TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
FURSA
ZA UFADHILI WA MAFUNZO KWA WATANZANIA
Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda
mfupi na muda mrefu katika kada mbalimbali kutoka Umoja wa Afrika, Serikali za China,
Ujerumani na Jamhuri ya Korea.
Kuhusu ufadhili wa mafunzo ya muda
mrefu, Umoja wa Afrika kupitia Mwalimu
Nyerere African Union Scholarship Scheme umetoa ufadhili wa mafunzo kwa
ngazi ya Shahada ya Uzamili na Uzamivu (PhD) kwenye masuala ya Sayansi,
Teknolojia, Uhandisi na Hesabu (STEM). Waombaji wa mafunzo haya ni wanawake
pekee wenye umri wa miaka isiyozidi 35 kwa mafunzo ya ngazi ya Shahada ya Uzamili
na miaka isiyozidi 40 kwa mafunzo ya ngazi ya Shahada ya Uzamivu (PhD). Maelezo
ya ziada kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia tovuti ya http://www.au.int. au maombi yatumwe kwa OlgaA@african-union.org na nakala
kwa mwalimunyerere@africa-union.org. Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 30 Aprili, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma.
Aidha, Baraza la Ufadhili wa
Mafunzo la China limetoa nafasi za ufadhili wa mafunzo ya muda mrefu. Maelezo
kuhusu mafunzo haya yanapatikana kupitia http://www.esc.edu.cn. Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 30 Aprili, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara
ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora.
Vilevile, Serikali ya China imetoa fursa ya ufadhili wa
mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili katika masuala ya Utawala
na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Nadharia ya Uchumi na Maendeleo ya Taifa.
Maelezo ya ziada ya kozi hizi yanapatikana kupitia http://www.isscad.pku.edu.cn. Pia
maombi yatumwe kupitia http://www.administration@isscad.pku.edu.cn. Mwisho
wa kutuma maombi ni tarehe 30 Mei, 2018. Mafunzo haya yanaratibiwa na Wizara ya
Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa pamoja na Ofisi ya Rais, Menejimentii ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Wakati huohuo, Serikali ya China
imetoa fursa za ufadhili wa mafunzo kwa wataalam wa kilimo kutoka Tanzania.
Mafunzo haya yatafanyika Beijing, China. Mratibu wa mafunzo haya ni Wizara ya
Kilimo na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Kwa upande mwingine, Wizara
imepokea nafasi za mafunzo ya muda mfupi kutoka Serikali ya Ujerumani katika
Kozi ya Stashahada ya Juu ya Usimamizi wa Mazingira kwa Nchi Zinazoendelea (International Postgraduate Course on
Environmental Management for Developing Countries). Mafunzo haya
yatafanyika Ujerumani kuanzia tarehe 10 Januari, 2019 hadi tarehe 12 Julai,
2019. Mafunzo haya yanaratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais, (Mazingira) na
Baraza la Mazingira (NEMC).
