Jumuiya ya Watanzania waishio
Jeddah nchini Saudi Arabia “Tanzania Welfare Society” hivi karibuni ilifanya
Mkutano wa pamoja wa wanajumuiya Watanzania na Wanadiaspora. Mkutano huo pia
ulihudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza.
Wanajumuiya walipata fursa ya kujadiliana mambo
mbalimbali yakiwemo uwekezaji na uchumi, ajira nchini Saudi Arabia, masomo
nchini Saudi Arabia. Aidha, wanajumuiya walipata maelezo kuhusu matumizi ya
mfumo mpya uhamiaji mtandao “e-immigration” ambapo walifahamishwa na kutakiwa
kuanza rasmi kuomba pasi mpya za kusafiria za ki-electronic, hati za dharura za
kusafiria za ki-electronic. Pia wanajumuiya walitakiwa kuwahamasisha
wageni kutembelea Tanzania kwa shughuli za utalii, uwekezaji na biashara, na pia
sasa wanaweza kuomba viza za kuingia Tanzania kwa njia ya mtandao
“e-visa”.
Wanajumuiya walisisitizwa kuwa na umoja na uzalendo kwa
Tanzania. Walitakiwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanachangia
maendeleo ya Tanzania
|
Kutoka Kushoto Afisa Utawala wa Konseli Kuu ya Jeddah Ali Mohamed, Makamu wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Jeddah, Bw. Salim Ali Shatri, Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia Mhe. Hemedi Mgaza akihutubia, kujibu maswali na kutoa ufafanuzi, mwisho kulia ni Mweka Hazina wa Jumuiya ya Watanzania ya Jeddah, Bw. Abdallah Faris.
|
Watanzania na Wanadiaspora wa
Jeddah wakiwa mkutanoni. |
|
|
Watanzania na Wanadiaspora wa
Jeddah wakisikiliza hotuba katika hoteli ya Trident Jeddah.
|
|
Watanzania na Wanadiaspora wa Jeddah wakipata chakula |
|
Wanajumuiya wakipata chakula |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.