Friday, March 2, 2018

Ubalozi wa Tanzania, The Hague wawapokea Wanafunzi wa Al Muntazir

Balozi wa Tanzania uliopo The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akizungumza na wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir ya Jijini Dar es Salaam walipomtembelea Ofisi kwake wakati wa ziara yao nchini humo ya kushirki Kongamano la Wanafunzi linalojulikana kama Farel Model United Nations-FAMUN 2018 lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Mwalimu Getrude Mtenga kwa ushiriki na uwakilishi mzuri wa Tanzania katika Kongamano la FAMUN 2018
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Bi. Zainab Sumar ambaye ni Mwanafunzi aliyepokea Tuzo ya "Best Delegate Award in ECOSOC at FAMUN 2018".
Mhe. Balozi Kasyanju akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi na Walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir waliotembelea Ubalozi hivi karibuni.
========================================================================
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTAZIR WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA THE HAGUE, UHOLANZI

Ubalozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi umewapokea Wanafunzi 10 na Walimu wawili (2) kutoka Shule ya Sekondari ya Almuntazir ya Jijini Dar es Salaam waliofika nchini Uholanzi kuhudhuria Kongamamo la Wanafunzi, linalojulikana kama Farel Model United Nations –FAMUN 2018, lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni.

Wakiwa nchini Uholanzi, wanafunzi hao Fatima Jiwan, Zeinab Mehboob Pyarali Sumar, Saleha Munavarali Virani, Jeet Kirti Hirwania, Waqaas Mahsen Mahdi, Saloha Said Aboud, Sakina Mohamed Akhtar Walji, Kadhim Mahmood Kara, Zahra Imtiyaz Gulamhussein, Neha Dharmendra Makwana pamoja na walimu; Bibi Getrude Mtenga na Bi. Zainab Muslim Dharsee walipata fursa ya kutembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo The Hague Uholanzi.

Kongamano la FAMUN hutoa fursa nzuri kwa wanafunzi wa shule za sekondari kuongeza ujuzi wa kuendesha mijadala kuhusu masuala mbalimbali ya kimataifa yanayoendelea ulimwenguni katika lugha ya Kiingereza, kujenga uwezo katika kufanya tafiti pamoja na kuunda urafiki mpya miongoni mwao. Ushiriki wa wanafunzi hao pia umeitangaza vizuri Tanzania kwenye Kongamano hilo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.