Monday, February 14, 2022
EMPLOYMENT OPPORTUNITIES
Friday, February 11, 2022
MAWAZIRI WA SEKTA YA NISHATI WA EAC WASISITIZA UMUHIMU WA KUPATIKANA KWA NISHATI YA UHAKIKA
Mawaziri wa Sekta ya Nishati wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana leo tarehe 11 Februari 2022 jijini Arusha, Tanzania kwa lengo la kuhudhuria Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya hiyo.
Mkutano
huu ulitanguliwa na mikutano ya awali ngazi ya Wataalamu/Maafisa waandamizi uliofanyika
tarehe 8 na 9 Februari 2022 na kufuatiwa na mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu
uliofanyika tarehe 10 Februari 2022.
Ujumbe
wa Tanzania kwenye mkutano huu umeongozwa na Waziri wa Nishati, Mhe. January
Makamba (Mb.) ambaye ameambatana na; Katibu Mkuu Wizara ya Nishati - Tanzania
Bara, Mhandisi Felschesmi Mramba; Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini -Zanzibar;
Dkt. Mngereza Miraji; Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli
Tanzania (TPDC), Dkt. James Mataragio; Kamishna wa Petroli na Gesi kutoka
Wizara ya Nishati; Bw. Michael Mjinja na Maafisa Waandamizi kutoka Wizara ya Nishati na Taasisi
zake kwa ujumla.
Akihutubia
wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Waziri Makamba aliwakaribisha nchini wajumbe wa
mkutano huo na kuwahakikishia kuwa mkutano utafanikiwa kuyafikia malengo
yake kufuatia uongozi imara wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe.
Peter Mathuki.
Vilevile
akaeleza ukanda wa Afrika Mashariki umejaaliwa rasilimali nishati za kutoka
hivyo, ni wakati sasa kwa kila nchi kuwa na mikakati imara ya kuhakikisha
nishati ya uhakika inapatikana ili kuihakikishia jamii upatikanaji wa huduma
zote zinazohitaji nishati.
“Tukiwa
tunapitia changamoto za ugonjwa wa COVID-19 tumeshuhudia namna gani nishati zilihitajika
katika kusaidia kuleta nafuu na kuokoa maisha ya wananchi wetu” alisema Mhe.
Makamba.
Naye
mwenyekiti wa mkutano huo na Waziri wa Nishati wa Jamhuri ya Kenya, Mhe. Dkt.
Monica Juma alitumia nafasi hiyo kuwashukuru Watalamu na Makatibu Wakuu kwa
kufanya maandalizi mazuri ya Mkutano huo na kusisitiza kuwa upatikanaji wa
umeme wa uhakika ni moja ya viashiria vya kukua kwa uchumi wa nchi yeyote.
Pia
akaeleza kukua kwa uchumi husaidia kupunguza utegemeze na hivyo jitihada za
makusudi zinahitajika kuziwesha Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya
uzalishaji wa kutosha viwandani na katika sekta ya kilimo.
Mkutano huu wa 15 wa Baraza la Mawaziri wa
Kisekta la Nishati pamoja na mambo mengine utapitia na kutoa maamuzi juu ya;
Tarifa ya hali ya utekelezaji wa maagizo ya mikutano iliyopita; Hatua iliyofikiwa
hadi sasa katika sekta za Nishati Jadidifu, Nishati ya Umeme na Nishati ya
Mafuta; pamoja na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kitaifa na Kikanda ya
Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kadhalika mkutano huu utajadili kwa kina utekelezaji wa mradi wa kituo cha Nishati Jadidifu cha Afrika Mashariki; Mradi wa Kufua Umeme wa Nsongezi; Mradi wa kufua Umeme wa Murongo/Kigagati (14MW) na Taasisi ya Mamlaka ya udhibiti wa Nishati katika Nchi za Afrika Mashariki.
===================================================
Maafisa Waandamizi kutoka Wizara za Nishati Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar. |
Maafisa Waandamizi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) |
Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Mgeta Sabe pamoja na maafisa waandamizi kutoka Taasisi za Nishati wakifuatilia mkutano |
Ujumbe kutoka Kenya |
Ujumbe kutoka Uganda |
Balozi Kilima ateta na Wawekezaji kutoka Ujerumani
Wawekezaji hao ambao ni Dkt. Michael Voch na Bw. Claus Heim kutoka Ujerumani na Bw. Khalid Hamdoun M. Aljabri na Bw. Mohammed Al Riyami kutoka Taasisi ya IGD ya Oman wanakusudia kuwekeza katika sekta ya uzalishaji wa nguvu ya umeme wa kutumia Jua kwa teknolojia mpya inayoitwa Solar Container. Teknolojia hiyo inatumua maji kuzalisha hydrojen ambayo ndiyo inayotoa umeme na oxygen kama mabaki ya uzalishaji (byproducts)
Teknolojia hiyo tayari inatumika katika nchi za Ulaya na hivi karibuni itaanzishwa nchini Oman inaweza kutosheleza nyumba 200 Kwa kontena moja na pia inaweza kuunganishwa na Gridi ya Taifa
Wawekezaji hao pia wanakusudia kuanzisha miradi ya kilimo inayotumia Teknolojia ya Hydroponic system ambacho kinatunia eneo dogo lakini tija kubwa.
