTRADE), Bw.  Edwin Rutageruka.
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa meza kuu wakifuatilia taarifa ya ufunguzi. Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof. Joseph Buchweishaija, Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Anisa Mbega, Mkurugenzi Mtendaji-Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Bw. Godfrey Simbeye na Mwakilishi kutoka Chama cha Wafanyabiashara, Wakulima na wenye Viwanda Tanzania (TCCIA), Bw. Godfrid Muganda.
Wajumbe kutoka Serikalini na sekta binafsi wakifuatilia kikao. Waliokaa mstari wa kwanza  ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Suleiman Salehe. 
Wajumbe wakifuatilia kikao. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga na nyuma yake ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Bertha Makilagi.
Wajumbe wakifuatilia kikao.

Sehemu nyingine ya wajumbe wakifuatilia kikao.

Naibu Katibu Mkuu afungua mafunzo ya Maafisa wa Polisi

 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani M. Mwinyi, akifungua mafunzo ya Maafisa wa Polisi yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es salaam, mafunzo hayo yanaendeshwa na Wataalam kutoka chuo cha sayansi ya masuala ya Ulinzi Cha Naif Arab University cha Saud Arabia. Mafunzo hayo ni ya siku tatu(3), yaliyoanza tarehe 26-28 Februari,2018
Naibu Katibu Mkuu Balozi Mwinyi, kushoto kwake  ni Balozi Mohamed M. Al Malek , Balozi wa Saudi Arabia Nchini, kulia kwake ni , Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia, Balozi Hemedi Mgaza na mwisho ni Kamishna wa Operesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi Commissioner Nsato M. Marijani  wakifuatilia mafunzo hayo.


Mafunzo yakiendelea
 
Sehemu ya washiriki kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo

 Sehemu ya washiriki  na Wakufunzi wa mafunzo wakifuatilia mafunzo hayo
    Picha ya Pamoja.

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Mwakilishi wa Taasisi ya Aga Khan

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi wa masuala ya Diplomasia katika Taasisi ya Aga Khan, Balozi Arif Lalani.Katika mazungumzo yao walijadili kuhusu ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Taasisi hiyo katika sekta ya Elimu na Afya. Mazungumzo hayo ambayo yalihudhuriwa na Bw. Amin Kurji alieambatana na Balozi Lalani yalifanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam.   
Balozi Lalani akimweleza jambo Prof. Mkenda.
Mazungumzo yakiendelea.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Mkenda akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Lalani (wa tatu kushoto), Bw. Kurji (wa tatu kulia), Kaimu Mkurugenzi Kitengo cha Sheria, Bibi Caroline Chipeta (wa pili kulia), Katibu wa Katibu Mkuu, Bi. Bertha Makilagi (wa kwanza kushoto) na Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Elisha Suku.