Wednesday, July 9, 2014

Waziri Membe afungua rasmi mafunzo ya Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na baadhi ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kuwasili Chuoni hapo kwa ajili ya kufungua rasmi mafunzo yatakayotolewa na Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki iliyo chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa Wanafunzi 52 kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.  Idadi ya Wanafunzi hao kwenye mabano  na nchi wanazotokea  ni Kenya (10), Uganda (10), Burundi (5), Rwanda (5) na Tanzania (22).
Mhe. Membe akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili ukumbini kwa ajili ya kufungua rasmi mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki kwa wanafunzi kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Taasisi ya Uongozi ya Afrika Mashariki, Prof. Rwekaza Mukandala akimkaribisha Waziri Membe kufungua rasmi mafunzo hayo. Wengine katika picha ni Dkt. Benson Bana (wa kwanza kulia), Mhadhiri na Mratibu wa Mafunzo hayo kwa mwaka 2014 na Prof. Betram Mapunda (wa kwanza kushoto).
Sehemu ya Wanafunzi wakimsikiliza Prof. Mukandala (hayupo pichani)
Waziri Membe akitoa hotuba ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Sehemu nyingine ya Wanafunzi wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani) alipowahutubia. 
Mhe. Membe akisisitiza jambo wakati wa hotuba yake huku Prof. Mukandala akimsikiliza.
Mmoja wa wanafunzi hao kutoka Uganda akimuuliza swali Mhe. Membe.
Mmoja wa Wanafunzi hao kutoka Kenya nae akiuliza swali kwa Mhe. Membe.
Mhe. Membe akijibu maswali ya wanafunzi.
Dkt. Godius Kahyarara, Mkuu wa Shule ya Sayansi ya Jamaii katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akitoa neno la shukrani mara baada ya hotuba ya Mhe. Membe ya ufunguzi.
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na kundi la wanafunzi kutoka Kenya.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoa Uganda.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Rwanda.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi kutoka Burundi.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Tanzania.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Wahadhiri waliohudhiria ufunguzi huo.
Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na waliowahi kuwa wanafunzi (alumni) wa Taasisi hiyo miaka ya nyuma akiwemo Msaidizi wake Bw. Thobias Makoba (mwenye tai nyekundu waliosimama)
Mhe. Membe akizungumza na Vyombo vya Habari (Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali)

___________________________________________________________________________


SPEECH BY HONORABLE BERNARD K. MEMBE (MP) MINISTER FOR FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION ON THE OCCASION OF THE OFFICIAL OPENING OF THE 2014
 EAST AFRICAN UONGOZI SCHOOL AT THE COUNCIL CHAMBER,
UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM, 8TH JULY 2014

Professor Rwekaza Mukandala, Vice-Chancellor of the University of Dar es Salaam and Director, East African Uongozi Institute,

University of Dar es Salaam Leadership,

Uongozi School 2014 Participants,

Members of the Press,

Friends of East Africa,

Invited Guests;


Ladies and Gentlemen.


Let me begin by expressing my sincere gratitude to the organizers of this event—the East African Uongozi Institute (EAFUI)—for availing to me this honour to officiate the 2014 Uongozi School. I am aware that EAFUI has been organizing similar Uongozi School sessions since its inception in 1998. I am also made to understand that this year’s Uongozi School is unique as for the first time the number has increased from three to five Universities in East Africa. This is a commendable step taking aboard the reality of the expanding membership of the East African Community which has since 2006 include Burundi and Rwanda.
As we witness this opening, my congratulations goes to the leadership of the East African Uongozi Institute for conceiving the idea of the Uongozi School, implementing and sustaining it for more than a decade. Those of us who deal with inter-state relationships understand the dynamics and challenges involved. It is through hard work and commitment that this initiative could be sustained over the years. The work that EAFUI does is highly complementary to the efforts that the EAC partner states are making to deepen and strengthening the cooperation. When the young scholars of East Africa are brought together in a programme like this they start to appreciate that there is a lot that unites them than what can divide them. They begin to cultivate long term personal relationships and understandings that are critical for the sustainability of the Community. Programmes such as Uongozi School have sown seeds to a stronger and successful regional bloc as it nurtures future regional leaders. We in the government are proud of this initiative.

