Thursday, July 8, 2021

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA WHO

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Ketsela Mengestu ambapo pamoja na mambo mengine wamezungumzia juu ya masuala ya mapambano dcidi ya ugonjwa wa Corona
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Ketsela Mengestu akimsikiliza mwenyeji wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) hayupo pichani walipokutana kwa jailli ya mazungumzo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Ketsela Mengestu mara baada ya mazungumzo

 

Wednesday, July 7, 2021

BALOZI LIBERATA MULAMULA ASHIRIKI MKUTANO WA 23 WA KAMATI YA MAWAZIRI WA ASASI YA SIASA,ULINZI NA USALAMA YA SADC

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. George Simbachawene katika mkutano wa 23 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama (MCO) unaofanyika kwa nia ya mtandao. Nyuma ya Mawaziri hao aliyevaa barokoa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Edward Sokoine

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. George Simbachawene (Mb) wakifuatilia kwa karibu mjadala unaoendelea katika mkutano wa 23 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama (MCO) unaofanyika kwa nia ya mtandao. Nyuma ya Mawaziri hao aliyevaa barokoa ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Edward Sokoine


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. George Simbachawene (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Edward Sokoine (aliyevaa barokoa nyeupe) wakiwa pamoja na ujumbe wa Tanzania katika kutano wa 23 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama (MCO) unaofanyika kwa nia ya mtandao



 

Tuesday, July 6, 2021

BALOZI MULAMULA AAPA KUWA MJUMBE WA BARAZA LA MAAMUZI LA EALA

Na Mwandishi wetu, Dar

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge hilo.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge hilo Mhe. Martin Ngoga leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam Balozi Mulamula amesisitiza umuhimu wa bunge hilo kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano kutokana na umuhimu  na matarajio ya Wananchi kwa Bunge hilo.

Aidha Balozi Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na Bunge hilo kuendelea na vikao vyake kwa njia ya mseto ikiwa ni pamoja na kukutana ana kwa ana ama kwa njia ya mtandao licha ya changamoto ya uwepo wa ugonjwa wa UVIKO – 19 hali inayoonesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi.

“Wananchi wamekuwa na matarajio makubwa sana kupitia Bunge hili la Afrika Mashariki kiuweza kuona faida na mambo mazuri yanayofanyika kupitia jumuiya hii ya Afrika Mashariki,” Amesema Balozi Mulamula

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiapa kuwa Mjumbe wa Baraza la Maamuzi wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) leo tarehe 6 Juni 2021 katika mkutano uliofanyika kwa njia ya Mtandao jijini Dar es Salaam 



Monday, July 5, 2021

DKT. MPANGO: WIZARA NA BALOZI ENDELEENI KUAINISHA, KUTANGAZA FURSA

Na Mwandishi wetu, Dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Balozi za Tanzania kuainisha na kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini hususani biashara na uwekezaji.

Dkt. Mpango ametoa maelekezo hayo alipotembelea banda la Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam. Mara baada ya kuwasili katika banda la Wizara, Dkt. Mpango amepokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk.

“Naipongeza Wizara kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya ya kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia ……..lakini pia Wizara iendelee kuzishirikisha Balozi zetu katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini, na Balozi hizo ziainishe fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye nchi za uwakilishi kwa ajili ya Watanzania,” Amesema Dkt. Mpango

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Mpango ameielekeza Wizara ya Maambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kuboresha majukumu ya Wizara ikiwa ni pamoja na balozi za Tanzania na Taasisi zake.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiongea na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk pamoja na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango akiongea na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk pamoja na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam


Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam 

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na watumishi wa Wizara wakati alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam 


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Geoffrey Mwambe (Mb) akipokea nakala ya Jarida la Diplomasia linalochapishwa na  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam 

 

Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Ibrahim Mmbaga akifafanua jambo kwa mwananchi aliefika kwenye banda la Wizara katika Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es salaam








BALOZI MULAMULA ATEMBELEA MAONESHO YA SABSABA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) alipowasili katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere kutembelea maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kujionea shughuli zinazoendelea katika maonesho hayo


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika banda la Chuo cha Diplomasia alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda hilo kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam

 

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bw. Emmanuel Buhohela akimueleza jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha moja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam











