Monday, November 4, 2019
Friday, November 1, 2019
Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Afrika, Nordic
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic (Norway, Denmark, Finland, Sweden na Iceland) unaotarajiwa kufanyika tarehe 08 Novemba 2019 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Akiongea na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe alisema kuwa mkutano huu utafunguliwa rasmi na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ambapo hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huu mkubwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.
Kwa mujibu wa Dkt. Mnyepe, mkutano huu utajumuisha jumla ya mawaziri 34 wa Mambo ya Nje wa nchi za Afrika na Nordic pamoja na washiriki wengine ambao idadi yao inatarajiwa kufikia 250. Mawaziri watakaokuja kutoka nchi za Nordic ni wa nchi za Sweden, Norway, Denmark, Finland na Iceland. Kutoka nchi za Afrika watakuja Mawaziri wa Algeria, Angola, Benin, Botswana, Burkina Faso, Burundi, Comoros na Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC).
Nyingine ni pamoja na Misri, Ethiopia, Ghana, Kenya, Lesotho, Mali, Malawi, Morocco, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Niger, Rwanda, Senegal, Somalia, Afrika Kusini, Tunisia, Uganda, Zambia, Zimbabwe na sisi wenyeji Tanzania. Aidha, mkutano huo utajumuisha Mawaziri, Mabalozi wa nchi shiriki za Afrika katika nchi za Nordic, Mabalozi wa nchi za Nordic hapa nchini pamoja na watendaji wa Serikali. Kauli mbiu ya mkutano huu ni: "Ushirikiano kwa Maendeleo Endelevu"
"Mkutano huu unafanyika hapa Tanzania kutokana na ushirikiano kati ya Tanzania na nchi za Nordic ni wa kihistoria na wa kipekee. Ushirikiano huu ulianza hata kabla ya uhuru wa Tanganyika ambapo Wamisionari kutoka nchi hizo walikuja kufanya kazi hapa nchini kwenye sekta za afya na elimu. Katika sekta ya elimu, nchi hizo zilianzisha Kituo cha Kilimo cha Uyole na Kituo cha Elimu cha Kibaha kupitia Mradi wa Nordic-Tanganyika Project.
Ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulichangiwa kwa kiwango kikubwa na falsafa zilizokuwa zinafanana kuhusu maendeleo ya watu, ukombozi wa Afrika, urafiki miongoni mwa viongozi wetu na nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika Bara la Afrika," alisema Dkt. Mnyepe
Ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulichangiwa kwa kiwango kikubwa na falsafa zilizokuwa zinafanana kuhusu maendeleo ya watu, ukombozi wa Afrika, urafiki miongoni mwa viongozi wetu na nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika Bara la Afrika," alisema Dkt. Mnyepe
Katibu Mkuu aliongeza kuwa, "katika nchi za Afrika, Tanzania inapokea misaada mingi kutoka nchi za Nordic kuliko nchi nyingine yoyote. Kwa mfano kwa miaka mitano ya kuanzia mwaka 2013 hadi 2018, Tanzania imepokea takribani Shilingi za Kitanzania bilioni 900 kutoka nchi za Nordic. Nchi hizo zimekuwa zikisaidia sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo: elimu; afya; miundombinu; nishati; TEHAMA; utafiti; ukusanyaji wa kodi; bajeti; misitu; usawa wa jinsia; utunzaji wa mazingira; na ukuzaji wa sekta ya biashara,".
"Kufuatia ushirikiano huu wa kihistoria kati ya Tanzania na nchi za Nordic, nchi hizo ziliiomba Serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu kutokana na mahusiano na mazuri yaliyopo na hatua za kasi za kimaendeleo zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Kutokana na urafiki na historia hiyo hiyo Serikali ya Tanzania ilikubali kuwa mwenyeji wa mkutano wa mkutano huo na utafunguliwa na Mheshimiwa Rais. Kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni, Ushirikiano kwa Maendeleo Endelevu," aliongeza Katibu Mkuu
Aidha, mkutano huu, utajadili fursa za uwekezaji, biashara, amani na usalama na masuala mengine mtambuka, kama vile athari za mabadiliko ya tabianchi. Katika mkutano huu, tutazungumzia pia mahusiano baina yetu na nchi moja moja hususan ubia wa kimaendeleo. Kutokana na mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano, wenzetu wa Afrika na Nordic watapenda pia kusikia uzoefu na mafanikio ya Tanzania kwenye sekta za afya, elimu, nishati, miundombinu, kilimo, utalii, ukusanyaji wa kodi, mafanikio ya vita dhidi ya rushwa, ujangili, madawa ya kulevya na maeneo mengine.
Kwa upande wake Balozi wa Norway nchini Tanzania, Balozi Elisabeth Jacobsen alisema kuwa mkutano huu utatoa pia fursa ya mazungumzo ya uwili (bilateral meetings) kati ya nchi za Nordic na nchi za Afrika.
