Sunday, January 19, 2020
UJUMBE MAALUM WA RAIS DKT MAGUFULI WAWASILI MUSCAT - OMAN
Saturday, January 18, 2020
TANZANIA YATANGAZA UTALII UHOLANZI
Balozi Irene Kasyanju ( wa pili kulia) akiwa na wawakilishi wa TTB na Kampuni ya MAKASA Safaris kutoka Moshi, Kilimanjaro. |
Friday, January 17, 2020
KAMPUNI YA ALRIFAI YA KUWAIT YATEMBELEA TANZANIA, KUANGALIA FURSA ZA UWEKEZAJI
Na
Mwandishi wetu,
Kampuni
ya Alrifai inayojihusisha na biashara ya mazao mchanganyiko iko nchini kwa
lengo la kuangalia fursa za uwekezaji hususani kununua zao la korosho na kahawa
na kuangalia uwezekano wa kujenga kiwanda cha kuchakata zao la korosho nchini.
Ujumbe
wa watu watatu (3) ukiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo ya Alrifai,
Bwn. Abdellah Foaud, Meneja Viwango Bwn. Ahmed Mohamed Bahie pamoja na Meneja
wa Manunuzi Bwn. M. K Hussin uko nchini tangu tarehe 13 Januari, 2020 kwa lengo
kuu la kuangalia uwezekano wa Kununua korosho zilizokwisha chakatwa pamoja na
kahawa zilizokobolewa na pia kuona maeneo ambayo wanaweza kuwekeza katika
kiwanda cha kuchakata korosho.
Ujumbe
huo ulifanya kikako na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Bodi ya Kahawa
(TCB), Mamlaka ya Maendeieo ya Biashara Tanzania (TanTrade) pamoja na Bodi ya Mazao
Mchanganyiko na kuweza kupata fursa ya kufahamu kwa undani juu ya taratibu za
ununuzi wa mazao hayo pamoja na taratibu za uwekezaji wa kiwanda cha kuchakata
korosho hapa nchini.
Akitoa
maelezo juu ya uzalishwaji wa zao la Korosho nchini, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma
za Biashara wa TanTrade, Bi. Twilumba Mlelwa alisema kuwa korosho ghafi kwa
mwaka huzalishwa kati ya tani 250,000 na tani 300,000 ambapo kiasi kikubwa
huzalishwa Mtwara, Lindi, Ruvuma (Tunduru), Pwani (Mkuranga na Kibaha) pamoja
na Tanga.
"Naomba
niwatoe shaka juu ya zao la korosho kwani kwa sasa viwanda vya korosho ni 18
ambapo vinauwezo wa huhifadhi tani 63,000 za korosho lakini kwa sasa
vinavyofanya kazi ni 13 na vina uwezo wa kubangua tani 43,000" Amesema Bi.
Mlelwa
Kwa
upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni hiyo ya Alrifai, Bwn. Abdellah
Foaud,ameushukuru Ubalozi wa Tanzania nchini Kuwait kwa ushirikiano alioupata
kutoka ubalozini hadi kwa viongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje kwa kuweza
kuratibu zoezi la kukuagua zao la Korosho, kahawa pamoja na karafuu.
"Binafsi
nashukuru kwa ushirikiano nilioupata kwa viongozi wa Mkoa wa Lindi na Mtwara, Bodi
ya Mazao Mchanganyiko, TIC, TanTrade, Bodi ya Kahawa pamoja na Balozi Mhandisi
Aisha Amour kwa namna alivyolisimamia jambo hili tangu likiwa wazo mpaka sasa
tunapoelekea kwenye utekelezaji niwaahidi tu kuwa utekelezaji wa kununua mazao
haya utaanza mara moja mara tu baada ya kufanya maamuzi na mikataba itasainiwa kwa
mujibu wa sheria," amesema Bwn. Foaud
Aidha,
mbali na maelezo ya uzalishaji wa zao la Korosho nchini, ujumbe huo pia ulipata
fursa ya kuona zao la korosho lililohifadhiwa katika ghala la Serikali eneo la
Kurasini jijini Dar es Salaam na uliridhishwa na zao hilo na kuahidi kuwekeza
nchini kwani korosho zinzazalishwa ni nzuri na bora.
Meneja
Viwango Bwn. Ahmed Mohamed Bahie amesema "tumejionea wenyewe ubora wa
korosho, kahawa na karafuu kwa kweli ni nzuri sana na sote tumeridhika na ubora
huo. Tutajitahidi kukamilisha taratibu zote muhimu na kuanza mara moja uagizaji
wa korosho na baadae kujenga kiwanda cha kuchakata korosho hapa Tanzania,".
