|
Balozi wa Tanzania uliopo The Hague, Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju akizungumza na wanafunzi na walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir ya Jijini Dar es Salaam walipomtembelea Ofisi kwake wakati wa ziara yao nchini humo ya kushirki Kongamano la Wanafunzi linalojulikana kama Farel Model United Nations-FAMUN 2018 lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi hivi karibuni. |
|
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Mwalimu Getrude Mtenga kwa ushiriki na uwakilishi mzuri wa Tanzania katika Kongamano la FAMUN 2018 |
|
Mhe. Balozi Kasyanju akimpongeza Bi. Zainab Sumar ambaye ni Mwanafunzi aliyepokea Tuzo ya "Best Delegate Award in ECOSOC at FAMUN 2018". |
|
Mhe. Balozi Kasyanju akiwa kwenye picha ya pamoja na Wanafunzi na Walimu kutoka Shule ya Sekondari ya Al Muntazir waliotembelea Ubalozi hivi karibuni. |
|
========================================================================
WANAFUNZI WA
SHULE YA SEKONDARI YA ALMUNTAZIR WATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA THE HAGUE,
UHOLANZI
Ubalozi wa Tanzania, The Hague, Uholanzi umewapokea Wanafunzi 10 na Walimu wawili (2) kutoka
Shule ya Sekondari ya Almuntazir ya Jijini Dar es Salaam waliofika nchini Uholanzi kuhudhuria Kongamamo
la Wanafunzi, linalojulikana kama Farel
Model United Nations –FAMUN 2018, lililofanyika Mjini Amersfoort, Uholanzi
hivi karibuni.
Wakiwa nchini Uholanzi, wanafunzi hao Fatima Jiwan,
Zeinab Mehboob Pyarali Sumar, Saleha Munavarali Virani, Jeet Kirti Hirwania,
Waqaas Mahsen Mahdi, Saloha Said Aboud, Sakina Mohamed Akhtar Walji, Kadhim
Mahmood Kara, Zahra Imtiyaz Gulamhussein, Neha Dharmendra Makwana pamoja na
walimu; Bibi Getrude Mtenga na Bi. Zainab Muslim Dharsee walipata fursa ya
kutembelea Ubalozi wa Tanzania uliopo The Hague Uholanzi.
Kongamano la FAMUN hutoa fursa nzuri kwa wanafunzi wa
shule za sekondari kuongeza ujuzi wa kuendesha mijadala kuhusu masuala
mbalimbali ya kimataifa yanayoendelea ulimwenguni katika lugha ya Kiingereza,
kujenga uwezo katika kufanya tafiti pamoja na kuunda urafiki mpya miongoni
mwao. Ushiriki wa wanafunzi hao pia umeitangaza vizuri Tanzania kwenye
Kongamano hilo.