"Ni imani yangu kuwa kupitia mkutano huu tutaweza kujadilili mambo mbalimbali ikiwemo hatua za kimaendeleo zilizofikiwa katika sekta mbalimbali hususan afya, huduma za kijamii, elimu na mazingira kibiashara na uwekezaji kwani Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Nordic," alisema Balozi Elisabeth.
Nae Balozi wa Sweden nchini, Balozi Anders Sjoberg alisema kuwa mkutano wa kwanza ulifanyika nchini Sweden mwaka 2001 ambapo baada ya hapo mikutano kama hii ilikuwa inafanyika kwa kupokezana kutoka Bara la Afrika na nchi za Nordic.
"Kwanza kabisa naipongeza Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa mkutano huu wa Mawaziri wa Mambo ya Nje, ni fursa kutumia mkutano huu kujadili masuala ya kibiashara, uwekezaji, amani na usalama kwa maslahi ya nchi za Afrika na Nordic," alisema Balozi Sjoberg.
Wednesday, October 30, 2019
NAIBU WAZIRI AONGOZA UJUMBE WA WIZARA KWENYE KIKAO CHA KAMATI YA BUNGE
Kikao cha Wizara na Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kikiendelea. |
Sehemu ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao. |
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia taarifa ya Wizara iliyokuwa ikiwasilishwa wakati wa kikao. |
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Musa Azzan Zungu (MB), akichangia jambo wakati wa kikao. |
Sehemu nyingine ya Waheshimiwa Wabunge (Wajumbe wa Kamati) wakifuatilia kikao. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI MOJA KWA AJILI YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA MSALATO WA JIJINI DODOMA PAMOJA NA BARABARA ZA MZUNGUKO JIJINI HUMO.
Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imepongeza uamuzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli wa kuhamia Dodoma na kuahidi kuidhinisha kiasi cha dola za kimarekani milioni 455 sawa na zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Msalato sambamba na ujenzi wa barabara za mzunguko Jijini humo.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina ameyasema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abijdan Nchini Ivory Coast wakati wa Mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa benki hiyo itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Rais Dkt John Pombe Magufuli katika kipindi chake cha Uenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) lakini pia kwa Tanzania.
Amesema Benki hiyo tayari imeshaidhinisha kiasi cha dola za marekani milioni 180 kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma na kwamba kiasi kingine cha dola za marekani milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato kinatarajiwa kuidhinishwa na mapema mwezi Novemba 2019.
Dkt. Adesina ameongeza kuwa Benki ya Maendeleo ya Afrika ina imani na mageuzi ya kiuchumi yanayotekelezwa chini ya Uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ikiwa ni pamoja na utoaji wa huduma za kijamii ikiwemo elimu bila malipo,afya na maji pamoja na mapambano dhidi ya rushwa na kuleta uwajibikaji katika taaisisi za uma na kwamba iko tayari kuunga jitihada hizo za serikali kwa kuwekeza katika sekta ya miundombinu..
Aidha Dkt. Adesina ameelezea nia yake ya kutaka kushudia bara la Afrika likipiga hatua kubwa za kimaendeleo sasa na kwa haraka na sio kusubiri baadae na kwamba katika kipindi chake cha uongozi katika Benki ya Maendeleo ya Afrika atapambana kuhakikisha azma hiyo inatekelezeka.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ushirikiano inayoutoa kwa Tanzania hususani katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na rais Dkt. John Pombe Magufuli ambayo kimsingi yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi na hatimae Bara zima la Afrika.
Prof. Kabudi ameongeza kuwa tayari Benki ya Maendeleo ya Afrika iko tayari kufadhili ujenzi wa reli ya kisasa yaani standard gauge railway ya kipande cha kutoka Isaka hadi Kigali nchini Rwanda na kuelekea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mara baada ya kukamilika mchakato wa utoaji wa fedha hizo ambapo mazungumzo ya awali kuhusu ufadhili huo yameanza.
Pia Prof. Kabudi amemtaka Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika Dkt. Akinwumi Adesina kuimarisha ofisi za kanda za benki hiyo ili ziweze kutoa huduma zote za kibenki ili kusogeza huduma karibu na wanufaika wa benki hiyo sambamba na kuunga mkono miradi yote ya kimkakati inayounganisha nchi na nchi katika bara la Afrika ili kuboresha nakurahisisha huduma ya usafiri katika Bara la Afrika na hivyo kuwezesha biashara miongoni mwa nchi za Kiafrika na kujiletea maendeleo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi yuko Abijdan Nchini Ivory Coast kushiriki mkutano wa siku mbili wa dharura wa Mawaziri wa fedha uliondaliwa na Benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB).
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Abidjan - Ivory Coast.