Ujumbe
huo ulipata fursa ya kutembelea maeneo kadhaa kwa lengo la kupata maelezo
kuhusu taratibu na fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini, maeneo hayo ni pamoja
na mikoa ya Lindi, Mtwara na Kilimanjaro pamoja na Zanzibar ambapo waliweza
kuona uzalishaji wa Karafuu.
Ujio
wa kampuni hiyo ni matokeo ya juhudi za Ubalozi wa Tanzania nchini Kuwait ambapo
ulifanya mazungumzo na Kampuni ya Alrifai inayojihusisha na biashara ya mazao
mchanganyiko kuhusu nia yao ya kununua zao la korosho na kahawa na kuangalia
uwezekano wa kujenga kiwanda cha kuchakata zao la korosho nchini Tanzania.
Kaimu
Mkurugenzi wa Bodi ya kahawa nchini(TCB),Primus Kimaryo akiwaelezea jambo viongozi
wa Kampuni Alrifai juu ya upatikanaji wa zao la kahawa nchini
|
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Alrifai, Bwn. Abdellah Foaud, akiongea na viongozi
kutoka TIC, TCB, TanTrade pamoja na Bodi ya Mazao Mchanganyiko wakati
walipokutana katika mkutano uliofanyika Jijini Dar es Salaam
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Alrifai, Bwn. Abdellah Foaud pamoja na Meneja wa
Manunuzi Bwn. Hussain wakikagua korosho zilizohifadhiwa kwenye moja ya ghala hapa
nchini, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Dkt. Anselm
Moshi
|
Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Mazao Mchanganyiko, Dkt. Anselm Moshi akimuonyesha Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Alrifai, Bwn. Abdellah Foaud jinsi korosho zinavyohifadhiwa
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Alrifai, Bwn. Abdellah Foaud akiuliza kitu wakati
alipotembelea moja kati ya viwanda vya kubangua korosho Mkoani Mtwara
Ujumbe
wa Kampuni ya Alrifai ukiwa katika moja ya kiwanda cha kubangua korosho mkoani
Mtwara
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bwn.
Gelasius Byakanwa (kulia) akiwa ofisini kwake na Ujumbe wa Kampuni ya Alrifai
ambapo ujumbe huo ulitembelea pia chuo cha utafiti wa Korosho Nariendele na
baadhi ya viwanda vya kubangua korosho
Ujumbe
wa Kampuni ya Alrifai ukiwa katika moja ya duka la kuuza karafuu Mjini
Zanzibar
Thursday, January 16, 2020
PROF. KABUDI ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA SULTAN WA OMAN
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akipokelewa na Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi katika ubalozi wa Oman - Tanzania. Prof. Kabudi amekwenda ubalozini hapo kwa ajili ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Sultan wa Oman, Sultan Qaboos bin Said. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Oman uliopo Jijini Dar es Salaam kufutia kifo cha Sultan wa Oman, Sultan Qaboos bin Said. Waliosimama ni Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ramadhan Muombwa Mwinyi. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Oman uliopo Jijini Dar es Salaam kufutia kifo cha Sultan wa Oman, Sultan Qaboos bin Said. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi,Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Ramadhan Muombwa Mwinyi na viongozi wa Ubalozi wa Oman hapa Nchini pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. |
Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiagana na Balozi wa Oman hapa Nchini Mhe. Ally Abdallah Almahruqi,mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Sultan wa Oman,Sultan Qaboos bin Said.
Wednesday, January 15, 2020
SERIKALI YAAGIZA CHUO CHA DIPLOMASIA KUTOA ELIMU KWA VITENDO ZAIDI
Serikali
imekitaka Chuo cha Diplomasia kutoa taaluma ya vitendo kwa wanafunzi
wanaojiunga na chuo hicho ili kuwawezesha wahitimu kuwa na mchango katika Taifa
hususani wakati huu wa utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi.
Akihutubia
mahafali ya 22 ya Chuo cha Diplomasia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) ambaye ni Mgeni Rasmi
katika mhafali hayo, amesema Serikali itafurahi kusikia chuo kinatoa mafunzo ya
stratejia, jiopolitiki na demokrasia pamoja na haki za binadamu hasa kwa
muktadha wa kiafrika.
Waziri
Kabudi ameongeza kuwa taaluma inayotolewa na Chuo hicho isiwe ya nadharia pekee
bali iambatane na vitendo ili elimu hiyo itumike kusaidia kufafanua masuala ya
Kidiplomasia na uhusiano wa Kimataifa yanayotokea duniani.
