Uongozi wa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini Uganda wakiwa katika picha ya pamoja. |
Monday, October 14, 2019
Wanafunzi Uganda Wafanya Mdahalo kuhusu Mwalimu Nyerere
Sunday, October 13, 2019
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAKABIDHIWA JENGO JIPYA NA CHINA
Balozi wa China hapa Nchini, Balozi Wang Ke akisoma hotuba yake wakati wa makabidhiano ya jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es salaam |
Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki wamalizika Jijini Arusha.
12 Oktoba 2019, Arusha.
Mkutano wa 30 wa Baraza la
kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango
umemalizika tarehe 12 Oktoba 2019 kwenye Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Jijini Arusha - Tanzania. Mkutano huu wa siku sita (06) umefanyika
katika Ngazi zifuatazo:
- Mkutano
katika Ngazi ya Maafisa Waandamizi tarehe 7 na 8 Oktoba, 2019;
- Mkutano
katika Ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 9 na 10 Oktoba 2019 na
- Mkutano
katika Ngazi ya Mawaziri tarehe 11 na 12 Oktoba 2019.
Ujumbe wa Tanzania katika
mkutano huu umeongozwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb) akisaidiana na Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent L. Bashungwa (Mb); Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb); Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaju (Mb); Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mary Mwanjelwa
pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Mkutano huu umetoa maamuzi na
maelekezo mbalimbali ya kisera na kimkakati kwa Nchi Wanachama pamoja na
Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Utekelezaji wa
maamuzi na maelekezo ya mikutano ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki iliyopita pamoja na mkutano wa 10 hadi 28
wa Baraza la kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya
Afrika Mashariki na Mipango; Utekelezaji wa Soko la pamoja la Afrika Mashariki; Utekeleaji
wa maagizo katika taarifa ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (2000 –
2017); Vipaumbele vya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2020/21; Maelekezo
kuhusiana na mikutano ya Wakuu wa taasisi za masuala ya Uhamiaji na Kazi za
Jumuiya, na maagizo ya hadidu za rejea za maandalizi ya mkakati wa mpango wa
sita wa maendeleo ya Afrika Mashariki (2021/22).
Aidha, mkutano huu ulitoa mapendekezo katika taarifa
ya hali ya ulipaji wa michango ya Nchi Wanachama katika Jumuiya; Taarifa ya uhamasishaji
katika masuala ya rasilimali za jumuiya ya Afrika Mashariki na mikakati ya
ushirikiano; Taarifa ya Tume ya Ukaguzi ya Jumuiya kwa mwaka 2017/18; Taarifa
ya maendeleo ya makubaliano ya maeneo huru ya biashara katika utatu wa
COMESA-EAC-SADC;Taarifa ya maendeleo ya makubaliano kuhusu eneo huru la
kibiashara barani Afrika (AFCFTA); Taarifa ya maendeleo ya masuala ya kisiasa,
na Kalenda ya majukumu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha mwezi
Julai hadi Desemba 2019.
Vilevile, wajumbe wa mkutano wamejadili
kuhusiana na maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa jumuiya
ya Afrika Mashariki mwaka 2000, baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya awali
iliyoundwa mwaka 1967 na kuvunjika mwaka 1977.
Saturday, October 12, 2019
Watalii kutoka Israel wawasili nchini kwa ziara ya siku nane.
Sehemu nyingine ya Watalii kutoka nchini Israel wakipata huduma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. |
Kikundi cha ngoma cha Wamasai kikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kuwalaki wageni hao. |
Friday, October 11, 2019
Madereva wa taxi kutoka Uingereza wapanda Mlima Kilimanjaro
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke akizungumza katika hafla hiyo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Dkt. Devota Mdachi na Kiongozi wa Madereva wa Taxi wakiweka saini MoU. |
| ||
|
Timu ya Madereva kutoka Uingereza ikipanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya maveterani wa kijeshi (military veterans) huko Uingereza. |
Timu ya Madereva wa Taxi kutoka Uingereza ikiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak). |
Thursday, October 10, 2019
TAARIFA KWA UMMA
UJIO WA WATALII ZAIDI YA 1000 KUTOKA ISRAEL
Tanzania inatarajia kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mwezi huu wa Oktoba.
Kundi la kwanza lililokuwa na zaidi ya watalii 200 liliwasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 na kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Watalii wengine zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu baada ya Makampuni ya Uwakala wa Utalii kukamilisha taratibu za safari zao.
Watalii hao wanatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar, Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuitangaza nchi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa kushirikiana na wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi.
Tanzania imejipanga kuwapokea na kuwatembeza watalii hao katika vivutio vya utalii vilivyoko nchini. Serikali inawakaribisha watalii hao kutembelea vivutio hivyo vya utalii ambavyo nchi imebarikiwa kuwa navyo ili wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania nchini kwao na kwingine watakakokwenda.
