Waziri wa Katiba na Sheria ambaye pia ni Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Kikao cha 40 cha Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (wa tatu kushoto) akizungumza na Kamishna wa Haki za Biandamu, Bi. Michelle Bachelet (mwenye miwani kulia) kuhusu masuala ya haki za binadamu. Wakati wa mazungumzo yao, Bi. Bachelet aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kupambana na rushwa, kupigia hatua za maendeleo ya kiuchumi, kuendelea kuwahifadhii wakimbizi na ushiriki katika ulinzi wa amani barani Afrika. Kwa upande wake, Prof. Kabudi alisema Tanzania itaendeea kulinda Haki za Binadamu kwa wananchi wote na kuahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Kamishna huyo. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.