Wawekezaji imeiomba Serikali ya Tanzania kuwapatia eneo la uwekezaji pamoja na kuunganishwa na makampuni yatakayoweza kununua bidhaa watakazozalisha kama wanavyofanya nchini UAE, waneingia mkataba na Shirika la Ndege la Emirate kununua bidhaa za vyakula watakavyozalisha.
Kwa upande wake, Mhe. Balozi aliwaeleza wawekezaji hao kwamba Tanzania inakarubisha uwekezaji katika sekta ya uzalishaji wa nguvu za umeme wa kutumia Jua kwani ni nishati mbadala na rahisi kutumika. Kwa upande wa mradi wa kilimo cha hydroponic, Mhe. Balozi alieleza kwamba kilimo hicho kinaweza kuwa mkombozi wa kilimo cha kutegemea mvua ambacho huwa ni cha msimu. Hivyo mradi huo unaweza kuongeza uzalishaji na kupata ziada ya kuuza nje ya nchi.
Balozi wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akizungumza na wawekezaji kutoka Ujerumani. Kulia Kwake ni Dkt. Michael Voch na Bw. Claus Heim |
Thursday, February 10, 2022
MAKATIBU WAKUU WA SEKTA YA NISHATI WA EAC WAMEKUTANA JIJINI ARUSHA
Mkutano wa Makatibu Wakuu ulitanguliwa na mkutano wa Maafisa Waandamizi
uliofanyika tarehe 8 na 9 Februari 2922. Hii ni mikutano ya awali
kwaajili ya maandalizi ya Mkutano wa 15 Wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la nishati la Jumuiya ya Afrika Mashariki utakaofanyika kesho tarehe 11 Februari 2022.
Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Makatibu Wakuu umeongozwa na
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati (Tanzania Bara), Mhandisi Felchesmi Mramba ambaye ameambatana na
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini wa Zanzibar, Dkt. Mngereza Miraji.
Pamoja na mambo mengine Mkutano wa Makatibu Wakuu umepitia
na kuandaa: Taarifa ya hali ya utekelezaji wa maagizo ya mikutano
iliyopita; Hatua iliyofikiwa hadi sasa katika sekta za Nishati Umeme, Nishati
Mafuta, na Nishati Jadidifu; pamoja na Utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Kitaifa
na Kikanda ya Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano mwenyekiti wa mkutano huo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati wa Jamhuri ya
Kenya, Maj. Gen. Dkt. Gordon Kihalangwa, CBS alieleza kuwa uhaba wa nishati
ndani ya nchi zetu na jumuiya kwa ujumla huleta changamoto kwa wananchi wote na
kushusha shughuli za uchumi na pato la taifa kwa ujumla. Hivyo, akasisitiza
umuhimu wa kuunganisha nguvu katika kutekeleza miradi ya nishati ya kitaifa na
kikanda.
Vilevile akaeleza umuhimu wa sekta ya afya
kupatiwa nishati ya kutosha na ya uhakika ili kuondoa changamoto za mara kwa
mara zinazochangia kukosekana kwa huduma hizo.
“Huduma za mama na mtoto pamoja na
huduma nyingine za afya ni muhimu zikazingatia upatikanaji wa nishati ili
kupunguza matatizo yatokanayo na kukosekana kwa nishati ya uhakika kwa baadhi
ya vifaa vinavyohitaji nishati ya umeme na gesi” alisema Dkt. Gordon.
Mkutano huu umefanyika kwa njia ya mseto
ambapo nchi za Tanzania, Kenya na Uganda wameshiriki mkutano wa ana kwa ana
isipokuwa Burundi, Rwanda na Sudan Kusini wameshiriki kwa njia ya mtandao.
Kulia ni Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia majadiliano katika mkutano huo. |
Ujumbe wa Tanzania |
Mkutano ukiendelea |
Ujumbe kutoka Uganda |
Ujumbe kutoka Kenya |
WATANZANIA WAASWA KUILINDA NCHI
Semina ya siku moja kwa wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dodoma masuala mbalimbali ya Mtangamo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiendelea |
Sehemu ya wadau wakifuatilia semina ya siku moja kwa wanafunzi wa shule za sekondari za jijini Dodoma iliyofanyika kwenye ukumbi wa informatics katika Chuo Kikuu cha Dodoma |
Picha ya patoja |
Semina ikiendelea |
Semina ikiendelea |
Wednesday, February 9, 2022
Tuesday, February 8, 2022
RAIS WA BENKI YA MAENDELEO YA AFRIKA (AFDB) DKT. ADESINA AWASILI DODOMA
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
akisalimiana na Rais wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi
Adesina alipowasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma akiwa
katika ziara ya kikazi ya siku tatu nchini.