Imetolewa na:
Dkt. Faraji K. Mnyepe
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
DODOMA
PROF. KABUDI AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA HISPANIA HAPA NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini. Kulia kwa Prof. Palamagamba John Kabudi ni Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero. |
Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi huyo hapa Nchini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akigongeana glasi ishara ya kutakiana kheri na Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero,wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini. |
Baadhi ya waalikwa walihohudhuria maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini. |
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu. Mkutano katika ngazi hiyo ulikuwa wa siku mbili na umemalizika leo. Pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 11 na 12 Oktoba 2019. Pichani; wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka Rwanda, Balozi Richard Masozera akiongoza mkutano huo, wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Miundombinu, Mhandisi Steven D. M. Mlote, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia sekta za uzalishaji na jamii, Mhe. Christophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara inayoshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kenya, Bw. Rafael Kanoth. |
Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akisaini taarifa ya mapendekezo mbalimbali katika mkutano huo kwaajili ya kuwasilisha taarifa hiyo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri. Pembeni yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akishuhudia zoezi la utiaji saini. |
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban pamoja na Dkt. Ndumbaro na Prof. Mchome wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo. |
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen P. Mbundi pamoja na wajumbe wengine wa mkutano wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo. |
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (kushoto) pamoja na sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wakifuatilia majadiliano. |
Sehemu nyingine ya wajumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano katika mkutano. |
Viongozi wa ujumbe wa mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wakikamilisha zoezi la utiaji saini wa taarifa ya mapendekezo ya mkutano huo. |
Wednesday, October 9, 2019
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WAANZA MAJUKUMU YA UENYEKITI WA KUNDI LA MABALOZI KUTOKA NCHI ZA SADC WALIOPO NCHINI HUMO
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akipokea Makabrasha kutoka kwa Balozi wa Namibia nchini India, Mhe. Gabriel P. Sinimbo ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa Kundi la Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC ) waliopo India. Tanzania ilipokea uenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Namibia mwezi Agosti 2019 wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika jijini Dar es Salaam.
|
Balozi Luvanda (katikati) akizungumza mara baada ya kupokea uenyekiti wa kundi la Mabalozi kutoka Nchi za SADC waliopo India. Katika picha ni Balozi Sinimbo (kulia) kutoka Namibia na Balozi E.A Ferreira (kushoto) kutoka Msumbiji. |
Mkutano ukiendelea |
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na na
Mabalozi kutoka nchi za SADC waliopo India pamoja na Maafisa wa Ubalozi mara baada ya kikao
cha Mabalozi hao kilichofanyika kwenye Jengo la Ubalozi jijini New Delhi.
|
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Zambia nchini India, Mhe. Judith K. Kapijimpanga ambaye kabla ya kuiwakilisha
Zambia nchini India alihudumu katika nafasi hiyo nchini Tanzania.
|
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, Dkt. Kheri Goloka (kushoto) na Bi. Natihaika Msuya (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa kundi la Mabalozi wa nchi za SADC nchini India aliyemaliza muda
wake Balozi wa Namibia Mhe. Gabriel P. Sinimbo.
|
Monday, October 7, 2019
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango.
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango umefunguliwa leo kwenye Ukumbi wa Mikutano uliopo katika Jengo la Jumuiya ya Afrika Mashariki, jijini Arusha na utafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 12 Oktoba 2019. Mkutano huo unaanza na vikao vya awali ambavyo ni kikao cha Maafisa Waandamizi kinachofanyika tarehe 7 na 8 Oktoba 2019 na utafuatiwa na kikao ngazi ya Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 9 na 10, na kumalizia na ngazi ya Mawaziri tarehe 11 na 12 Oktoba 2019. Pichani; Wapili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa kikao cha ngazi ya Wataalamu na Afisa Mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kutoka Jamhuri ya Rwanda, Bw. Emmanuel Kamugisha akiongoza kikao hicho. Pembeni ya Mwenyekiti wa pili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Christophe Bazivamo, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Forodha na Biashara, Bw. Keneth Bagamuhunda, na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Bw. Raphael Kanoth. |
Wakurugenzi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu. Wapili kushoto ni Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika kikao hicho ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen Mbundi, kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Benard Haule, wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria, Bi. Caroline Chipeta na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango, Bw. Gerald Mweli. |
Ujumbe wa Tanzania ukifatilia majadiliano katika kikao cha ngazi ya wataalamu. |
Mkutano ukiendelea. |
Simbu afuzu moja kwa moja kushiriki mashindano ya mwakani
Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab akiwa na wakimbiaji wa Tanzania walioshiriki mbio za marathon jijini Doha, Qatar. wakimbiaji hao walienda Ubalozini kuaga kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Wakimbiaji wa
Tanzania walimaliza rasmi mashindano ya mbio za Marathon na kwa bahati mbaya
wanariadha wawili hawakuweza kumaliza mbio hizo kutokana na maumivu ya goti na
misuli. Mwanariadha Alphonce Simbu ambaye alikuwa anatetea medali yake ya shaba
alishika nafasi ya 16 na alikuwa miongoni mwa wakimbiaji 20 bora ambao wamefuzu
moja kwa moja kushiriki mashindano ya mwakani.
Wakimbiaji wa
Ethiopia walishinda medali za dhahabu na fedha na Mkenya alishinda medali ya
shaba.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)