Friday, February 15, 2019

Naibu Waziri atembelea Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.) akizungumza na Watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar alipofanya ziara kwenye Ofisi hiyo ikiwa ni miongoni mwa ziara zake za kuzitembelea Taasisi za Wizara zilizopo nje ya Dodoma. Katika mkutano wake na Watumishi hao, Mhe. Naibu Waziri aliwataka  kuanzisha mazungumzo ya pamoja kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara katika vikao vitakavyofanyika kwa zamu baina ya Zanzibar na Dodoma ili kukuza ufanisi wa Wizara kwa ujumla. Wengine katika picha ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Mohammed H. Hamza. Ziara hiyo imefanyika tarehe 15 Februari 2019.
Balozi Hamza akizungumza na kumkaribisha Mhe. Dkt. Ndumbaro kwenye Ofisi za Mambo ya Nje Zanzibar ambapo pia alimweleza mafanikio ya Ofisi hiyo yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu ya kuratibu masuala ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa upande wa Zanzibar.
Bw. Suleiman M. Mohammed, ambaye ni Mhasibu kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar akizungumza wakati wa ziara ya Naibu Waziri
Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Bw. Iddi Seif Bakari, Afisa Mambo ya Nje alipokuwa akieleza changamoto mbalimbali zinazowakabili Watumishi kwenye Ofisi hiyo
Bi. Asia Hamdani, Afisa Tawala kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar nae akizungumza kwenye mkutano kati ya Watumishi wa Ofisi hiyo na Mhe. Naibu Waziri
Mtumishi mwingine ambaye ni Afisa Mambo ya Nje kwenye Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bw. Salim R. Haji akichangia jambao wakati wa mkutano kati ya Watumishi wa Ofisi ya Mambo ya Nje Zanzibar na Naibu Waziri.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.