Picha ya pamoja. |
Monday, June 10, 2024
BALOZI MUSSA AWAASA VIJANA KUWA MABALOZI WAZURI NJE YA NCHI
KATIBU MKUU MAMBO YA NJE AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KIKAO CHA SADC MASUALA YA SIASA NA DIPLOMASIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo ameongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Kikao cha Pamoja cha Kamati Ndogo ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuhusu masuala ya Siasa na Diplomasia kilichofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 10 Juni 2024.
Akifungua kikao hicho ambacho kimefanyika kwa ngazi ya Makatibu Wakuu , Mwenyekiti ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Zambia, Bi. Etambuyu Gundersen aliwataka wajumbe kujadili na kutoa mapendekezo katika agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao ili hatimaye mapendekezo hayo yawasilishwe kwenye kikao cha Mawaziri kitakachofanyika mwezi Julai 2024 kwa ajili ya kuridhiwa.
Akichangia hoja kwenye kikao hicho, Balozi Shelukindo amezishukuru na kuzipongeza Nchi Wanachama wa SADC kwa kufanikisha uundwaji na uzinduzi wa Sanamu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliofanyika mwezi Februari 2024 katika Makao Makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Amesema uzinduzi huo ambao ulihudhuriwa na idadi kubwa ya wakuu wa nchi wa Afrika ulidhihirisha namna ambavyo wanaenzi mchango mkubwa uliotolewa na Hayati Mwalimu Nyerere kwenye Ukombozi wa Nchi za Kusini mwa Afrika.
Kadhalika amesema Tanzania inaendelea na mawasilianao ya ndani ili kukamilisha Mpango wa Taifa wa Utekelezaji wa Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 kuhusu kuwawezesha Wanawake kushiriki katika juhudi za kutatua, kuzuia na kudhibiti migogoro duniani huku akizipongeza nchi zilizokamilisha Mpango huo ikiwemo Zimbawe na Madagascar.
Vilevile, ametumia fursa hiyo kuzipongeza Jamhuri ya Afrika Kusini na Jamhuri ya Madagascar kwa kufanikisha uchaguzi mkuu wa Rais na Wabunge uliofanyika kwenye nchi hizo kwa amani na utulivu tarehe 29 Mei 2024 mtawalia.
Amesema, kikanda uchaguzi katika nchi hizi mbili umeakisi viwango vya kimataifa vya demokrasia pamoja na kanuni na miongozo ya SADC kuhusu uchaguzi unaofuata misingi ya demokrasia.
Kikao hicho ambacho kimefanyika kwa ajili ya kuandaa mkutano wa Mawaziri unaotarajiwa kufanyika mwezi Julai 2024, kimehudhuriwa na Nchi za Tanzania, Lesotho, Eswatini, Botswana, Angola, Namibia, Afrika Kusini, Shelisheli , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Zambia na Zimbabwe.
Kikao kikiendelea |
Friday, June 7, 2024
WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA CANADA AKUTANA NA MABALOZI WA AFRIKA
Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada, Mhe. Melanie Joly akizungumza na Mabalozi wa Afrika waliopo nchini humo uliofanyika hivi karibuni jijini Ottawa |
Monday, June 3, 2024
MKUTANO WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI LINALOSHUGHULIKIA MASUALA YA EAC NA MIPANGO WAANZA ARUSHA
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Benjamini Mwesiga akichangia hoja kwenye Mkutano 33 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango ngazi ya Wataalam unaofanyika jijini Arusha |
Mkutano ukiendelea |
Mkutano ukiendelea |
Meza kuu wakiongoza Mkutano 33 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango ngazi ya Wataalam unaofanyika jijini Arusha |
KAMATI YA BUNGE YA NUU YASISITIZA UWAJIBIKAJI
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) imeisisitiza Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuendelea kusimamia utekelezaji wa miradi yake kwa wakati iliyo katika hatua mbalimbali.
Msisitizo huo umetolewa katika kikao cha ufuatiliaji kati ya kamati hiyo na Menejimenti ya Wizara kilichofanyika Bungeni jijini Dodoma, tarehe 3 Juni 2024.
Akiwasilisha taarifa ya miradi ya ujenzi iliyo chini ya Wizara, Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato (Mb.), kwa niaba ya Mhe. January Makamba (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameeleza kuwa, Wizara imewekeza nguvu kubwa katika kuhakikisha mradi wa ujenzi wa jengo la ofisi ya Wizara lililopo mji wa Serikali Mtumba, Dodoma na jengo la mihadhara la Kituo cha Uhusiano cha Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim kilichopo Kurasini, jijini Dar es Salaam yanakamilika kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya NUU na Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, Mhe. Vita Kawawa (Mb.) alieleza juu ya umuhimu wa Wizara kushirikiana na Kamati hiyo katika kutekeleza majukumu yake.
Aidha, wajumbe wa Kamati wamepongeza jitihada zilizofanywa na Wizara katika utekelezaji wa miradi na wamesisitiza weledi katika usimamizi wa matumizi ya kifedha na mikataba ya miradi ya ujenzi.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amewashukuru wajumbe wa Kamati ya NUU kwa kuendelea kuwa chachu katika usimamizi wa miradi inayotekelezwa na Wizara. Pia, amewaalika Wajumbe wa Kamati hiyo kutembelea mradi wa ujenzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu unaotekelezwa katika eneo la Lakilaki, Arusha.
========================================
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU) wakifuatilia kikao. |
Sehemu ya Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikifuatilia kikao. |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Menejimenti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikifuatilia kikao. |
Kikao kikiendelea. |
Friday, May 31, 2024
MAWAZIRI WA BIASHARA ,VIWANDA, FEDHA NA UWEKEZAJI WA EAC WAAZMIA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mhe. Stephen Byabato akifuatilia mkutano |
Mkutano ukiendelea |
Mkutano ukiendelea |