Friday, October 18, 2019
Thursday, October 17, 2019
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 18 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC KUANZIA TAREHE 7-8 NOVEMBA 2019
17 Oktoba, 2019
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA 18 WA MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE WA NCHI ZA AFRIKA NA NORDIC KUANZIA TAREHE 7-8 NOVEMBA 2019
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi za Afrika na Nordic (Norway, Denmark, Finland, Sweden na Iceland) unaotarajiwa kufanyika tarehe 08 Novemba 2019 kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huu kufanyika hapa nchini tangu kuanzishwa kwake mwaka 2000.
Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na washiriki takribani 250 ambao kati yao thelathini na nne (34) ni Mawaziri wa Mambo ya Nje akiwemo Mhe. Prof. Palamagamba J.A.M. Kabudi (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kadhalika, Mabalozi wa nchi shiriki za Afrika katika nchi za Nordic, Mabalozi wa nchi za Nordic hapa nchini, watendaji kutoka Wizara za Mambo ya Nje za nchi shiriki, wawakilishi wa taasisi za biashara na uwekezaji na Wafanyabiashara za hapa nchini wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huu.
Lengo la kuanzishwa kwa mkutano huu, ambao kwa mara ya kwanza ulifanyika mwaka 2000, ilikuwa ni kutoa nafasi kwa nchi za Nordic na nchi chache za Afrika marafiki zao wa karibu, kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili, kuainisha vipaumbele katika ushirikiano huo na kuweka mikakati ya pamoja ya kutekeleza vipaumbele hivyo. Nchi za Afrika na Nordic zimekuwa zikipokezana uenyeji wa mikutano hii kila mwaka. Mwaka 2017, mkutano huu ulifanyika Abuja, Nigeria na mwaka 2018 ulifanyika Copenhagen, Denmark na mwaka huu, utafanyika Tanzania.
Kwa mwaka huu, mkutano huu utajadili namna ya kuimarisha mahusiano yenye tija kwa maendeleo ya nchi washiriki hususan namna ya kukuza ushirikiano kwenye sekta ya biashara na uwekezaji kwa maendeleo endelevu. Aidha, ushirikiano kwenye masuala ya ulinzi na usalama unatarajiwa kupewa kipaumbele kwenye mkutano huu ikizingatiwa kuwa utekelezaji wa shughuli za maendeleo unategemea uwepo wa amani na usalama.
Tanzania ni nchi ya kipaumbele kwa nchi za Nordic. Ushirikiano kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulianza hata kabla ya uhuru wa Tanganyika ambapo wamisionari kutoka nchi hizo walikuja kufanya kazi hapa nchini kwenye sekta za afya na elimu. Katika sekta ya elimu, nchi hizo zilianzisha Kituo cha Kilimo cha Uyole na Kituo cha Elimu cha Kibaha kupitia Mradi wa Nordic-Tanganyika Project. Ushirikiano wa karibu kati ya Tanzania na nchi za Nordic ulichangiwa kwa kiwango kikubwa na falsafa zilizokuwa zinafanana kuhusu maendeleo ya watu, ukombozi wa Afrika, urafiki miongoni mwa viongozi wetu na nafasi ya kimkakati ya Tanzania katika Bara la Afrika.
Hadi sasa, Tanzania ni nchi pekee iliyopokea msaada mkubwa kifedha kutoka katika nchi za Nordic. Kuanzia mwaka 2013 hadi 2019, Tanzania imepokea takribani shilingi za kitanzania bilioni 900 kutoka kwa nchi za Nordic. Nchi hizo zimekuwa zikisaidia sekta mbalimbali hapa nchini ikiwemo: elimu; afya; miundombinu; nishati; TEHAMA; utafiti; ukusanyaji wa kodi; bajeti; misitu; usawa wa jinsia; hali ya hewa; na ukuzaji wa sekta ya biashara. Kufuatia ushirikiano huu wa kihistoria kati ya Tanzania na nchi za Nordic, nchi hizo ziliiomba Serikali ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano wa mwaka huu na Serikali kuridhia kwa minajili ya kuendelea kuboresha ushirikiano kati ya pande hizi mbili kwa manufaa ya pande zote.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam.