Ladies and Gentlemen,

I therefore congratulate all participants of the 2014 Uongozi School for securing a chance to this prestigious programme. I am aware that the selection process is very stringent and that only the best students can go through. I urge you to keep up the hard work and I believe through this programme you will not only learn around the topic at discussion, but also be inspired to lead in any sector you will find yourselves in. You are not only the future of EAC, but the future of Africa. I also join the organizers to welcome to Tanzania those participants who have come from outside Tanzania. I am sure you will find Dar es Salaam and other places that you will visit in Tanzania to be enjoyable.

Ladies and Gentlemen,

Through this event, I must say EAC is one of the most promising and success story in the continent, having elevated itself to the Common Market stage of the integration process.  As we all know, there is no other Regional Economic grouping in the continent that has reached that stage.  That said, one point must be made clear; that member states are free to have bilateral projects and programs, and they are free to do so without involving other partner states.  However, for those projects that fall directly under the East African Community, they must without exception involve all member states of the Community.

Ladies and Gentlemen,

The theme of the 2014 Uongozi School “African States, Competing Identities and Democratization” could not come at a more promising time.  As coined, this theme goes beyond East Africa and it touches our continent at large. Politics of identity or politicization of ethnic identities seem to be at the helm in many African countries. This is not to say it is a new acceptable way of life in the continent. Exclusion of people from effective control of state power and economic resources has been a source of many of the post-independence violent conflicts in Africa. One of the undesirable consequences of the third wave democratization that re-introduced multiparty politics was resorting to cheap ethnic politics. Ethnic entrepreneurs mobilized people emphasizing sub-nationalities and aspiring to maximize their corporate political, economic and social interests. A state ceases to be the arbiter of different group interests and becomes the centre for group contestations. Ethnic politics is shortsighted and counterproductive as voters are only concerned with enabling their members or coalition to control the state.  As scholars, I would encourage participants to this year’s programme not to shy away from discussion openly about this topic. Your research papers will form a part in solution pursuit and influencing political actors on this topic. This continent is on the verge of transformation and we are all to play a part.

Ladies and Gentlemen,

Some political leaders convince ethnic groups to believe that they rule the country on their behalf. The president is seen as an ethnic ruler rather than a leader for all citizen. People believe that if one of their own holds a high post, it is held in trust for the benefit of their ethnic community. Some political parties promote ethnic politics and regard the introduction of multiparty democracy as a way of decentralizing the state in favour of ethno-nationalism. Rather than ameliorating the differences and mediating them, this kind of politics is amenable to conflicts as electoral outcomes are highly zero-sum and thus generators of dissatisfaction.

To the Participants,

I have looked at programme and saw close to 20 presentations and panel discussions. I am happy that many of the issues pertinent to competing identities and democratization in Africa will be adequately treated. I strongly urge all of you to effectively use the six weeks of your training to turn all the challenges of multiparty democracy into opportunities for African growth. 

Ladies and Gentlemen,
Invited guests,
My duty today was simply to officially open the 2014 Uongozi School and not to make a lecture. I want to reiterate my sincere thanks to the organizers for inviting me to grace this occasion. To the participants I wish you all the best in your deliberations in this year’s Uongozi School.

With these few remarks, may I now officially declare that the 2014 Uongozi School is open.


THANK YOU FOR YOUR KIND ATTENTION

LONG LIVE UONGOZI SCHOOL




Tuesday, July 8, 2014

Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia wapata semina Wizarani

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akitoa mada kuhusu Sera ya Mambo ya Nje na Uhusiano kati ya nchi na nchi hususan uhusiano wa nchi za Asia na Tanzania katika semina kwa  Wanafunzi wa Chuo cha Diplomasia (CFR) wanaofanya mafunzo kwa vitendo  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. 
Baadhi ya Wanafunzi hao wakimsikiliza Balozi Mbelwa (hayupo pichani)
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Batholomeo Jungu akifuatilia semina hiyo
Semina ikiendelea

Viongozi mbalimbali watembelea banda la Mambo ya Nje sabasaba

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova  akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Banda la Maonesho la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika Viwanja vya Sabasaba
Mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Janeth Widambe akipata maelezo alipotembelea Banda la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba
Wananchi wakiwa wamefurika katika Banda la Maonesho la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watumishi wa Mambo ya Nje na Taasisi zake.

