Sunday, February 20, 2022

BALOZI MBAROUK AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUMUAGA BALOZI EDWIN RUTAGERUKA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiongoza waombolezaji katika kuaga mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasi ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Marehemu Balozi Edwin Rutageruka katika kijiji cha Musibuka, Wilayani Misenyi Mkoani Kagera.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akitoa salamu za mwisho kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasi ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Marehemu Balozi Edwin Rutageruka katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Musibuka, Wilayani Misenyi Mkoani Kagera

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine akitoa salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa familia ya marehemu Balozi Edwin Rutageruka wakati wa mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Musibuka Wilayani Misenyi Mkoani Kagera 

Sehemu ya Waombolezaji wakiwa msibani



Askofu msaidizi wa Jimbo katoliki la Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini akiongoza ibada ya mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasi ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Marehemu Balozi Edwin Rutageruka katika mazishi yaliyofanyika jana kijijini kwake Musibuka, Wilayani Misenyi Mkoani Kagera

Askofu msaidizi wa Jimbo katoliki la Bukoba Mhashamu Methodius Kilaini akisimika msalaba kwenye kaburi la aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Diplomasi ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Marehemu Balozi Edwin Rutageruka  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) pamoja na mume wake wakiweka shada la maua kwenye kaburi la Balozi Edwin Rutageruka

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiweka taji kwenye kaburi la Balozi Edwin Rutageruka

Baadhi ya Wakurugenzi wa Idara na Vitengo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiweka mashada ya maua kwenye kaburi la Balozi Edwin Rutageruka kwa niaba ya Menejimenti ya Wizara hiyo



Naibu Waziri Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja kwenye kaburi la Marehemu Balozi Edwin Rutageruka mara baada ya maziko ya Balozi Edwin Rutegaruka

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.