"Nakiagiza
Chuo kuandaa mpango mkakati wa mafunzo kwa vitendo ili tuangalie ni jinsi gani
Wizara inaweza kusaidia. Aidha, Chuo kipitie mitaala yake mara kwa mara kama
ilivyopendekezwa ili kisipitwe na wakati. Dunia inabadilika kwa kasi. Nasi
hatuna budi kwenda kwa kasi hiyo," Amesema Prof. Kabudi.
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa, ni vyema Chuo kikawa mstari wa mbele kutoa mafunzo hayo
kwa wanadiplomasia, wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, na wafanyabiashara
waliopo hapa nchini.
"Nimefarijika
kusikia kuwa mmefanya mazungumzo na Chuo cha ISRI cha Angola kwa nia ya kufikia
makubaliano ya kutoa mafunzo ya lugha ya Kiswahili nchini Angola ambapo rasimu
ya Hati ya Makubaliano imeandaliwa na inasubiri kusainiwa," Amesema Prof.
Kabudi.
Prof.
Kabudi aliongeza kuwa, Serikali inatambua kwamba Balozi za Iran, Libya, Urusi,
Indonesia na China zimekuwa zikitumia wigo huu wa ushirikiano na kubadilishana
uzoefu, kutoa mada mbalimbali chuoni hapo. Aidha, alitumia fursa hiyo
kuzikaribisha ofisi nyingine za kibalozi hapa nchini kutembelea Chuo cha
Diplomasia na kutoa uzoefu wao kwa vinafunzi pamoja na wakufunzi. Hivyo basi,
ni vyema menejimenti ya Chuo kutoa mwaliko kwa Balozi zote na wawakilishi wa
kudumu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini kuja kutoa uzoefu wao kwani nayo
itakuwa sehemu ya diplomasia ya ulimwengu.
Awali
akimkaribisha mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Drkt. Faraji Mnyepe amesema wahitimu 453 wametunikiwa
vyeti baada ya kupata mafunzo na kufuzu ambapo kati yao 98 ni wa ngazi ya
Astashahada ya Msingi, 119 ni wa Stashahada ya kawaida, 130 ni wa Shahada, 83
ni wa Stashahada ya Uzamili, 45 Stashahada ya uzamili wa diplomasia ya uchumi.
"Nina
imani kuwa wahitimu wa leo kama wale wa miaka ya iliyopita, wameiva ipasavyo
katika fani za mahusiano ya kimataifa, Diplomasia na Stratejia. Naamin pia kuwa
mtakuwa rasilimali kubwa kwa Taifa letu katika fani mlizosomea" Amesema
Dkt. Mnyepe.
Dkt.
Mnyepe ameongeza kuwa, katika mwaka wa masomo 2019/20 chuo kimeweza kuongeza
udahili wa wanafunzi kutoka 1029 kwa 2018/19 hadi kufikia 1275 kwa mwaka wa
masomo 2019/20 ambapo pamoja na mambo mengine juhudi zinaendelea katika kutanua
wigo wa udahili kwa kuanziasha udahili wa mwezi Machi pamoja na kuanzisha
program mpya.
"Katika mwaka wa masomo 2019/20 chuo pia
kimeweza kupanua mawanda ya program zake kwa kuongeza idadi ya program za muda
mrefu. Chuo kimeanzisha Stashahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Amani na
Udhibiti wa Migogoro ambapo kwa sasa program hii inaendeshwa Dar es Salaam na
Dodoma," Amesema Dkt. Mnyepe.
Chuo
cha Diplomasia kilianzishwa rasmi tarehe 13 Januari 1978 kwa kusainiwa
Makubaliano yaliyofanywa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi zetu mbili wa wakati
huo, Mhe. Benjamini William Mkapa wa Tanzania na Mhe. Joaquim Chissano wa
Msumbiji. Kwa miaka yote hiyo, Chuo cha Diplomasia kimejikita kuwaandaa
wanadiplomasia, wanastratejia na wabobezi wengi wa masuala ya Uhusiano wa
Kimataifa.
Chuo
kilitumika kuwaandaa wapigania uhuru wa nchi ya Msumbiji na baadae kilipanua
huduma zake na kutumika kuwaandaa pia wapigania uhuru wa nchi za Angola,
Zimbabwe, Namibia n.k.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), ambaye pia alikua mgeni rasmi wa Mahafali ya 22 ya
Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam, akifungua rasmi Mahafali hayo yaliyofanyika
katika viwanja vya Chuo hicho Kurasini Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika MasharikiDkt. Faraji
Mnyepe akifuatiwa na Kaimu
Mkurugenzi wa Chuo, Dkt. Jeremia Ponera.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), (katikati) akiwa katika picha ya ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika MasharikiDkt. Faraji Mnyepe na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo, Dkt. Jeremia pamoja na wanafunzi walifaulu vizuri masomo yao
|
Mgeni
Rasmi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Faraji
Mnyepe wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Mahafali ya 22 ya chuo cha
Diplomasia. Wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Chuo, Dkt.