Picha na Reginald Philip

Sunday, July 6, 2014

Mwanamfalme Akishino wa Japan amaliza ziara yake rasmi nchini

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki (Mb.) akizungumza na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino kabla ya kuondoka. Prince Akishino amemaliza ziara yake aliyo ifanya hapa nchini kuanzia tarehe 3 hadi 6 Julai 2014
Naibu waziri Angela Kairuki akimsindikiza Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino tayari kwa kuanza safari, kushoto pichani Afisa Mambo ya Nje Ramadhani Ditopile
Naibu Waziri Angela Kairuki akiagana na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino kabla ya kuanza safari yake katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es salaam.

Picha na Reginald Philip

Saturday, July 5, 2014

Rais Kikwete Atembelea Banda la Mambo ya Nje, Sabasaba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya Sabasaba
Rais Dkt. Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje
Rais Kikwete (Mwenye Koti la Blue) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake.
Mtumishi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mbwana Msingwa akiweka saini katika kitabu cha wageni alipokuja na familia yake kwenye banda la Mambo ya nje lililopo kwenye viwanja vya sabasaba
Mpiga Picha wa Rais Muhidin Issa Michuzi (Ankal) akisalimiana na Afisa Mawasiliano Ally kondo, alitembelea Banda la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba

Picha na Reginald Philip

Waziri Membe ahudhuria msiba wa Mzazi wa Felista Rugambwa

Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa heshima za mwisho kwenye Kanisa la Anlikana la Mt. Joseph, kumuaga Mzee Rugambwa ambaye ni baba wa mtumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Idara ya Ulaya na Marekani Bi. Felista Rugambwa leo Julai 5, 2014.  
Mhe. Bernard K. Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara John Haule na Mkurugenzi wa Idaho ya Ulaya na Marekani Balozi Joseph Sokoine, wakifuatilia misa iliyofanyika kwenye kanisa la Mt. Josefu, Dar es salaam leo tarehe 5 Julai 2014. 

Felista Rugambwa (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na ndugu zake wakifuatilia misa.
Familia ya Marehemu Mzee Rugambwa wakitoa shukrani (pichani juu)                        

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akitoa shukrani kwa niaba ya Wizara (pichani chini)


Friday, July 4, 2014

Dkt. Shein akutana na Mwana Mfalme wa Japan

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Ali Mohamed Shein (kulia) akisalimiana na Mwana Mfalme wa Japani Prince Akishino alipowasili Ikulu Mjini Zanzibar leo akiambatana na Mkewe Princess Akishino na baadae kufanya Mzazungumzo.
Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein (kushushoto) akizungumza na Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Ali Mohamed Shein (katikati) akiwapa maelezo Mwana Mfalme wa Japani Prince Akishino na Mkewe juu ya moja ya mti uliopo mbele yao
Picha ya pamoja


Picha na Reginald Philip

Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa UNFPA nchini

Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akisalimiana na Mwakilishi mpya wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa unaoshughulikia Idadi ya Watu (UNFPA) hapa nchini, Dkt. Natalia Kanem alipofika Ofisini kwake kwa ajili ya kuwasilisha Hati za Utambulisho.
Mhe. Membe akipokea Hati za Utambulisho za Dkt. Kanem.
Mhe. Membe akizungumza na Dkt. Natalia kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu idadi ya watu na maendeleo. Kwa upande wake Dkt. Kanem aliahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika masuala ya idadi ya watu ambapo pia aliipongeza Tanzania hususan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwa mstari wa mbele katika kutetea Afya ya Mama na Mtoto duniani. 
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Membe na Dkt. Kanem. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa pili kutoka kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi Mindi Kasiga (wa pili kutoka kulia), Afisa Mambo ya Nje, Bibi Samira Diria (wa kwanza kulia) na Mtaalam wa Mawasiliano kutoka UNFPA, Bi. Sawiche Wamunza.

Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali

Waziri Membe apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa IFAD nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Chakula na Kilimo (IFAD) hapa nchini, Bw. Francisco Javier Pichou Angulo.  Hafla hiyo fupi ilifanyika Ofisini kwa Mhe. Membe tarehe 04 Julai, 2014.
Mhe. Membe akimsikiliza Bw. Angulo alipozungumza nae baada ya kupokea hati zake za Utambulisho. Miongoni mwa masuala aliyoahidi Mwakilishi huyo ni pamoja na kuendelea kushirikiana kwa karibu na Serikali ya Tanzania katika Sekta ya Kilimo na Chakula.
Mhe. Membe nae akizungumza huku akisikilizwa na Mwakilishi huyo pamoja na Afisa aliyefuatana nae pamoja Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kushoto)
Picha ya pamoja.


Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali