Friday, February 8, 2019

Naibu Mawaziri watembelea Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja cha Mtukula.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) amekutana na Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Julius Wandera Maganda katika Kituo cha kutoa huduma kwa pamoja mpakani cha Mutukula mpakani mwa Tanzania na Uganda Tarehe 7 Februari 2019. Mara baada ya kukutana walipata fursa ya kutembelea na kujionea namna kituo cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani cha Mtukula (OSBP) kinavyofanya kazi na kufanya Mkutano wa pamoja uliowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Uganda. Mkutano huo umefanyia Mpakani mwa Tanzania na Uganda eneo la Mtukula.

Dkt. Ndumbaro akizungumza na Mhe. Waganda kabla ya kufanya mkutano wa pamoja na wadau mbalimbali. Wengine katika picha ni wajumbe walioongozana na Naibu Mawaziri hao.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt.Ndumbaro (Mb.) akizungumza kwenye Mkutano na wadau mbalimbali pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo.

Naibu Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki wa Uganda, Mhe. Maganda naye akizungumza na wadau pamoja na jumuiya ya wafanya biashara walio hudhuria mkutano huo

Wadau kutoka upande wa Tanzania wakisikiliza kwa makini  wakati Naibu Mawaziri, Mhe. Dkt. Ndumbaro na Mhe. Maganda walipokuwa wakizungumza kwenye mkutano uliyofanyika mpakani wa Tanzania na Uganda-Mtukula
Mhe. Dkt. Ndumbaro akiwa na Mhe. Maganda wakisikiliza kwa makini michango mbalimbali ya wadau iliyokuwa ikiwasilishwa kwenye mkutano.
Mwakilishi wa jumuiya ya wafanya biashara akichangia mada kwenye mkutano
Mmbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Uganda naye akichangia mada wakati wa mkutano huo ukiendelea.

Ujumbe wa Uganda nao wakifuatilia mazungumzo hayo kwa makini.
Viongozi wa pande zote mbili walipata fursa ya kuzungumza na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari waliohudhuria mkutano huo na kuwaelezea yaliyojiri kwenye mkutano.
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa mkutano.
Viongozi hao wakifanya ziara kwenye maeneo mbalimbali ya kituo hicho cha pamoja na kujione namana watendaji wanavyo fanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali ikiwemo namna ya udhibiti wa magonjwa ya mlipuko.
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Maganda wakimsikiliza Afisa wa ukusanyaji mapato kutoka Tanzania Bw. Mohamed Shamte alipokuwa akielezea namna kituo hicho cha pamoja kinavyo fanya kazi. Naibu Mawaziri hao walijione namna watendaji wanavyofanya kazi kwa umakini kwa kutumia vifaa vya kisasa katika kupambana na mambo mbalimbali, ikiwemo udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kama vile Ebola..
Dkt. Ndumbaro pamoja na Mhe. Julius wakiendelea na kukagua  Kituo ili kujionea namna watendaji wake wanavyotoa huduma kwa wananchi wa pande zote mbili.
Katika picha ni jengo la Kituo cha kutolea hudmua kwa pamoja Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Akizungumza kwenye mkutano huo, Mhe. Dkt. Ndumbaro alisema lengo la ziara yao katika kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja Mtukula ni pamoja na kujionea mafanikio na kubaini changamoto zinazokabili utendaji wa kazi na kuzipatia ufumbuzi. 

Akiainisha mafanikio makubwa yaliyofikiwa na kituo hicho , Dkt. Ndumbaro alieleza namna mizigo mbalimbali ikipita kwa wakati kwa kuzingatia taratibu zote zilizopo pamoja na wafanyabiashara kati ya nchi hizi mbili wakifanya biashara zao bila vikwazo vyovyote vile.

Pamoja na mambo mengine Dkt. Ndumbaro alitumia fursa hiyo kuwajulisha wadau mbalimali waliohudhuria mkutano huo, kuwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeanzisha safari za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), kutoka Dar es Salaam, Arusha mpaka Enttebe, Uganda. Mafanikio hayo yametokana na mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliyopo baina ya Tanzania na Uganda na pia kupitia Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. 

Kwa upande wake Mhe Maganda, alifurahishwa na hali ya kituo hicho namna huduma zinavyotolewa. Aidha, aliahidi kuwa Serikali ya Uganda itaongeza watendaji kazi kwenye kituo hicho ili kuwezesha upande wa Uganda kufanya kazi masaa 24 kama ilivyo kwa upande Tanzania. Pia alisisitiza nchi yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali ya Ushirikiano.
    
Pia katika Mkutano huo wadau walitoa pongezi kwa viongozi wa Serikali za pande zote mbili kwa kuanzisha kituo hicho cha kutolea huduma kwa pamoja mpakani Mtukula, ambapo walisema kuanzishwa kituo hicho kumeongeza chachu ya maendeleo kwa wafanyabiashara wa pande zote mbili ambapo wamekuwa wakisafirisha bidhaa zao kwa wingi bila kupata changamoto kulinganisha na hapo awali kabla ya kuanzishwa kwa kituo hicho.

 Kadhalika wadau walitoa pongezi kwa watendeji waliopo kituoni hapo kwa upande wa Tanzania, kwa kutoa huduma nzuri kwa masaa 24 kwenye kituo hicho ambapo, imepelekea wafanyabiashara kutokupoteza muda mwingi wafikapo mpakani hapo. 


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
9 Februari 2019















No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.