Jeremia Ponera
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb), ambaye pia alikua mgeni rasmi wa Mahafali ya 22 ya
Chuo cha Diplomasia, Dar es Salaam, akitoa hutuba yake wakati wa mhafali yaliyofanyika
katika viwanja vya Chuo hicho Kurasini Jijini Dar es Salaam
|
Baadhi
ya wanafunzi wakisubiri kutunikiwa
|
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji
Mnyepe akisoma hotuba yake kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi
|
Kaimu Mkurugenzi wa Chuo, Dkt. Jeremia Ponera
akimkaribisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe ili amkaribishe mgeni rasmi kufungua mahafali ya
22 ya chuo
|
Baadhi ya wahadhiri wa Chuo cha Diplomasia wakiwa wamesimama huku wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza
kwa mahafali
|
Baadhi ya Mabalozi na viongozi waandamizi wa Serikali
wakiwa wanaimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa Mahafali ya 22 ya chuo cha
Diplomasia Jijini Dar es Salaam
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb), akimkabidhi zawadi mmoja kati ya wanafunzi
walifaulu vizuri masomo yake |
Tuesday, January 14, 2020
NAIBU WAZIRI DKT NDUMBARO AFANYA MAZUNGUMZO NA MWAKILISHI MKAZI WA ICRC
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi (Head of Regional Delegation) wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross – ICRC) katika Nchi za Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois.
Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam,ambapo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) amesema kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatambua na kuthamini mchango wa ICRC katika utoaji wa huduma na misaada ya kibinadamu hapa nchini hasa katika kambi za wakimbizi zilizopo hapa Nchini.
Amesisitiza kuwa Tanzania ikiwa ni mwanachama hai wa ICRC itaendelea kutimiza wajibu wake wa Kitaifa na Kimataifa na kwa kuzingatia Sheria za kimataifa zilizopo chini ya ICRC,sheria za Tanzania na mkataba wa uenyeji (Head Quarter Agreement) kati ya Tanzania na ICRC uliosainiwa mwaka 2001.
Kwa upande wake Bw. Dubois ameishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuishirikisha ICRC katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali hususani ile inayohusu utoaji wa misaada ya kibinadamu (Humanitarian assistance) kwa kushirikiana na Chama cha Msalaba Mwekundu – Tanzania (Tanzania Red Cross Society – TRCS).
Ameongeza kuwa ICRC itaendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wadau wengine katika utoaji wa huduma kwa wakimbizi walioko hapa nchini,wafungwa/mahabusu waliopo magerezani,mafunzo kwa vyombo vya ulinzi na usalama hususani wakati wa ulinzi wa amani (Training on International Humanitarian Law during peace keeping mission).
Bw. Dubois ameambatana na Bi. Andrea Heath mwakilishi Mkaazi wa ICRC – Tanzania.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi (Head of Regional Delegation) wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross – ICRC) katika Nchi za Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akimsikiliza Mwakilishi Mkazi (Head of Regional Delegation) wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross – ICRC) katika Nchi za Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois. |
Mwakilishi Mkazi (Head of Regional Delegation) wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross – ICRC) katika Nchi za Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) |
Mwakilishi Mkazi (Head of Regional Delegation) wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross – ICRC) katika Nchi za Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois akimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) Hayupo pichani. Pembeni yake anayeandika ni Bi. Andrea Heath mwakilishi Mkaazi wa ICRC – Tanzania |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi (Head of Regional Delegation) wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (International Committee of the Red Cross – ICRC) katika Nchi za Tanzania,Kenya na Djibouti Bw. Olivier Dubois. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam |
Thursday, January 9, 2020
SERIKALI YAWATAKA MABALOZI KUZINGATIA SHERIA, TARATIBU ZA NCHI
Tanzania
imewataka Mabalozi, Makaimu Mabalozi na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa
kuzingatia sheria za nchi pamoja na mikataba ya kimataifa ili kuhakikisha kuwa
wanatekeleza majukumu yao nchini kwa ufanisi na ufasaha.