Rais
wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinwumi Adesina awasili jijini Dodoma akiwa katika ziara ya
kikazi ya siku tatu nchini. Katika uwanja wa ndege wa Dodoma Dkt. Adesina
amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba.
Dkt.
Adesina yuko nchini kwa ziara ya siku tatu ambapo
tarehe 09 February 2022 atashiriki katika uzinduzi wa ujenzi wa barabara za
mzunguko zinazojengwa katika jiji la Dodoma utakaofanywa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Ujenzi
wa barabara hizo za mzunguko zenye urefu wa kilomita 112.3 unagharamiwa kwa
pamoja kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na benki hiyo. Ujenzi wa barabara hizo utalifanya jiji la Dodoma kuwa na barabara za aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.
MKUTANO WA 15 WA BARAZA LA MAWAZIRI LA KISEKTA LA NISHATI LA EAC WAFUNGULIWA JIJINI ARUSHA KATIKA NGAZI YA WATAALAMU
Mkutano wa 15 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la Jumuiya ya Afrika
Mashariki umefunguliwa leo tarehe 8 Februari 2022 jijini Arusha, Tanzania
katika ngazi ya Wataalamu.
Mkutano huu utafanyika katika ngazi tatu ambapo umeanza na;
Mkutano Ngazi ya Wataalamu unaofanyika tarehe 8 hadi 9 Februari 2022,
utafuatiwa na Mkutano Ngazi wa Makatibu Wakuu utakaofanyika tarehe 10 Februari
2022 na utamalizika kwa Mkutano Ngazi ya Mawaziri utaofanyika tarehe 11
Februari 2022.
Lengo la Mkutano huu ni kupitia na kuandaa
taarifa ya hali ya utekelezaji wa Maamuzi/Maagizo ya mikutano iliyopita; Hatua
iliyofikiwa hadi sasa katika sekta za Nishati Umeme, Nishati Mafuta, na Nishati
Jadidifu; pamoja na Utekelezaji wa Miradi/Programu mbalimbali za Kitaifa na
Kikanda ya Sekta za Nishati inayotekelezwa ndani ya
Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.
Ujumbe wa Tanzania katika
Mkutano Ngazi ya Wataalamu unaongozwa na Kamishna Msaidizi Maendeleo ya
Umeme kutoka Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila ambaye ameambatana
na Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota,
Mkurugenzi Idara ya Nishati na Madini kutoka Wizara ya Nishati na Madini
Zanzibar, Mhandisi Said H. Mdungi pamoja na maafisa wengine Waandamizi kutoka
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye dhamana katika sekta ya nishati.
Mkutano Ngazi ya Wataalamu
na Ngazi ya Makatibu Wakuu ni sehemu ya mikutano ya awali kwaajili ya
maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Nishati la
Jumuiya ya Afrika Mashariki utaofanyika tarehe 11 Februari 2022.
Kushoto ni Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika Mkutano Ngazi ya Wataalamu na Kamishna Msaidizi wa Maendeleo ya Umeme katika Wizara ya Nishati, Mhandisi Styden Rwebangila na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Eliabi Chodota akifafanua jambo wakati wa majadiliano ya mkutano huo. |
Mwenyekiti wa Mkutano Ngazi ya Wataalamu na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu kutoka Jamhuri ya Kenya, Mhandisi Benson Mwakina (Kushoto) akiongoza majadiliano, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Bw. Christophe Bazivamo. |
Kushoto ni Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi Mgeta Sabe na wajumbe wengine wa Tanzania wakifatilia majadiliano. |
Ujumbe wa Tanzania. |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania. |
WAZIRI MULAMULA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA 46 WA DHARURA WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC
Mkutano ukiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu Balozi Joseph Sokoine (katika) na Mkurugenzi wa Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen Mbundi wa Wizara hiyo wakifuatilia Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea |
Ujumbe wa Tanzania ukifuatilia Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendele |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea kwenye Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akichangia hoja kwenye Mkutano wa 46 wa Dharura wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika kwa njia ya mtandao. |
Monday, February 7, 2022
WAZIRI MULAMULA: TUTAENDELEA KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Edwin Rutageruka (wa kwanza kusho), Mkurugenzi wa Diplomasia Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Makamu wa Rais wa Kampuni ya dmg event ya nchini Uingereza Bw. Damian Howard (wa pili kushoto) na Bw. Abdulsamad Abdulrahim (kulia) Mkurugenzi wa Kampuni ya Ocean Business Partners Tanzania Ltd walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma. |
Mazungumzo yakiendelea |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma |