Friday, February 22, 2019

Tanzania na Ufaransa ushirikiano wazidi kuimarika

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Ufaransa ushirikiano wazidi kuimarika

Tanzania na Ufaransa  zimeahidi kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo; kuongeza uwekezaji na biashara; na kutafuta ufumbuzi wa migogoro inayozikabili nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu, Ukanda wa Bahari ya Hindi na changamoto nyingine za kiusalama katika maeneo hayo.

Ahadi hiyo ilitolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi hizo jijini Paris leo walipokutana kwa ajili ya mazungumzo. Mhe. Dkt. Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki yupo nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi siku siku mbili 21 na 22 Februari 2019 kufuatia mwaliko wa Waziri wa Ulaya na Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean- Yves Le Drian ambaye ameahidi pia kufanya ziara ya kikazi nchini Tanzania hivi karibuni.
Kabla ya mazungumzo hayo, Mheshimiwa Balozi Mahiga alikutana na kufanya mazungumzo na kundi la Maseneta wa Ufaransa ambao ni marafiki wa Tanzania wakiongozwa na Seneta Ronan Dantec ambaye ni Mwenyekiti wa Maseneta hao. Maseneta hao walipendekeza kuanzishwa kwa ushirikiano dada kati ya jiji la Paris na Dodoma. Ushirikiano huo ujikite zaidi katika matumizi bora ya ardhi, mipango miji na kutekeleza miradi mbalimbali ya kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Vilevile, Maseneta hao wameelezea dhamira  yao ya kutaka kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuibua vipaji vya mchezo wa mpira wa miguu katika shule mbalimbali nchini.

Wakati huo huo, Mhe. Mahiga alifanya mazungumzo na Bibi Marie Audouard, Naibu Mshauri wa Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa anayeshughulikia masuala ya Afrika. Katika mazungumzo yao, Bibi Audouard aliainisha maeneo ya kipaumbele ya Mhe. Rais Emmanuel Macron katika mahusiano yake na nchi za Afrika. Vipaumbele hivyo ni pamoja na kuimarisha zaidi mahusiano na nchi zinazoongea lugha ya kiingereza na kireno; kuendelea kushirikiana katika usuluhishi wa migogoro ya kikanda na kimataifa; kuhamasisha sekta binafsi ya Ufaransa kwenda kuwekeza Afrika; na  kubadilishana uzoefu katika nyanja za utamaduni hasa kwa vijana.
Viongozi wengine aliofanya nao mazungumzo Mhe. Waziri ni pamoja na Bibi Audrey Azoulay, Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO; na Bw. Bertrand Walckenaer, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Ufaransa (AFD).
Katika mazungumzo na Mkurugenzi wa UNESCO, Waziri Mahiga alilishukuru Shirika hilo kwa kuwa mshirika wa Tanzania kwa miaka mingi kwenye masuala ya elimu, sayansi na utamaduni na kuahidi kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana katika masuala mbalimbali yanayohusu elimu, sayansi na utamaduni.
Kwa upande wa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa AFD, Mkurugenzi huyo alieleza kuwa, kutokana na ushirikiano mzuri uliopo wameongeza mara mbili kiwango cha fedha za maendeleo nchini Tanzania ambazo zitatumika kufadhili miradi katika sekta za uchukuzi, nishati, maji safi na taka, kilimo, afya na mabadiliko ya tabianchi.
Mheshimiwa Waziri anahitimisha ziara yake leo kwa kukutana na Jumuiya ya Wawekezaji na wafanyabiashara wa Ufaransa (MEDEF) na Bi. Luise Mushikiwabo, Mtendaji Mkuu wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (IOF).