Saturday, July 3, 2021

MAREKANI YAADHIMISHA MIAKA 245 YA UHURU

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisalimiana na Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright mara baada ya kuwasili katika makazi ya Balozi huyo Dar Es Salaam kushiriki katika hafla ya miaka 245 ya Uhuru wa marekani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa pamoja na Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright wakiimba wimbo wa Taifa la Marekani katika maadhimisho ya miaka 245 ya Uhuru wa Taifa la Marekani. Hafla hiyo imefanyika katika makazi ya Balozi huyo Jijini Dar Es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa pamoja na Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright wakiimba wimbo wa Taifa la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 245 ya Uhuru wa Taifa la Marekani. Hafla hiyo imefanyika katika makazi ya Balozi huyo Jijini Dar Es Salaam
Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright akisoma risala katika maadhimisho ya miaka 245 ya Uhuru wa Taifa la Marekani yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam katika makazi ya Balozi huyo. Kushoto aliyekaa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) ambale ni mgeni rasmi katika maadhimisho hayo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiinua glasi dhidi ya Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright ikiwa ni ishara ya kutakiana heri katika maadhimisho ya miaka 245 ya Uhuru wa Taifa la Marekani yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam katika makazi ya Balozi huyo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb)akisoma risala katika maadhimisho ya miaka 245 ya Uhuru wa Taifa la Marekani yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam katika makazi ya Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright

Hadhira  ya Wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 245 ya Uhuru wa Taifa la Marekani yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam katika makazi ya Balozi wa Marekani hapa Nchini Dkt. Donald Wright wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb)

Friday, July 2, 2021

BALOZI SOKOINE: WAFANYABIASHARA TUMIENI BALOZI ZA TANZANIA

Na Mwandishi wetu, Dar

Wafanyabiashara nchini wanaofanya biashara nje ya nchi wameshauriwa kuwasiliana na balozi za Tanzania ili kupata taarifa sahihi kuhusu fursa za biashara na uwekezaji katika nchi wanazopenda kufanya nazo biashara.

Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.

Balozi Sokoine amesema kuwa endapo wafanyabiashara watatumia Balozi za Tanzania Nje ya Nchi itakuwa rahisi kwao kuwapatia taarifa sahihi zaidi kuliko kutumia vyanzo vingine.

“Endapo wafanyabiashara wetu wanaofanya biashara nje watatumia fursa ya kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje kupitia Balozi zake Nje ya Nchi watapatiwa taarifa sahihi ambazo zitawasaidia kuokoa muda na kupata bidhaa kwa wakati,” Amesema Balozi Sokoine.

Pamoja na mambo mengine, Balozi Sokoine amewasihi watanzana kwa ujumla kupita katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje ili kuweza kupata uelewa wa taarifa/ufafanuzi wa masuala mbalimbali ya kidiplomasia.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Joseph Sokoine akisaini kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Joseph Sokoine akimsikiliza Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Bw. Emmanuel Buhohela katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade  Balozi Mteule, Mhe. Edwin Rutageruka.


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Joseph Sokoine akiongea na waandishi wa habari katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Joseph Sokoine, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade  Balozi Mteule, Mhe. Edwin Rutageruka na Mwakilishi kutoka chuo cha Diplomasia, Mhe. Balozi Innocent Shio wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Joseph Sokoine akipata ufafanuzi kutoka banda la magazeti ya Serikali (TSN) wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam 


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Joseph Sokoine akiwa katika banda la Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC) wakati alipotembelea Maonesho ya 45 ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) yanayoendelea Jijini Dar es Salaam 















WIZARA YA MAMBO NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI YAVUTIWA NA KASI YA UJENZI WA SGR


Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inajivunia na kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa reli mpya ya kisasa (Standard Gauge Railway - SGR) unaoendelea katika hatua mbalimbali nchini. 

Haya yamesemwa na Bw. Eliabi Chodota Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii,alipotembelea mradi huo ambao kwa sasa ndio mradi pekee mkubwa wa reli ya kisasa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Ameongeza kuwa mradi huu sio tu ni muhimu kwa Tanzania bali utazinufaisha pia nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki na nchi zingine jirani. Bwana Chodota pia ameeleza kuridhishwa kwake na ushiriki wa Watanzania katika katika ujenzi wa mradi huo, ambapo kati ya Wafanyakazi zaidi ya 6000, zaidi ya asilimia 80 ni Watanzania. 