Pia, Jamhuri ya Korea kupitia
Program ya Dkt. Lee Jong-Wook imetoa nafasi mbili za ufadhili wa masomo ya muda
mfupi kwa wataalam wa tiba kwa kipindi cha kati ya miezi 2 hadi 12. Mafunzo
haya yanaratibiwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
06 Aprili, 2018
|
Friday, April 6, 2018
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Waziri Mahiga aongoza kumbukumbu za Wataalam wa Kichina waliokufa wakati wa ujenzi wa Reli ya TAZARA
Dkt. Mahiga pamoja na Viongozi mbalimbali kutoka Serikalini wakitoa heshima zao kwa kuinamisha vichwa kama ishara ya kuwakumbuka wataalam hao kutoka China. |
Dkt. Mahiga akiweka Ua katika moja ya kaburi la wataalam hao.Wanaoshuhudia ni Balozi wa China, Mhe. Wang Ke, Prof. Palamagamba Kabudi, Bw. Joseph Butiku na viongozi wengine. |
Naye Balozi Wang Ke naye akitoa hotuba yake wakati wa hafla hiyo. |
Dkt. Mahiga akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kumaliza hafla hiyo. |
Dkt. Mahiga akiweka saini kwenye kitabu cha kumbukumbu ya vifo vya wataalam hao. |
Thursday, April 5, 2018
Waziri Mahiga akutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Shelisheli na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ugiriki
Ujumbe ulioambatana na Balozi Faure kutoka kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa nchi hiyo Bw. Frank Ally, Kamishina Mkuu wa Polisi wa nchi hiyo Bw. Krishnan Labonte wakifuatilia mazungumzo hayo. |
Dkt. Mahiga akiagana na Balozi Faure mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. |
Mhe. Mahiga na mgeni wake Balozi Faure, wakiwa katika picha ya pamoja |
Waziri Mahiga akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ugiriki
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Ugiriki Mhe. Terens Quicq (kushoto), mazungumzo hayo yalifanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara tarehe 05 Aprili,2018, Dar es Salaam. Mhe. Quicq aliwasili hapa nchini tarehe 04 Aprili,2018
Pamoja na mambo mengine mazungumzo yalijikita katika kukuza zaidi mahusiano kati ya Tanzania na Ugiriki hasa katika biashara na Uwekezaji katika maeneo ya viwanda vya kuzalisha madawa ya binadamu na wanyama,nishati na utalii.
Ujumbe uliongozana na Mhe. Quicq, kutoka kulia ni Balozi wa Ugiriki nchini Tanzania mwenye makazi yake nchini Kenya, Mhe. Balozi Konstantinos Moatsos(Kulia), Balozi wa Heshima Bw.William K. Ferentinos(katikati) na Bi. Maya Solomou kutoka Ubalozi wakifuatilia mazungumzo hayo.
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo .
Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akimkaribisha Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Balozi Sara Catherine cooke, alipomtembelea Wizarani kwa ajili ya mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Mkutano wa Wizara tarehe 4 Aprili,2018, Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo pamoja na mambo mengine yalijikita kwenye ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Serikali na nchi za Umoja wa Madola (CHOGM), Mkutano huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 16-20, Jijini London, Uingereza.
Prof. Mkenda akifafanua jambo kwa Balozi Sarah Cooke katika mazungumzo hayo.
Mazungumzo yakiendelea, wanaofuatilia mazungumzo hayo ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy(katikati kulia), anayefuata ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Bw. Deusdedit Kaganda na wa mwisho kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi Bw. Mark Thayre.
Wednesday, April 4, 2018
Katibu Mkuu akutana na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Japan
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda(Kulia) akifafanua jambo kwa Kaimu Balozi wa Japan nchini Bw. Hiroyuki Kubota katika mazungumzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara, Dar es Salaam, tarehe 03 Aprili,2018.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kuboresha mahusiano ya Tanzania na nchi ya Japan. Prof. Mkenda alisema Mahusiano ya Tanzania na Japan ni ya Kihistoria na katika kuendelea kudumisha mahusiano haya na kwa kuzingatia Japan ni kati ya nchi zinazosifika katika Teknolojia mbalimbali za kisasa, aliwakaribisha kuongeza uwekezaji katika eneo hilo. Naye Bw. Kubota aliahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali hasa katika kujenga uwezo wa wataalamu wa Tanzania ili kuweza kushiriki vyema katika uchumi wa Viwanda.
Mazungumzo yakiendelea, wanaofuatilia mazungumzo hayo kutoka kushoto ni Maafisa kutoka Ubalozi wa Japan na kulia ni Maafisa kutoka Wizarani.
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo
Tuesday, April 3, 2018
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda akutana kwa mazungumzo na Balozi wa China nchini
Mwalimu Mroso akimshukuru Balozi Wang Ke kwa mchango waliotoa kwa ajili ya kuisaidia Shule ya Msingi Msinga iliyopo Moshi Vijijini. |
Maafisa kutoka Ubalozi wa China. |
Balozi Shiyo na Balozi Wang Ke wakiwa katika picha ya pamoja na Mwalimu Mroso (wa tatu kushoto) pamoja na wajumbe wengine walioshiriki mazungumzo |
Mazungumzo yakiendelea |
Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi zasaini Mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Mhe. Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (Kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, wakisaini Mkataba wa Mkopo wenye Masharti nafuu wa kiasi cha shilingi bilioni34 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Uvinza hadi Malagarasi, yenye urefu wa Kilometa 31, kwa kiwango cha lami.
Mhe. Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe (Kushoto), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi, Mhe. Saif Al Suwaidi, (Kushoto),wakionesha mkataba huo baada ya kusainiwa.
Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi zasaini Mkopo wa masharti nafuu
TANZANIA
NA MFUKO WA MAENDELEO WA ABU DHABI ZASAINI MKOPO WA MRADI WA UJENZI WA BARABARA
YA UVINZA-MALAGARASI YA MKOANI KIGOMA
Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi leo
tarehe 02 Aprili, 2018 zimesaini mkataba wa mkopo nafuu wa Dola za Kimarekani
milioni 15 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa barabara ya Uvinza-Malagarasi yenye
urefu wa kilometa 51.
Hafla
fupi ya uwekaji saini wa mkataba huo imefanyika katika makao makuu ya mfuko huo
yaliyopo Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) ambapo Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa amesaini kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na Mhe. Mohamed Saif Al Suwaidi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa
Abu Dhabi amesaini kwa niaba ya Mfuko
huo.
Kusainiwa
kwa mkataba huo ni mwendelezo wa ushirikiano baina ya Tanzania na mfuko huo baada ya kukamilika kwa
awamu ya kwanza ya barabara ya Kidahwe-Uvinza (KM 77) ambayo pia ilifadhiliwa
na mfuko huo kwa mkopo nafuu wa Dola za Kimarekani milioni 57. Hivyo,
kukamilika kwa barabara ya Uvinza –Malagarasi kutaunganisha Daraja la
Malagarasi (Kikwete Bridge) ikiwa ni azma ya Serikali ya kuunganisha barabara
za Kigoma, Tabora hadi Manyoni (Singida) ambapo pia itaiunganisha nchi jirani
za Burundi na Kongo DRC.
Akizungumza
baada ya kusaini mkataba huo, Mhandisi Iyombe amesema kuwa, Serikali ya Awamu
ya Tano imedhamiria kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati kwa kuimarisha
miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara ambapo kusainiwa kwa mkataba huo ni
ishara mojawapo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo wa Abu Dhabi kwa upande wake amesema kuwa Mfuko huo
uko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo nchini hususan katika kipindi hiki ambapo Serikali ya
Tanzania imeidhihirishia dunia umakini katika kutekeleza miradi mikubwa ya
maendeleo kwa kufufua nidhamu ya fedha; kupambana na rushwa pamoja na
uwajibikaji kwa manufaa ya watanzania.
Balozi
Mbarouk alisema kuwa, UAE ina fursa nyingi sana katika uchumi ambapo Tanzania
inaweza kunufaika nazo hususan kwenye upande wa uwekezaji, biashara na utalii. Tanzania inaweza kupata wawekezaji wakubwa kutoka UAE; kupata soko
la bidhaa zake hususan mazao ya kilimo na mifugo pamoja na kukuza utalii
kupitia familia za kifalme zinazokuja kutalii nchini lakini kwa kuvutia watalii
wanaotembelea huku hususan Dubai ili waje pia Tanzania. “Hii yote
inawezekana kutokana na mahusiano mazuri yalipo baina ya Tanzania na Umoja wa
Falme za Kiarabu yanayoendelea kukua siku hadi siku” …alisema Balozi Mbarouk.
MWISHO,
02
Aprili, 2018
ABU
DHABI, UMOJA WA FALME ZA KIARABU
Thursday, March 29, 2018
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Subscribe to:
Posts (Atom)