Job Announcement at the United Nations Environment Programme
PRESS RELEASE
Job Announcement at the United Nations Environment Programme
The Ministry of Foreign Affairs and
East African Cooperation has received vacancy notification from the United Nations Environment
Programme (UNEP) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Chief
Scientist available at the Science Division.
Application details can be found on the https://www.unenvironment.org/work-with-us
Closing date for application is 24th October
2019.
Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East
African Cooperation,
|
Wednesday, October 16, 2019
Balozi Kairuki awasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Vietnam
Tuesday, October 15, 2019
PROF KABUDI KATIKA KONGAMANO LA MIAKA 20 BILA NYERERE - UDSM
Monday, October 14, 2019
Wanafunzi Uganda Wafanya Mdahalo kuhusu Mwalimu Nyerere
Uongozi wa wanafunzi wa Tanzania wanaosoma nchini Uganda wakiwa katika picha ya pamoja. |
Sunday, October 13, 2019
WIZARA YA MAMBO YA NJE YAKABIDHIWA JENGO JIPYA NA CHINA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) na Balozi wa China hapa Nchini, Balozi Wang Ke,wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharii lililojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Jamhuri ya Watu China na kukabidhiwa Serikaali ya Tanzania. Tukio hilo limefanyika jijini Dar es Salaam. |
Naibu katibu Mkuu, Mizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi na Balozi wa China hapa Nchini, Balozi Wang Ke wakisaini mkataba wa makabidhiano ya jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Anayeshuhudia ni
|
Balozi wa China Nchini, Balozi Wang Ke akishikana mkono na Naibu katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Ramadhani Mwinyi mara baada ya kubadilishana nyaraka walizosaini za kukabidhiana Jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililojengwa kwa msaada wa Jamhuri ya Watu wa China Jijini Dar es Salaam. |
Balozi wa China hapa Nchini, Balozi Wang Ke akisoma hotuba yake wakati wa makabidhiano ya jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), akisoma hotuba yake wakati wa makabidhiano ya jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yaliyofanyika jijini Dar es salaam
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), Balozi wa China nchini nchini Tanzania Wang Ke na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje mara baada ya kukabidhiana jengo jipya la wizara hiyo.
|
Jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lililopo jijini Dar Es Salaam lililojengwa kwa msaada wa Jamhuri ya Watu wa China kwa jailli ya matumizi ya Ofisi za Wizara hiyo. |
Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki wamalizika Jijini Arusha.
12 Oktoba 2019, Arusha.
Mkutano wa 30 wa Baraza la
kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango
umemalizika tarehe 12 Oktoba 2019 kwenye Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Jijini Arusha - Tanzania. Mkutano huu wa siku sita (06) umefanyika
katika Ngazi zifuatazo:
- Mkutano
katika Ngazi ya Maafisa Waandamizi tarehe 7 na 8 Oktoba, 2019;
- Mkutano
katika Ngazi ya Makatibu Wakuu tarehe 9 na 10 Oktoba 2019 na
- Mkutano
katika Ngazi ya Mawaziri tarehe 11 na 12 Oktoba 2019.
Ujumbe wa Tanzania katika
mkutano huu umeongozwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb) akisaidiana na Waziri wa
Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent L. Bashungwa (Mb); Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb); Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaju (Mb); Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mary Mwanjelwa
pamoja na viongozi wengine waandamizi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania.
Mkutano huu umetoa maamuzi na
maelekezo mbalimbali ya kisera na kimkakati kwa Nchi Wanachama pamoja na
Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu Utekelezaji wa
maamuzi na maelekezo ya mikutano ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki iliyopita pamoja na mkutano wa 10 hadi 28
wa Baraza la kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya
Afrika Mashariki na Mipango; Utekelezaji wa Soko la pamoja la Afrika Mashariki; Utekeleaji
wa maagizo katika taarifa ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (2000 –
2017); Vipaumbele vya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa mwaka 2020/21; Maelekezo
kuhusiana na mikutano ya Wakuu wa taasisi za masuala ya Uhamiaji na Kazi za
Jumuiya, na maagizo ya hadidu za rejea za maandalizi ya mkakati wa mpango wa
sita wa maendeleo ya Afrika Mashariki (2021/22).