30 OCTOBER 2019
BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AfDB) KUIPATIA TANZANIA ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI MOJA KWA AJILI YA UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA MSALATO NA BARABARA MZUNGUKO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina,mara baada mazungumzo yaliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abidjan Nchini Ivory Coast.Wengine katika picha ni viongozi wa AfDB na Afisa kutoka Wizara ya Fedha na Mipango wa Tanzania. |
Monday, October 28, 2019
Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC Wafanyika JIANGSU
Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC kutoka Jimbo la Jiangsu umefunguliwa leo jijini Nanjing na Naibu Gavana wa Jimbo hilo Ndugu Ma Qiulin. Mkutano huo umehudhuriwa na Mabalozi 11 wa nchi za SADC na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa SADC ambaye pia ni Mkurugenzi wa Miundombinu wa Sekretariat ya SADC Bi Mapolao Mokolena.
Katika hafla ya ufunguzi wa mkutano huo Balozi wa Tanzania Mhe. Mbelwa Kairuki alitoa hotuba kwa niaba ya Jumuiya ya Mabalozi wa Nchi za SADC nchini China ambapo pamoja na mambo mengine aliyakaribisha makampuni ya SADC kuchangamkia fursa za uwekezaji katika nchi za SADC kutokana na fursa za soko kubwa la SADC lenye idadi ya watu wanaokadiliwa kuwa milioni 345 na uchumi wa GDP 600 Billioni.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miundombinu wa SADC Bi Makolane alipokuwa akitoa mada alielezea mazingira mazuri yaliyopo ya biashara na uwekezaji katika nchi za SADC. Aidha, Mabalozi wa nchi za SADC walielezea fursa zilizopo katika nchi za SADC katika sekta za miundombinu, kilimo, viwanda; madini; utalii nk.
Jiangsu ni jimbo la pili kwa ukubwa wa uchumi nchini China likiwa na GDP ya USD 1.2 Trillion na idadi ya watu milioni 80. Jimbo hilo linaongoza nchini China katika sekta ya viwanda. Makampuni kutoka Jimbo la Jiangsu yamefanya uwekezaji nchini Tanzania katika sekta ya viwanda.
Balozi wa Tanzania nchini China Mhe. Mbelwa Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Afrika na wenyeji China mara baada kuhitimisha mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC uliofanyika jimbo la Jiangsu nchini China |
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Mkutano wa kuvutia uwekezaji katika nchi za SADC ulifanyika Jiangsu, China |
Mhe. Balozi Mbelwa Kairuki (mstari wa mbele katikati) akifuatilia Mkutano wa kuvutia uwekezaji uliokuwa ukiendelea |
Wajumbe kutoka chi za SADC na Wenyeji tao China wakifutilia Mkutano uliokuwa ukiendelea |
Friday, October 25, 2019
TANZANIA YATAKA ZIMBABWE KUONDOLEWA VIKWAZO VYA KIUCHUMI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akihutubia katika kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu kutoka Zimbabwe. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza katika kongamano la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe |
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (Mb) akitoa hotuba ya majumuisho na kufunga kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. John Jingu, akihutubia hadhara wakati alipowasilisha mada iliyolenga hali ya utawala na diplomasia ya uchumi Afrika katika kongamano maalumu la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe. |
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye akimkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano maalumu lililojadili vikwazo vya kiuchumi na hatma ya Afrika: Uzoefu kutoka zimbabwe.
|
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Mstaafu Joseph Warioba (wa pili kutoka kulia) pamoja na viongozi waandamizi wa Serikali, vyama vya siasa wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano maalumu |
Baadhi ya mabalozi wateule pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) katika kongamano la kujadili vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Zimbabwe. |
Vingozi, Mabalozi na wananchi wakifuatilia mdahalo wa kujadili jinsi ya kuiwezesha Zimbabwe kuondolewa vikwazo vya kiuchumi.
|
Wageni wa Meza kuu wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masahariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango (Mb) na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. William Anangisye pamoja na watoa mada wakiwa katika picha ya pamoja na mabalozi wateule katika picha ya pamoja mara baada ya kuhitimishwa kwa kongamano
|
Mabalozi wa SADC, Qatar watoa wito kuiondolea vikwazo Zimbabwe.
