Wadau walioshiriki ziara za Naibu mawaziri hao wakisikiliza wakati Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) akizungumza |
Sehemu nyingine ya wadau wakimsikiliza Dkt. Ndumbaro (hayupo pichani) |
Mkutano ukiendelea |
Wananchi wakipata huduma kwenye kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja |
Dkt. Ndumbaro pamoja na Dkt. Kijaji wakimsikiliza Bw. Bilali Juma, Afisa Mkemia wa kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Horohoro |
Dkt. Ndumbaro akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo na wadau mbalimbali |
Kituo cha kutolea huduma kwa pamoja cha Horohoro kilihopo Mpakani mwa Tanzania na Kenya kama kinavyoonekana pichani |
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye Nyumba iliyojengwa mpakani mwa Tanzania na Kenya. Horohoro. Mhe. Ndumbaro akiwa upande wa Kenya na Mhe. Kijaji akiwa upande wa Tanzania |
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji wakiendelea na ziara na kujionea alama za mipaka zilizopo mpakani hapo |
Mhe. Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Dkt. Kijaji wakiwa kwenye moja ya alama za mpaka |
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa ziara yao kwenye kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Horohoro |
Waandishi wa habari wakiwa kazini |
Waheshimiwa Naibu Mawaziri wakimsikiliza Mohamed Ibrahim anayesoma Darasa la nne Shule ya Vumba Kuu iliyopo Kenya. Mohamed alikuwa amerudi nyumbani kupata chakula wakati wa mapumziko mafupi kabla ya kurudi darasani. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
ZIARA YA PAMOJA YA NAIBU
MAWAZIRI WA MAMBO YA NJE NA FEDHA MPAKANI HOROHORO
Watendaji wa Kituo Cha Kutoa Huduma kwa Pamoja cha
Horohoro kilichopo mkoani Tanga kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya wametakiwa
kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa ya kukusanya mapato kwenye kituo hicho
yanafikiwa.
Kauli hiyo ilitolewa kwa pamoja na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb)
na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb)
walipotembelea kituo hicho tarehe 10 Februari 2019.
Dkt. Ndumbaro alishangazwa na mwenendo wa
ukusanyaji wa mapato wa kituo hicho ambapo takwimu zimekuwa zikipungua badala
ya kuongezeka kila mwaka. ‘Kwa miaka mitatu mfululizo takwimu za ukusanyaji wa
mapato ya kodi katika Kituo hiki zimekuwa zikishuka badala ya kupanda, jambo
ambalo si zuri kiuchumi na linakwenda kinyume kabisa na malengo ya Serikali ya
Awamu ya Tano chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli’; Dkt. Ndumbaro
alimwambia Meneja wa TRA kituoni hapo.
Kwa mujibu wa takwimu hizo mwaka wa fedha
2017/2018, makusanyo ya kodi kwenye kituo hicho ni asilimia 81 ya malengo na
mwaka wa Fedha 2018/2019 inatarajiwa makusanyo yatafikia asilimia 76 ya malengo
yaliyowekwa.
Mhe. Naibu Waziri aliwataka watendaji hao kuwa
wabunifu kuhakikisha kuwa malengo ya Serikali yanafikiwa bila kumuonea mtu
ikiwemo ubunifu wa kutatua changamoto zinazokikabili kituo hicho. Changamoto
hizo ni pamoja na ukosefu wa maji ambapo yananunuliwa kwa gharama ya Shilingi
milioni sita kwa mwezi. Naibu Waziri alishangazwa na uamuzi huo wa kutumia
fedha nyingi kwa ajili ya maji wakati kuchimba kisima hakiwezi kugharimu zaidi
ya milioni 10.
Dkt. Ndumbaro pia hakuridhishwa na ubora wa jengo
la kituo hicho na kubainisha kuwa ndio sababu zinazofanya kituo hicho
kutozinduliwa rasmi hadi leo.
Kwa upande wake, Dkt. Kijaji alisikitishwa na
utendaji usiokuwa na kiwango wa mamlaka zote zilizopo kwenye kituo hicho na
kusisitiza kuwa, kwa kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ipo chini ya himaya
yake atachukua hatua zinazostahili. Moja ya maeneo yenye udhaifu katika kituo
hicho ni uchukuaji wa takwimu zikiwemo za magari yanayoingia na kutoka ambapo
kila mamlaka iliyopo hapo ina takwimu tofauti.
Aidha, Mhe. Kijaji alipiga marufuku kwa
wafanyabiashara wa Wilaya ya Mkinga kwenda Wilaya ya Muheza kufuata huduma za
kodi zikiwemo za kulipia kodi mbalimbali. Mhe. Naibu Waziri alimuagiza Mkuu wa
Wilaya ya Mkinga kuwatangazia wafanyabiashara wa Mkinga marufuku hiyo na
kuagiza watumishi wa TRA wa Mkoa kwenda Mkinga kutoa huduma za kikodi angalau
mara tatu kwa wiki.
Kuhusu ubora wa jengo hilo, Dkt. Kijaji aliagiza
apatiwe nyaraka za jengo hilo ifikapo tarehe 15 Februari 2019 ili aone majukumu
ya kila mmoja katika ujenzi wa jengo hilo kwa madhumuni ya kuchukua hatua
stahiki.
Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Dkt. Kijaji walifanya
ziara ya pamoja kwenye kituo hicho cha Horohoro kwa lengo la kujionea
changamoto ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
13 Februari
2019
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.