Aidha, mkutano huu ulitoa mapendekezo katika taarifa
ya hali ya ulipaji wa michango ya Nchi Wanachama katika Jumuiya; Taarifa ya uhamasishaji
katika masuala ya rasilimali za jumuiya ya Afrika Mashariki na mikakati ya
ushirikiano; Taarifa ya Tume ya Ukaguzi ya Jumuiya kwa mwaka 2017/18; Taarifa
ya maendeleo ya makubaliano ya maeneo huru ya biashara katika utatu wa
COMESA-EAC-SADC;Taarifa ya maendeleo ya makubaliano kuhusu eneo huru la
kibiashara barani Afrika (AFCFTA); Taarifa ya maendeleo ya masuala ya kisiasa,
na Kalenda ya majukumu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa kipindi cha mwezi
Julai hadi Desemba 2019.
Vilevile, wajumbe wa mkutano wamejadili
kuhusiana na maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 tangu kuanzishwa kwa jumuiya
ya Afrika Mashariki mwaka 2000, baada ya kuvunjika kwa jumuiya ya awali
iliyoundwa mwaka 1967 na kuvunjika mwaka 1977.
Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki umemalizika tarehe 12 Oktoba 2019 Jijini Arusha, Tanzania. Pichani ni viongozi wa ujumbe kutoka Nchi Wanachama katika ngazi ya Mawaziri wakisaini maamuzi na mapendekezo waliyoyatoa katika mkutano wa 30 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango. Kutoka kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro (Mb); Waziri anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mshariki, Mambo ya Nje na Uhusiano wa Kimataifa kutoka Rwanda, Mhe. Balozi Olivier J.P Nduhungiuhe; Katibu Mkuu Wizara ya Afrika Mashariki na Maendeleo ya Kikanda kutoka Kenya, Mhe. Ken M. Obura; Waziri Ofisi ya Rais anayeshughulikia masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Burundi, Mhe. Isabelle Ndahayo; Waziri wa Masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Uganda, Mhe. Rt. Dkt. Kirunda Kivejinja; pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Mhe. Paul Mayom Akec kutoka. |
Mawaziri wa Serikali ya Tanzania walioshiriki katika mkutano wa 30 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango wakiwa katika kikao cha ndani cha maandalizi pamoja na maafisa wengine waandamizi kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hawapo pichani). Pichani; Kutoka kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas D. Ndumbaro, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Innocent L. Bashungwa (Mb); Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Balozi Dkt. Augustine P. Mahiga (Mb); Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Mary Mwanjelwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaju (Mb). |
Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen P. Mbundi akijadili jambo pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Miundombinu, Mhandisi Steven D. M. Mlote (kulia) na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia sekta za uzalishaji na jamii, Mhe. Christophe Bazivamo (kushoto). |
Saturday, October 12, 2019
Watalii kutoka Israel wawasili nchini kwa ziara ya siku nane.
Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Bi. Devotha Mdachi akiwakaribisha watalii kutoka nchini Israel mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro kwa ndege ya shirika la El Al Israel, leo tarehe 12 Oktoba 2019. Watalii wapatao 920 wameendelea kuwasili nchini katika makundi tofauti ambapo Watalii wanaowasili kupitia uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro wanatarajiwa kufika 720 na Watalii 200 kwa wale waliokwishawasili kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar. |
Sehemu ya Watalii kutoka nchini Israel wakipata huduma mara baada ya kuwasili ndani ya Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Wakiwa nchini watalii hao watatembelea hifadhi ya Serengeti, Ngorongoro, Tarangire, Manyara pamoja na Zanzibar ili kuweza kujionea vivutio mbalimbali na kujifunza mambo mbalimbali ya mila na utamaduni wa kitanzania. |
Sehemu nyingine ya Watalii kutoka nchini Israel wakipata huduma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. |
Kikundi cha ngoma cha Wamasai kikitumbuiza katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikiwa ni ishara ya kuwalaki wageni hao. |
Friday, October 11, 2019
Madereva wa taxi kutoka Uingereza wapanda Mlima Kilimanjaro
11 Oktoba 2019,
Dodoma
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Madereva wa taxi kutoka Uingereza wapanda Mlima Kilimanjaro
Timu ya madereva taxi watano kutoka Uingereza
ilifanya ziara nchini kuanzia tarehe 28 Septemba hadi 10 Oktoba 2019. Ziara
hiyo iliratibiwa na Wizara kupitia Ubalozi wetu London kwa kushirikiana na TTB.
