Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma M. Rajab (wa kwanza kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wajumbe walioshiriki mkutano wa kikao cha Kwanza cha Wajumbe wa Global Dryland Alliance. Balozi Rajab alimwakilisha Mhe. Dkt. Charles Tizeba, Waziri wa Kilimo. Mkutano huo ulifanyika kwenye Makao Makuu ya Umoja iliyopo Doha, Qatar hivi karibuni. Umoja huo ambao ulianzishwa rasmi mwaka 2017 unaangalia namna ya kutatua majanga ya njaa yanayosababishwa na ukame, upungufu wa mvua na mabadiliko ya hali ya hewa. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.