Monday, February 7, 2022

WAZIRI MULAMULA: TUTAENDELEA KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA SEKTA YA NISHATI NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amesema Wizara kwa kushirikiana na Wizara zingine, Mashirika na Taasisi za Serikali na Sekta binafsi itaendelea kuweka jitihada katika kutangaza fursa za uwekezaji zinazotokana na sekta ya nishati. 

Waziri Mulamula ameeleza haya wakati wa mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ocean Business Partners Tanzania Ltd Bw. Abdulsamad Abdulrahim na Makamu wa Rais, wa Kampuni ya dmg event ya nchini Uingereza Bw. Damian Howard yaliyofanyika Ofisini kwake jijini Dodoma. “Licha ya hazina kubwa tuliyonayo katika sekta ya nishati, serikali pamoja sekta binafsi bado tunakazi kubwa ya kuendelea kutangaza na kutafuta wawekezaji ili kukuza uwekezaji na mapato katika sekta hii. Waziri Mulamula. 

Bwana Abdulsamad na Bw. Howard wamepongeza juhudi zinazoendelea kufanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi madhubuti wa Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini. Waliongeza kusema Makampuni yao yataendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika kutangaza fursa za uwekezaji zinazotokana na sekta ya nishati nje ya mipaka ya Tanzania. 


Katika tukio jingine Waziri Mulamula amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima alipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma. 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Edwin Rutageruka (wa kwanza kusho), Mkurugenzi wa Diplomasia Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Makamu wa Rais wa Kampuni ya dmg event ya nchini Uingereza Bw. Damian Howard (wa pili kushoto) na Bw. Abdulsamad Abdulrahim (kulia) Mkurugenzi wa Kampuni ya Ocean Business Partners Tanzania Ltd walipokutana kwa mazungumzo jijini Dodoma.
Mazungumzo yakiendelea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Adam Malima wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika ofisi za Wizara jijini Dodoma

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.