TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania
kushiriki Maonesho ya Biashara ya Dunia ya EXPO 2020
Tanzania
itashiriki Maonesho ya Dunia ya Biashara (Expo 2020 yatakayofanyika Dubai
kuanzia mwezi Oktoba
2020 na kumalizika mwezi April 2021.
Uwekaji
saini wa Mkataba wa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho hayo ulifanywa tarehe
16 Januari 2019 na Balozi wa
Tanzania nchini UAE ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa Tanzania wa DUBAI EXPO 2020,
Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk.
Kwa upande wa UAE, mkataba huo uliwekwa saini na
Mkurugenzi wa DUBAI EXPO 2020, Mhe. Najeeb Mohammed Al Ali.
Baada
ya uwekaji saini wa Mkataba huo, Mhe. Balozi Mbarouk alieleza kuwa Serikali
inayapa umuhimu mkubwa maonesho hayo kwa kuwa ni fursa adhimu ya kuitangaza
Tanzania kwenye sekta za uwekezaji, biashara, viwanda, utalii na mila na
utamaduni.
Aidha,
Mkurugenzi wa DUBAI EXPO
2020 alieleza kuwa amefurahishwa na hatua ya Tanzania kusaini Mkataba huo ambapo
itatoa fursa kwa nchi kujiandaa mapema
na taratibu nyingine za ushiriki.
Baada
ya uwekaji saini wa Mkataba huo,` kitakachofuata ni utayarishaji wa simulizi ya
maudhui ya maonesho (pitch story) ambayo inatakiwa kuthibitishwa na Kamati ya
Kitaifa ya Tanzania ya DUBAI Expo 2020. Simulizi ya maudhui hayo yatahusu
vipaumbele vya Tanzania kama vile maendeleo ya viwanda, miundombinu, masuala ya
biashara na uwekezaji, utalii, kilimo, elimu, afya, sanaa na utamaduni. Simulizi ya maudhui pia itatumika katika kusanifu
muonekana wa banda la maonesho la Tanzania.
Tanzania inakuwa miongozi mwa nchi washiriki
zipatazo 100 ambazo tayari zimesaini Mkataba wa Ushiriki tangu Dubai ilipochaguliwa
kuwa mwenyeji wa maonensho hayo.
Wengine walioshuhudia uwekaji saini wa Mkataba huo
ni Bw. Ali Jabir Mwadini, Kansela Mkuu, Ubalozi Mdogo wa Tanzania, Dubai; Bi Samira
Ahmed Diria, Afisa Ubalozi; na kwa upande wa DUBAI EXPO 2020 ni Bi Manuela Garcia Pascual, Mkurugenzi wa Washiriki
wa Kimataifa na Bi. Esther Omondi, Meneja wa Nchi/Afisa dawati la Tanzania.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
17 Januari
2019
|