Friday, February 1, 2019

Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa EAC wamalizika Arusha

Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwa wamesimama kutoa heshima wakati wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiimbwa kabla ya kuanza rasmi Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutsno cha Kimataifa cha Arusha (AICC) tarehe 1 Februari 2019. Katika picha ni Mhe. Yoweri Kaguta Museveni (wa nne kulia), Rais wa Uganda, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (wa tatu kulia), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Paul Kagame (wa nne kushoto), Rais wa Rwanda, Mhe. Uhuru Kenyatta (wa tatu kushoto), Rais wa Kenya, Mhe. Gaston Sindimo (wa pili kulia), Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi ambaye alimwakilisha Rais wa nchi hiyo Mhe. Pierre Nkurunziza, Mhe. Paul Mayom Akechi (wa pili kushoto), Waziri wa Biashara, Viwanda na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Sudan Kusini ambaye alimwakilisha Rais wa nchi hiyo Mhe. Salva Kiir. Wengine katika picha ni Mhe. Kirunda Kivejinja (kulia), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Uganda ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo na Dkt. Liberat Mfumukeko (kushoto), Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Pamoja na mambo mengine, Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda alikabidhiwa uenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja na Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ambaye amemaliza muda wake. Pia Wakuu hao walishuhudia kuapishwa kwa Jaji mpya wa Mahakama ya Haki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Mhe. Jaji Sauda Mjasiri kutoka Tanzania.
Marais wanne walioshiriki Mkutano wa 20 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama wanavyonekana kwenye picha. Kutoka kulia ni Mhe. Dkt. Magufuli, Mhe. Rais Museveni, Mhe. Rais Kagame na Mhe. Rais Uhuru
Mkutano ukiendelea









No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.