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
22 Februari 2019

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akipokelewa na mwenyeji wake, Waziri wa Ulaya na Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean- Yves Le Drian jijini Paris. Dkt. Mahiga yupo nchini Ufaransa kwa ziara ya siku mbili tarehe 21 na 22 Februari 2019.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kushoto) akiwa katika mazungumzo na mwenyeji wake, Waziri wa Ulaya na Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mhe. Jean- Yves Le Drian




Thursday, February 21, 2019

Tanzania na Umoja wa Ulaya waazimia kuimarisha Uhusiano

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Umoja wa Ulaya waazimia kuimarisha Uhusiano

Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU) wamekubaliana kuimarisha uhusiano na ushirikiano kwa kufanya majadiliano ya mara kwa mara yatakayojengwa katika misingi ya kuaminiana, usawa, uwazi na kuheshimiana ili kujenga uelewa wa pamoja katika maeneo mbali mbali yenye changamoto kwa manufaa  mapana ya watu wa pande zote mbili.

Makubaliano hayo yamefikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb) na Mkurugenzi wa Idara ya Pembe ya Afrika na Afrika Mashariki, Huduma za Nje katika Umoja wa Ulaya, Bw. Patrick Simonnet wakati wa ziara yake iliyofanyika nchini kuanzia tarehe 17 hadi 20 Februari 2019.

Katika mazungumzo hayo, Mhe. Waziri aliushukuru Umoja wa Ulaya kwa misaada ambayo umekuwa ukiipatia Tanzania kwa ajili ya utekelezji wa miradi mbalimbali ya maendelea katika sekta za kilimo, nishati na ujenzi wa miundombinu ya barabara na viwanja vya ndege. “Umoja wa Ulaya ni mbia muhimu wa Tanzania katika shuguli za maendeleo tokea mahusiano rasmi ya kidiplomasia yalipoanzishwa mwaka 1975; baada ya kusainiwa kwa mkataba wa kwanza wa Rome baina ya kundi la nchi za Afrika, Caribbean na Pasifiki (ACP) na nchi wanachaama wa Umoja wa Ulaya”; alisema Mhe. Mahiga.

Viongozi hao walihitimisha mazungumzo yao kwa kuazimia kuendelea kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya pande mbili hizi katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na biashara, uwekezaji, ushirikiano wa maendeleo na usalama wa majini, hususan katika pwani ya Bahari ya Hindi. 
Aidha, walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kimataiafa ikiwa ni pamoja na kusaidia juhudi za kudumisha na kuimarisha hali ya amani, usalama na utulivu katika eneo la Maziwa Makuu.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
21 Februari 2019


Tuesday, February 19, 2019

Wanadiaspora wa Saudia wapigwa msasa Uhamiaji mtandao

 Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah nchini Saudi Arabia “Tanzania Welfare Society” hivi karibuni ilifanya Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza.

Wanajumuiya walipata fursa ya kujadiliana mambo mbalimbali yakiwemo uwekezaji na uchumi, ajira nchini Saudi Arabia, masomo nchini Saudi Arabia. Aidha, wanajumuiya walipata maelezo kuhusu matumizi ya mfumo mpya uhamiaji mtandao “e-immigration” ambapo walifahamishwa na kutakiwa kuanza rasmi kuomba pasi mpya za kusafiria za ki-electronic, hati za dharura za kusafiria za ki-electronic.  Pia wanajumuiya walitakiwa kuwahamasisha wageni kutembelea Tanzania kwa shughuli za utalii, uwekezaji na biashara, na pia sasa wanaweza kuomba viza za kuingia Tanzania kwa njia ya mtandao “e-visa”. 

Wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia maendeleo ya Tanzania

Kutoka Kushoto  Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah, Bw. Salim Ali Shatri, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akihutubia, kujibu maswali na kutoa ufafanuzi, mwisho kulia ni Mweka Hazina wa Jumuiya ya Watanzania ya Jeddah, Bw. Abdallah Faris.
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakiwa mkutanoni.
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident Jeddah.

Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakipata chakula
Wanajumuiya wakipata chakula

Friday, February 15, 2019

Re-advertisement for the post of Director of Internal Oversight



PRESS RELEASE

Re-advertisement for the post of Director of Internal Oversight 

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received a note from the Secretariat of the Organization for the Prohibition of Chemical Weapons (OPCW) expressing that, it has extended closing date for the post of Director, Office of Internal Oversight, D-2 from 6th February 2019 to 20th February 2019.

Interested candidates are advised to make applications online through the Organization’s website www.opcw.org

Female applicants are highly encouraged.



Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
15th February 2019.

Naibu Waziri atembelea Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar alipofanya ziara kwenye Ofisi hiyo ikiwa ni miongoni mwa ziara zake za kuzitembelea Taasisi za Wizara zilizopo nje ya Dodoma. Katika mkutano wake na Watumishi hao, Mhe. Naibu Waziri aliwataka  kuanzisha mazungumzo ya pamoja kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika vikao vitakavyofanyika kwa zamu baina ya Zanzibar na Dodoma ili kukuza ufanisi wa Wizara kwa ujumla. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Mohammed H. Hamza. Ziara hiyo imefanyika tarehe 15 Februari 2019.
Balozi Hamza akizungumza na kumkaribisha Mhe. Dkt. Ndumbaro kwenye Ofisi za Mambo ya Nje Zanzibar ambapo pia alimweleza mafanikio ya Ofisi hiyo yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu ya kuratibu masuala ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar.
Bw. Suleiman M. Mohammed, ambaye ni Mhasibu kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri
Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Bw. Iddi Seif Bakari, Afisa Mambo ya Nje alipokuwa akieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi kwenye Ofisi hiyo
Bi. Asia Hamdani, Afisa Tawala kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar nae akizungumza kwenye mkutano kati ya Watumishi wa Ofisi hiyo na Mhe. Naibu Waziri
Mtumishi mwingine ambaye ni Afisa Mambo ya Nje kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bw. Salim R. Haji akichangia jambao wakati wa mkutano kati ya Watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar na Naibu Waziri.

Tanzania na Uganda zajadili Kuboresha Sekta ya Uchukuzi


Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz P. Mlima akiwa katika mazungumzo  na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda Mheshimiwa Mhandisi Monica Ntega  mjini Kampala ambapo walizungumzia changamoto na fursa zilizopo kwa nchi mbili kwenye sekta ya uchukuzi, reli na bandari na ushoroba wa kati. Mazungumzo hayo pia yalihidhuriwa na Waziri wa Nchi wa Ujenzi wa Uganda Jenarali Edward Katumba Wamala.

Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz P. Mlima akimkabidhi zawadi ya kahawa ya Tanzania Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mheshimiwa Mhandisi Monica Ntega baada ya mazungumzo yao  mjini Kampala

 Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe. Dkt Aziz P. Mlima akiwa na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mheshimiwa Mhandisi Monica Ntega  mjini Kampala na Waziri wa Nchi wa Ujenzi wa Uganda Jenarali Edward Katumba Wamala.
Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Mhe.  Dkt Aziz P. Mlima akiagana na  Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi wa Uganda, Mheshimiwa Mhandisi Monica Ntega baada ya mazungumzo yao  mjini Kampala

Thursday, February 14, 2019

Tanzania and Kazakhstan establish diplomatic relations

The Permanent Representative of the United Republic of Tanzania to the United Nations, H.E Ambassador Modest J. Mero (R) and Permanent Representative of Republic of Kazakhstan to the United Nations, H.E  Ambassador Kairat Umarov signing a communique to establish diplomatic relations between their Nations. The signing ceremonies took place in New York on 13th
  February 2019.
Ambassador Mero exchanges the signed communique with his counterpart, Ambassador Umarov.


Ambassador Mero and Ambassador Umarov posing for a photo after signing a communique to establish diplomatic relations between the two countries.

Wednesday, February 13, 2019

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Namibia nchini.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia Mhe. Balozi Theresia Samaria.  Mazungumzo hayo  ambayo yalijikita kwenye masuala ya kuimarsha ushirikiano kati ya nchi hizi mbili,  yamefanyika katika Ofisi ndogo ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam tarehe 13 Februari 2019.
Mazungumzo yakiendelea.







ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango  Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) kwa pamoja wamefanya ziara kwenye kijiji cha Jasini na Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja Mpakani cha Horohoro kilichopo mpakani mwa Tanzania na Kenya Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga. Pamoja na Mambo mengine Naibu Mawaziri hao waliweza kujionea changamoto mbalimbali ikiwamo ukusanyaji wa mapato kituoni hapo, pamoja na kuzungumza na wanakijiji cha Jasini na Watendaji wa Kituo hicho.   
Wadau walioshiriki ziara za Naibu mawaziri hao wakisikiliza  wakati Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) akizungumza
Sehemu nyingine ya wadau wakimsikiliza  Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani)
Mkutano ukiendelea
Wananchi wakipata huduma kwenye kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja
Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Kijaji wakimsikiliza Bw. Bilali Juma, Afisa Mkemia wa kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Horohoro
Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na wadau mbalimbali
Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja cha Horohoro kilihopo Mpakani mwa Tanzania na Kenya kama kinavyoonekana pichani 

Dkt. Ndumbaro akisaini kitabu cha wageni cha kijiji cha Jasini kilichopo wilaya ya Mkinga, Mkoani Tanga, kabla ya kuanza ziara kwenye kijiji hicho

Naibu Mawaziri pamoja na wadau mbalimbali wakiwa wamesimama kwenye moja ya jiwe ambalo linaonyesha Mpaka wa Tanzania na Kenya.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt.  Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya.  Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiendelea na ziara na kujionea alama za mipaka zilizopo mpakani hapo
Mhe. Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye moja ya alama za mpaka
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara yao kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Horohoro
Mhe. Dkt. Kijaji akitizama kitambulisho cha mjasiriamali mdogo huku Dkt. Ndumbaro akishuhudia tukio hilo. Mjasiriamali huyo aliwavuti Naibu Mawaziri hao kwa mwitikio wake chanya katika kuhakikisha kila mjasiriamali nchini anapata kitambulisho cha kufanyia biashara
Mmoja wa wanakijiji akielezea changamoto wanazokabiliana nazo kijijini hapo ikiwamo upatikanaji wa elimu kwa watoto wao ambao wanalazimika kwenda kusoma Kenya na jioni kurejea Tanzania.
Wanakijiji wakiwasikiliza kwa makini Naibu Mawaziri hawapo pichani


Naibu Mawaziri hao wakizungumza na baadhi ya wananchi wa Jasini mara baada ya kumaliza ziara kijijini hapo
Waandishi wa habari wakiwa kazini
Waheshimiwa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Mohamed Ibrahim anayesoma Darasa la nne Shule ya Vumba Kuu iliyopo Kenya. Mohamed alikuwa amerudi nyumbani kupata chakula  wakati wa mapumziko mafupi kabla ya kurudi darasani.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO

Watendaji wa Kituo Cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha Horohoro kilichopo mkoani Tanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wametakiwa kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa ya kukusanya mapato kwenye kituo hicho yanafikiwa.

Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) walipotembelea kituo hicho tarehe 10 Februari 2019.

Dkt. Ndumbaro alishangazwa na mwenendo wa ukusanyaji wa mapato wa kituo hicho ambapo takwimu zimekuwa zikipungua badala ya kuongezeka kila mwaka. ‘Kwa miaka mitatu mfululizo takwimu za ukusanyaji wa mapato ya kodi katika Kituo hiki zimekuwa zikishuka badala ya kupanda, jambo ambalo si zuri kiuchumi na linakwenda kinyume kabisa na malengo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli’; Dkt. Ndumbaro alimwambia Meneja wa TRA kituoni hapo.

Kwa mujibu wa takwimu hizo mwaka wa fedha 2017/2018, makusanyo ya kodi kwenye kituo hicho ni asilimia 81 ya malengo na mwaka wa Fedha 2018/2019 inatarajiwa makusanyo yatafikia asilimia 76 ya malengo yaliyowekwa.

Mhe. Naibu Waziri aliwataka watendaji hao kuwa wabunifu kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanafikiwa bila kumuonea mtu ikiwemo ubunifu wa kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho. Changamoto hizo ni pamoja na ukosefu wa maji ambapo yananunuliwa kwa gharama ya Shilingi milioni sita kwa mwezi. Naibu Waziri alishangazwa na uamuzi huo wa kutumia fedha nyingi kwa ajili ya maji wakati kuchimba kisima hakiwezi kugharimu zaidi ya milioni 10.

Dkt. Ndumbaro pia hakuridhishwa na ubora wa jengo la kituo hicho na kubainisha kuwa ndio sababu zinazofanya kituo hicho kutozinduliwa rasmi hadi leo.

Kwa upande wake, Dkt. Kijaji alisikitishwa na utendaji usiokuwa na kiwango wa mamlaka zote zilizopo kwenye kituo hicho na kusisitiza kuwa, kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo chini ya himaya yake atachukua hatua zinazostahili. Moja ya maeneo yenye udhaifu katika kituo hicho ni uchukuaji wa takwimu zikiwemo za magari yanayoingia na kutoka ambapo kila mamlaka iliyopo hapo ina takwimu tofauti.

Aidha, Mhe. Kijaji alipiga marufuku kwa wafanyabiashara wa Wilaya ya Mkinga kwenda Wilaya ya Muheza kufuata huduma za kodi zikiwemo za kulipia kodi mbalimbali. Mhe. Naibu Waziri alimuagiza Mkuu wa Wilaya ya Mkinga kuwatangazia wafanyabiashara wa Mkinga marufuku hiyo na kuagiza watumishi wa TRA wa Mkoa kwenda Mkinga kutoa huduma za kikodi angalau mara tatu kwa wiki.

Kuhusu ubora wa jengo hilo, Dkt. Kijaji aliagiza apatiwe nyaraka za jengo hilo ifikapo tarehe 15 Februari 2019 ili aone majukumu ya kila mmoja katika ujenzi wa jengo hilo kwa madhumuni ya kuchukua hatua stahiki.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji walifanya ziara ya pamoja kwenye kituo hicho cha Horohoro kwa lengo la kujionea changamoto ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
13 Februari 2019




Tuesday, February 12, 2019

Job Announcement at the Commonwealth Secretariat

PRESS RELEASE

Job Announcement at the Commonwealth Secretariat
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commonwealth Secretariat inviting qualified Tanzanians to apply for the post of Legal Adviser (Natural Resources) available at the Commonwealth Secretariat.

In line with the Commonwealth’s commitment to gender equality, the Commonwealth Secretariat encourages applications from appropriately qualified women for this post.

Application details can be found on the Secretariat’s website, http://thecommonwealth.org/jobsClosing date for application is Wednesday 20th February, 2019 at 17:00 GMT.

Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
12th February  2019.


Saturday, February 9, 2019

Tanzania na Azerbaijan kuanzisha Ushrikiano wa Kidiplomasia


Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kushoto) akisalimiana na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev jijini New York Marekani. Viingozi hao walikutana kwa ajili ya kusaini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Mataifa yao. 

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Modest J. Mero (kulia) na Mwakilishi wa Kudumu wa Azerbaijan katika Umoja wa Mataifa, Balozi Yashar Aliyev wakiweka saini Makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na Azerbaijan jijini New York, Marekani. Wengine katika picha ni maafisa wa ofisi za Balozi, Bi, Lilian A. Mukasa na Bw. Tofig F. Musayev. 

Balozi Mero na Balozi Aliyev wakiagana baada ya kusaini makubaliano ya kuanzisha ushirikiano wa kidiplomasia baina ya mataifa yao.