Timu hiyo ilikuja nchini kwa ajili ya kupanda mlima Kilimanjaro ikiwa ni zoezi
la hisani ili kuchangisha fedha kwa ajili ya maveterani wa kijeshi (military
veterans) huko Uingereza.
Katika kutambua uamuzi mzuri wa timu hiyo kuuchagua
mlima Kilimanjaro kwa zoezi hilo la hisani na kwa malengo ya kunufaika na ujio
wao katika kutangaza vivutio vyetu vya utalii nchini Uingereza, Wizara ya Mambo
ya Nje kwa kushirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) iliwaandalia timu hiyo
ziara ya kutembelea vivutio vya utalii mbalimbali hapa nchini zikiwemo mbuga za
wanyama za Serengeti, Ngorongoro na Tarangire.
Vilevile, Timu hiyo ya madereva taxi baada ya
kumaliza kutembelea vivutio vilivyotajwa hapo juu walitangazwa kuwa mabalozi wa
hiari wa utalii (tourism goodwill
ambassadors) wa Tanzania kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii vya hapa
nchini wawapo katika shughuli zao huko Uingereza. Hafla ya kuwatangaza
ilifanyika Hotel ya Mount Meru Arusha. Baada ya kutangazwa kuwa mabalozi wa hiari,
walisaini Hati ya Makubaliano (MoU) kati ya timu hiyo na TTB tayari kwa
kutekeleza majukumu yao.
Tukio hilo lilihudhuliwa na Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Nzuki, akimuwakilisha Mhe. Dkt.
Hamisi Kigwangallah (Mb), Waziri wa Maliasili na Utalii na Mkuu wa mkoa wa
Arusha Mhe. Mrisho Gambo. Aidha, Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo alikuwa Balozi
wa Uingereza hapa nchini, Mhe. Sarah Cooke.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
|
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. Sarah Cooke akizungumza katika hafla hiyo. |
Mkurugenzi Mtendaji wa TTB, Dkt. Devota Mdachi na Kiongozi wa Madereva wa Taxi wakiweka saini MoU. |
| ||
|
Timu ya Madereva kutoka Uingereza ikipanda mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya maveterani wa kijeshi (military veterans) huko Uingereza. |
Timu ya Madereva wa Taxi kutoka Uingereza ikiwa katika kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak). |
Thursday, October 10, 2019
TAARIFA KWA UMMA
UJIO WA WATALII ZAIDI YA 1000 KUTOKA ISRAEL
Tanzania inatarajia kupokea watalii zaidi ya 1000 kutoka nchini Israel ambao wanakuja nchini kwa ajili ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mwezi huu wa Oktoba.
Kundi la kwanza lililokuwa na zaidi ya watalii 200 liliwasili nchini kuanzia tarehe 05 Oktoba na kundi la pili lenye zaidi ya watalii 520 linatarajiwa kuwasili nchini tarehe 12 na kundi la tatu lenye watalii zaidi ya 200 litawasili nchini tarehe 13 Oktoba kupitia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Watalii wengine zaidi wanatarajiwa kuwasili nchini mwezi huu baada ya Makampuni ya Uwakala wa Utalii kukamilisha taratibu za safari zao.
Watalii hao wanatarajiwa kutembelea Visiwa vya Zanzibar, Hifadhi za Taifa za Serengeti, Tarangire na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Ujio wa watalii hao unatokana na jitihada za kuitangaza nchi zinazofanywa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini Israel kwa kushirikiana na wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi.
Tanzania imejipanga kuwapokea na kuwatembeza watalii hao katika vivutio vya utalii vilivyoko nchini. Serikali inawakaribisha watalii hao kutembelea vivutio hivyo vya utalii ambavyo nchi imebarikiwa kuwa navyo ili wakawe mabalozi wazuri wa kuitangaza Tanzania nchini kwao na kwingine watakakokwenda.