Akiongea katika mkutano na Mabalozi, Makaimu
Mabalozi pamoja na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) amesema
kuwa mahusiano ya Tanzania na nchi nyingine yanajengwa katika misingi ya
mkataba wa Viena, Mkataba wa umoja wa mataifa na sheria mbalimbali, hivyo ni
vizuri mabalozi kuzingatia taratibu hizo.
"Sisi kama tumesisitiza kuwa ni vyema mabalozi
na wawakilishi wa nchi zao wakafuata taratibu, mila pamoja na desturi zilizopo
katika mikataba hiyo ili kuhakikisha shughuli zao ndani ya Tanzania zinaendana
na kufuatana na mkataba wa Viena, mkataba wa umoja wa mataifa lakini pia kunga,
mila na desturi za kibalozi," Amesema Prof. Kabudi.
Aidha, Waziri Kabudi aliongeza kuwa Tanzania
kupitia mkutano huo imeanza ukurasa mpya wa mahusiano na uendeshaji wa shughuli
za Serikali na balozi pamoja na mashirika ya kimataifa yaliyopo Tanzania.
"………tunepata nguvu mpya baada ya mabalozi wote
kueleza kuridhika kwao kwa hali ya juu sana na hatua ambazo Serikali ya
Tanzania imechukua kupambana na rushwa, kupambana na ubadhirifu wa mali za
umma, hatua ambazo Tanzania imechukua katika kuimarisha makusanyo ya kodi
lakini pia kusimamia matumizi ya fedha za ndani pamoja na zile zinazotolewa na
nchi mbalimbali katika maendeleo ya Tanzania," Amesema Prof. Kabudi.
Katika mkutano huo, Waziri Kabudi amewahamasisha
mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini kuhusu kuhamia Makao
Makuu ya Nchi Dodoma kwa kuwaeleza maendeleo yaliyofikiwa kuhusu ujenzi wa
miundombinu mbalimbali muhimu na kwamba wakati umefika wa kuharakisha kuhamia
Dodoma kwa wakati muafaka kwa kuwa maendeleo yaliyofikiwa nayatoa fursa ya kuwawezesha
wao kuhamia jijini Dodoma.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi hao hapa
Nchini ambae pia ni Balozi wa Comoro Dkt. Ahamada Mohamed ameipongeza Tanzania
kwa kuitisha mkutano huo mapema ikiwa ni siku tisa tu tangu kuanza kwa mwaka
mpya wa 2020 kwa nia ya kubadilishana mawazo na kusikiliza changamoto za
mabalozi na wakuu wa mashirika ya kimataifa pia kuwaelezea hatua za utekelezaji
za masuala ya maendeleo chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli jambo
linalowapa fursa mabalozi hao kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi hapa nchini.
Nae balozi wa Kenya hapa Nchini Mhe. Dan Kazungu
ambaye pia Kiongozi wa Mabalozi wa Bara la Afrika amesema wao kama mabalozi
hawawezi kujua mipango, vipaumbele na changamoto za serikali bila ya kuelezwa
na kutaka mikutano ya namna hiyo kufanyika mara kwa mara jambo ambalo linatoa
uelewa na muelekeo wa utendaji kazi wa serikali
na hivyo kusaidia kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia kwa kutambua
fursa na changamoto zilizopo.
Awali akiwakaribisha mabalozi katika mkutano huo,
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt.
Faraji Mnyepe, aliwataka mabalozi kuhakikisha kuwa wanazingatia taratibu na
kanuni za nchi ili kuhakikisha shughuli zao ndani ya Tanzania zinaendana na
kufuatana na mkataba wa Umoja wa Mataifa.
"Nawasihi sana tufanye kazi kwa kuzingatia
taratibu za nchi pamoja na sheria na mikataba kwa manufaa ya nchi yetu
(Tanzania) na nchi zenu ili tuweze kuendelea kuimarisha uhusiano wa
kidiplomasia baina yetu kwa maendeleo endelevu" Amesema Dkt. Mnyepe
Mkutano huo umehudhuriwa pia na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro,Katibu Mkuu
Dkt Faraji Mnyepe na Mkuu wa Itifaki Balozi, Kanali Wilbert Ibuge, mabalozi 28,
Makaimu Mabalozi 12 na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa 10.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki, Dkt. Faraji Mnyepe akiongea na mabalozi, (hawapo pichani) wakati wa mkutano uliofanyika jijini Dar es Salaam
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiongea na mabalozi, manaibu
mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa katika mkutano uliofanyika
leo jijini Dar es Salaam
Baadhi ya mabalozi wakifuaatilia mkutano baina yao na Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) leo
jijini Dar es Salaam
|
Subscribe to:
Posts (Atom)