Bwana Chodota ametembelea maradi huo unaotekelezwa katika awamu tano (5) kama ifuatavyo: sehemu ya awamu ya kwanza Kilomita 202 (Dar es Salaam-Morogoro), awamu ya pili Kilomita 348 (Morogoro – Makutopora) awamu ya tatu Kilomita 294 (Makutopora-Tabora) awamu ya nne (Tabora-Isaka), na sehemu ya awamu ya tano Kilomita 341 (Isaka-Mwanza) kwa lengo la kujionea hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo.

Mradi huu wa SGR, unaoendelea kujengwa kwa kasi, baada ya kukamilika kwake unatarajiwa kuiunganisha Tanzania na nchi jirani za Rwanda na Uganda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Reli hii mpya inatarajiwa kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya usafiri na usafirishaji nchini kwa kupunguza msongamano barabarani, kupunguza muda wa kusafiri na kupunguza uharibifu wa miundombinu ya barabara. Sambamba na hayo, pia inatarajiwa kupunguza gharama za usafirishaji kwa 40%. Kila treni ya mizigo inatarajiwa kusafirisha hadi tani 10,000 kiasi ambacho kinaweza kusafirishwa na malori 500 kwa njia ya barabara.

Bwana Chodota ametoa rai kwa Watanzania hasa ambao wanazunguka eneo la mradi kuendelea kutoa ushirikiano kwa mamlaka na Mkandarasi ili kuendelea kuruhusu kasi ujenzi wa mradi iendelee na kuweka mazingira rafiki na salama kwa mradi huo wakati wote.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kushoto) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa katika kituo cha reli ya kisasa SGR cha mjini Morogoro muda mfupi baaada ya kuwasili katika kituo hicho. Wengine pichani ni Watumishi wa Wizara na Shirika la Reli Nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa kwanza kulia) akifuatilia maelezo ya Waandisi wa ujenzi wa mradi wa SGR.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (wa pili kushoto) akifuatilia maelezo ya Waandisi wa ujenzi wa mradi wa SGR katika Kituo Kikuu cha mradi huo jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) akiwa na baadhi ya watumishi wa Wizara na Shirika la Reli nchini kwenye kituo cha SGR cha Soga.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota (mwenye tai) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Wizara aliombatana nao katika ziara ya kutembelea mradi wa SGR.

Thursday, July 1, 2021

MHE WAZIRI MULAMULA AKUTANA KWA MAZUNGUMZO NA JAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu iliyopo Arusha, Mhe. Tujilane Chizumila alipomtembelea Ofisi kwake jijini Dodoma leo tarehe 1 Julai 2021 kwa ajili ya kumsalimia na kumpongeza kwa kuteuliwa kuwa Waziri. 


Mhe. Waziri akimsikiliza Mhe. Jaji Chizumila wakati wa mazungumzo kati yao

Mazungumzo yakiendelea

Mhe. Waziri akimweleza jambo Mhe. Jaji Chizumila mara baada ya kumaliza mazungumzo kati yao



 

BALOZI SOKOINE AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MKAZI WA (PEACE CORPS)

 Na Mwandishi wetu, Dar

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea maandalizi ya ujio wa wafanyakazi  wa kujitolea wa Shirika hilo kutoka Marekani.

Bibi. Stephanie Joseph de Goes amemueleza Balozi Sokoine kuwa wafanyakazi hao wanatarajiwa kuwasili hapa nchi kwa ajili ya kufanya kazi katika maeneo mbalimbali yenye uhitaji.

Pamoja na Mambo mengine, Katibu MKuu Balozi Sokoine amemhakikishia Mkurugenzi Mkazi huyo ushirikiano na kwamba Wizara ya Mambo ya Nje na UShirikiano wa Afrika Mashariki iko tayari kuratibu utendaji wa shirika hilo hapa nchini kwa kushirikiana na Wizara nyingine za Kisekta zinazoguswa kiutendaji na Shirika hilo kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisalimiana na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes akimkabidhi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine Ripoti ya Mwaka ya Shirika hilo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam


Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Wafanyakazi wa Kujitolea la Kimarekani (Peace Corps) Bibi. Stephanie Joseph de Goes akiagana na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine mara baada ya kumalizika kwa maongezi yao