Imetolewa na:
Dkt. Faraji K. Mnyepe
Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
DODOMA
PROF. KABUDI AHUDHURIA MAADHIMISHO YA SIKU YA HISPANIA HAPA NCHINI
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini. Kulia kwa Prof. Palamagamba John Kabudi ni Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero. |
Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero akihutubia wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi huyo hapa Nchini. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akigongeana glasi ishara ya kutakiana kheri na Balozi wa Hispania hapa Nchini Mhe. Fransisca Maria Pedro's Carretero,wakati wa maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini. |
Baadhi ya waalikwa walihohudhuria maadhimisho ya siku ya Uhispania yaliyofanyika Jijini Dar Es Salaam kwenye Makazi ya Balozi wa Uhispania hapa Nchini. |
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu
Mkutano wa 30 wa Baraza la Mawaziri la kisekta linaloshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango waendelea jijini Arusha katika ngazi ya Makatibu Wakuu. Mkutano katika ngazi hiyo ulikuwa wa siku mbili na umemalizika leo. Pamoja na mambo mengine, mkutano umejadili masuala mbalimbali ya utekelezaji ya jumuiya ya Afrika Mashariki na kutoa mapendekezo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri utakaofanyika tarehe 11 na 12 Oktoba 2019. Pichani; wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa mkutano ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka Rwanda, Balozi Richard Masozera akiongoza mkutano huo, wa pili kutoka kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Miundombinu, Mhandisi Steven D. M. Mlote, kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia sekta za uzalishaji na jamii, Mhe. Christophe Bazivamo na kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara inayoshughulikia masuala ya jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Kenya, Bw. Rafael Kanoth. |
Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania katika mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro (kushoto) akisaini taarifa ya mapendekezo mbalimbali katika mkutano huo kwaajili ya kuwasilisha taarifa hiyo katika mkutano wa ngazi ya Mawaziri. Pembeni yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome akishuhudia zoezi la utiaji saini. |
Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Amina Shaaban pamoja na Dkt. Ndumbaro na Prof. Mchome wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo. |
Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama, Balozi Stephen P. Mbundi pamoja na wajumbe wengine wa mkutano wakifuatilia majadiliano katika mkutano huo. |
Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dkt. Evaristo Longopa (kushoto) pamoja na sehemu nyingine ya ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo wakifuatilia majadiliano. |
Sehemu nyingine ya wajumbe wa Tanzania wakifuatilia majadiliano katika mkutano. |
Viongozi wa ujumbe wa mkutano katika ngazi ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wakikamilisha zoezi la utiaji saini wa taarifa ya mapendekezo ya mkutano huo. |
Wednesday, October 9, 2019
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI INDIA WAANZA MAJUKUMU YA UENYEKITI WA KUNDI LA MABALOZI KUTOKA NCHI ZA SADC WALIOPO NCHINI HUMO
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akipokea Makabrasha kutoka kwa Balozi wa Namibia nchini India, Mhe. Gabriel P. Sinimbo ikiwa ni ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa Kundi la Mabalozi wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC ) waliopo India. Tanzania ilipokea uenyekiti wa Jumuiya hiyo kutoka kwa Namibia mwezi Agosti 2019 wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC uliofanyika jijini Dar es Salaam.
|
Balozi Luvanda (katikati) akizungumza mara baada ya kupokea uenyekiti wa kundi la Mabalozi kutoka Nchi za SADC waliopo India. Katika picha ni Balozi Sinimbo (kulia) kutoka Namibia na Balozi E.A Ferreira (kushoto) kutoka Msumbiji. |
Mkutano ukiendelea |
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na na
Mabalozi kutoka nchi za SADC waliopo India pamoja na Maafisa wa Ubalozi mara baada ya kikao
cha Mabalozi hao kilichofanyika kwenye Jengo la Ubalozi jijini New Delhi.
|
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa
Zambia nchini India, Mhe. Judith K. Kapijimpanga ambaye kabla ya kuiwakilisha
Zambia nchini India alihudumu katika nafasi hiyo nchini Tanzania.
|
Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi, Dkt. Kheri Goloka (kushoto) na Bi. Natihaika Msuya (katikati) wakiwa katika picha ya pamoja na
Mwenyekiti wa kundi la Mabalozi wa nchi za SADC nchini India aliyemaliza muda
wake Balozi wa Namibia Mhe. Gabriel P. Sinimbo.
|
Subscribe to:
Posts (Atom)