Thursday, February 7, 2019

Wabunge wa EALA walivyotoa Elimu ya Mtangamano wa EAC

Mkurugenzi Mkazi wa Trade Mark East Africa (TMEA), Bw. John Ulanga akitoa mada kwa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kuhusu shghuli za taasisi hiyo. Alisema taasisi yake inashirikiana na Serikali kuboresha miundombinu mbalimbali kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa biashara katika nchi za EAC inafanyika bila vikwazo.

Waheshimiwa Wabunge wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakijadili kwa pamoja na Mkurugenzi wa TMEA kuhusu mchango wa taasisi hiyo katika kuboresha mwenendo wa biashara baina ya Tanzania na nchi nyingine za EAC.

Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakijadili mada iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkazi wa TMEA.

Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akijadili jambo na Makamu Mkuu wa Chuo cha Dar Es Salaam mara baada ya kuwasili katika chuo hicho kwa ajili ya kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusu EAC. 

Mwenyekiti wa Wabunge wa Tanzania katika Bunge la EALA, Mhe. Dkt. Abdallah Makame (kulia) akipata chakula cha mchana na wanafunzi wa UDSM katika Cafteria Namba moja ya Chuo hicho. Mwenye nguo za bluu ni Mbunge mwenzake wa EALA, Mhe. Pamela Maasay.

Wanafunzi wa UDSM wakipata chakula cha mchana ambapo Wabunge wa EALA walijumuika nao katika chakula hicho.

Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian (kushoto) akibadilishana mawazo na wanafunzi wa UDSM wakati wakipata kwa pamoja chakula cha mchana Cafteria.
Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiwa katika meza kuu kwenye Ukumbi wa Nkurumah kwa ajili ya kuongea na wanafunzi kuhusu fursa za EAC.
Mbunge wa EALA, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe akiwasilisha mada kuhusu EAC kwa wanafunzi wa UDSM.

Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakiongea na wanafunzi wa UDSM kuhusu fursa za Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Wanafunzi walioshiriki kwenye mazungumzo na Wabunge wa EALA. Mwenye suti ya bluu ni Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.
Washiriki wengine katika mazungumzo hayo.


Wanafunzi wakiuliza maswali na kutoa maoni namna Watanzania watakavyofaidika na Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki



Waheshimiwa Wabunge wa EALA wakikabidhi bendera ya EAC kwa viongozi wa UDSM ili iwe inapeperushwa chuoni hapo. Walitoa wito kwa taasisi nyingine, hususan za Serikali kupeperusha bendera hiyo.
Mkutano na Asasi za Kiraia
Mbunge wa EALA, Mwalimu Josephine Sabastian akitoa elimu kuhusu EAC kwa wawakilishi wa Asasi za Kiraia zilizopo hapa nchini.



Majadiliano baina ya Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia kuhusu ushiriki wa asasi hizo katika masuala ya EAC.

Wabunge wa EALA na wawakilishi wa Asasi za Kiraia wakiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Wabunge walisisitiza umuhimu wa wimbo huo kupigwa katika shughuli rasmi za Serikali.
Mdau akifanya tafrisi ya lugha ya ishara kwa watu wenye ulemavu wa kusikia.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.