Waheshimiwa Mabalozi wakiwa wanaendelea kutekeleza jukumu lao.
|
Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Mhe. Fatma Rajab akiongea na Waheshimiwa Mabalozi wa Nchi za Eswatini na Afrika Kusini ambao wanaunda kundi la Mabalozi wa nchi za SADC nchini Qatar. Waheshimiwa Mabalozi walikuwa wanakamilisha mpango mkakati wa kutumia siku ya tarehe 25 Oktoba kama ilivyoamuliwa na Viongozi wa Nchi za SADC kupaza sauti kwa njia mbalimbali kutoa wito kwa nchi za Magharibi kuiondolea vikwazo vya uchumi ilivyowekewa Zimbabwe. Mabalozi hao wamepanga kupeleka Waraka wa Kidiplomasia Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar, Balozi za EU na Ubalozi wa Marekani pamoja na kutoa makala kwenye vyombo vya habari kuelezea athari za vikwazo katika uchumi wa Zimbabwe. |
WAZIRI KABUDI ASHIRIKI MAADHIMISHO YA 74 YA SIKU UMOJA WA MATAIFA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini alipowasili katika uwanja wa Nyerere Square jijini Dodoma kushiriki maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa amesimama sehemu maalumu wakati wimbo wa Taifa ulipokuwa unapigwa kwenye sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa mbele ya parede maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akikagua parede maalumu liliondaliwa kwa ajili ya sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja Mataifa |
Sehemu ya hadhara iliyojitokeza katika uwanja wa Nyerere Square kushuhudia sherehe za maadhimisho 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (katikati) akifuatalia matukio yaliyokuwa yakiendelea wakati wa maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, akipokea zawadi kutoka Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini iliyowasilishwa na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi, kwenye sherehe za maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Mataifa iliyofanyika jijini Dodoma |
Meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi Wafanyakazi wa Ofisi za Umoja wa Mataifa nchini |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia hadhira iliojitokeza kwenye maadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Taifa iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Nyerere Square |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akihutubia hadhira iliojitokeza (hawapo pichani) kwenye amaadhimisho ya 74 ya Siku ya Umoja wa Taifa iliyofanyika jijini Dodoma katika uwanja wa Nyerere Square |
WAKATI HUO HUO MHE. PROF. KABUDI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BW. MICHAEL DUNFORD KAIMU MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi, akiwa na Bw.Michael Dunford Kaimu Katibu Makazi wa Umoja wa Mataifa nchini, walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi za Wizara jijini Dodoma. Wengine ni Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Ushikiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Bi.Glory Ngaiza Afisa Mambo ya Nje. |
Waziri Mhe. Prof. Kabudi akilelezea jambo wakati wa mazungumzo na Bw. Michael Dunford Kaimu Katibu Makazi wa Umoja wa Mataifa nchini. Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendelea kudumisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Umoja wa Mataifa |
VILEVILE WAZIRI MHE. PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akisisitiza jambo alipokutana wakati wa mazunguzo na Mkuu wa Shirika la Wahamiaji nchini Dr. Qasim Sufi walipokutana kwa mazungumzo katika ofisi za Wizara jijini Dodoma. Wawili hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuendelea kudumisha ushiririkiano kwa lengo la kuongeza ufanisi katika kutoa huduma. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akimsikiliza Mkuu wa Shirika la Wahamiaji nchini Dr. Qasim Sufi walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma |
Wednesday, October 23, 2019
MAADHIMISHO YA SIKU YA UMOJA WA MATAIFA KUFANYIKA KESHO, DODOMA
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara, jijini Dodoma. Katika mkutano huo Dkt. Mnyepe amewajulisha waandishi wa habari kuhusu kufanyika kwa maadhimisho ya siku ya Umoja wa Mataifa tarehe 24 Oktoba, 2019 jijini Dodoma kwenye uwanja wa Nyerere square. Dkt. Mnyepe amebainisha kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za maadhimisho hayo, yatakayofanyika kuanzia saa 2.30 asubuhi hadi 5.00 asubuhi. Maadhimisho ya mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo "Wanawake na Wasichana kuwa Kipaumbele katika kufikia Malengo ya Dunia. Kauli mbiu hii inalenga kusisitiza uwajibikaji na ushirikishwaji wa Wanawake katika kufikia malengo ya dunia. Aidha, Katibu Mkuu Dkt. Mnyepe amebainisha kuwa Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kuheshimu na kusimamia misingi ya kulinda na kutetea maslahi ya Wanawake na Wasichana ikiwemo kuwashirikisha katika mipango ya maendeleo ya kijamii na uchumi. Maadhimisho ya Siku ya Umoja wa Mataifa hufanyika kila mwaka tarehe 24 Oktoba. Maadhimisho ya mwaka huu ambayo yatapambwa na shamrashamra kutoka vikundi mbalimbali vya sanaa, yanatarajiwa kuhudhuriwa na Viongozi na Watendaji Wakuu wa Serikali, Wawakilishi kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa nchini, vijana, asasi za kiraia na wadau wengine mbalimbali. |
Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, akizungumza na waandishi wa habari kwenye mkutano uliofanyika ofisi za Wizara ya Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma. |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (katikati) Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Bw. Michael Dunford Kaimu Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakisikiliza maswali kutoka kwa Wanahabari (hawapo pichani). |
Picha ya pamoja baada ya mkutano na waandishi wa habari |
Subscribe to:
Posts (Atom)