Tuesday, May 28, 2019

Makamu wa Rais ashiriki sherehe za uapisho za Rais wa Comoro



Dodoma, 28 Mei 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 

Makamu wa Rais ashiriki sherehe za uapisho za Rais wa Comoro

Kufuatia Mwaliko kutoka Serikali ya Comoro, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliongoza ujumbe wa Tanzania katika sherehe za kuapishwa kwa Rais Mteule wa Muungano wa Visiwa vya Comoro, Mhe. Azali Assouman zilizofanyika Moroni, terehe 26 Mei 2019.

Sherehe hizo zinafuatia ushindi alioupata Mhe. Azali katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika tarehe 24 Machi  2019.

Mara baada ya Sherehe za Uapisho, Mhe. Makamu wa Rais alipata fursa ya kufanya mazungumzo na Mhe. Azali ambapo katika mazungumzo hayo, Mhe. Makamu wa Rais aliishukuru Serikali na Wananchi wa Comoro kwa mwaliko na mapokezi mazuri.

Aidha, aliwasilisha salamu za pongezi kutoka kwa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kumhakikishia kuendeleza uhusiano na ushirikiano wa kihistoria baina ya nchi hizi mbili.

Kwa upande wake, Mhe. Azali alielezea furaha yake kwa ujio wa Mhe. Makamu wa Rais na kueleza kwamba hiyo ni ishara ya udugu na uhusiano mzuri baina ya Tanzania na Comoro.

Aidha, Mhe. Rais alieleza kwamba kutokana na maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Serikali ya Tanzania, ipo haja kwa Tanzania kuendelea kuisadia Comoro katika sekta mbalimbali.

Mwisho, aliishukuru Tanzania kwa salamu za pole kufuatia nchi hiyo kukumbwa na kimbunga Kenneth tarehe 26 Aprili 2019.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
                          
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Comoro,Mhe. Azali Assouman jijini Moroni, Comoro. Mhe. Makamu wa Rais alikwenda nchini humo kushiriki sherehe za uapisho za Rais huyo zilizofanyika tarehe 26 Mei 2019.

Thursday, May 23, 2019

Waziri Prof. Kabudi akutana na Kiongozi wa Kanisa la Othodox

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II,katika ofisi ndogo za Wizara zilizoko Dar Es Salaam.
May 23,2019
Waziria wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II pamoja na ujumbe alioambatana nao,katika ofisi ndogo za Wizara zilizoko Dar Es Salaam.
May 23,2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II katika Ofisi ndogo za Wizara zilizoko Dar Es Salaam,May 23,2019


Tuesday, May 21, 2019

Waziri Kabudi akutana na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID)

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson alipomtembelea na baadhi ya wajumbe wake katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 21, 2019
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimwelezea jambo Bi. Jane Edmondson pamoja na ujumbe alioambatana nao
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Uingereza (DFID) Bi. Jane Edmondson  (wa pili kutoka kushoto) pamoja na wajumbe alioambatana nao, wa kwanza kushoto ni Afisa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Tunsume Mwangolombe





Call for Applications for the 2019/2020 Academic Year at the Pan African University

Dodoma. 21st May 2019

PRESS RELEASE

Call for Applications for the 2019/2020 Academic Year at the Pan African University
                                                                                                                 The Pan African University an initiative of the Heads of State and Government of the African Union is inviting young, qualified, talented and enterprising Tanzanians to apply for Masters or PhD degree programmes at any of the four Pan African University Institutes listed below:

  • Pan African University Institute for Basic Sciences Technology and Innovation (PAUST) at Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology (JKUAT) Kenya;

  • Pan African University Institute for Life and Earth Science including Health and Agriculture (PAULESI), at the University of Ibadan (UI), Nigeria;

  • Pan African University Institute for Governance, Humanities and Social Science (PAUGHSS), at the University of Yaoundé II and the University of Buea, Cameroon; and


  • Pan African University Institute for Water Energy Sciences-including climate change (PAUWES), at the University of Tlemcen, Algeria.


Interested candidates should visit the following links for enquiries and more details: - https://www.au-pau.org/submission and pau.scholarships@africa-union.org.

 

The call for applications is open from May 14, 2019 to June 27, 2019.


Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation

Waziri Kabudi akutana na Balozi wa Uingereza nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke alipomtembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 20, 2019
Maafisa Ubalozi wa Uingereza hapa nchini wakisikiliza mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Sarah Cooke (hawapo pichani)
Mazungumzo yakiendelea



Waziri Kabudi akutana na Balozi wa Iran nchini Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimuelezea jambo Balozi wa Iran hapa nchini Mhe. Mousa Farhang alipomtembelea katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam Mei 20, 2019
Maafisa Ubalozi wa Irani hapa nchini wakisikiliza mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mousa Farhang (hawapo pichani)
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Balozi Mousa Farhang (hawapo pichani), katikati ni Mkurugenzi Kitengo cha Habari na Mawasiliano Bw. Emmanuel Buhohela, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati Bw. Ayubu Mndeme (wa kwanza kushoto) na Katibu wa Waziri Bw. Murobi Magabilo
Mazungumzo yakiendelea.





VACANCY ANNOUNCEMENT AT THE AU COMMISSION


Dodoma, 21st May 2019

PRESS RELEASE

Job Announcement at the African Union Commission

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commission of African Union inviting qualified Tanzanians to apply for the posts available at the Commission.

The vacant positions currently available in the commission are as follows:-
Position
Department
Location
Deadline
DIRECTOR OF TRADE AND INDUSTRY
Department of Trade and Industry
Ethiopia
3/6/2019
DIRECTOR OF PEACE AND SECURITY
Peace and Security Department
Ethiopia
10/6/2019
HEAD CRISIS MANAGEMENT AND POST-CONFLICT RECONSTRUCTION DIVISION (CMPCRD)
Peace and Security Department
Ethiopia
10/6/2019

Details of the positions are available through the AUC E-recruitment Website http://aucareers.org/.


Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation.


Monday, May 20, 2019

Tanzania na Uholanzi zazindua Mradi wa Kukua na Kuku



Dodoma, 20 Mei 2019

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tanzania na Uholanzi zazindua Mradi wa Kukua na Kuku

Ubalozi wa Tanzania nchini Uholanzi kwa kushirikiana na Baraza la Biashara la Uholanzi na Africa (Netherlands – Africa Business Council - NABC) hivi karibuni waliongoza ujumbe wa Makampuni 7 kutoka Uholanzi yaliyobobea katika Sekta ya Ufugaji wa Kuku kwenda Mkoani Kilimanjaro kuzindua Mradi maalum wa ufugaji utakaoendeshwa na Makampuni hayo nchini Tanzania maarufu kama “Kukua Na Kuku (Growing with Chicken) Impact Cluster”.
      Mradi wa “Kukua Na Kuku” ni matokeo ya makubaliano ya kuanzisha ubia kati ya Tanzania na Uholanzi yanayolenga kuboresha Sekta ya Ufugaji Kuku nchini Tanzania na kuifanya kuwa endelevu kwa kutumia teknolojia ya kisasa kutoka Uholanzi. Makampuni hayo yatatoa mafunzo kwa lengo la kuwajengea uwezo wafugaji wazawa kwa kuboresha usimamizi wa kilimo cha ufugaji, afya ya wanyama, upatikanaji wa chakula (lishe) bora kwa ajili ya mifugo, vifaa muhimu vya kufugia, na hata utafutaji masoko.
Uzinduzi huo ulifanyika kwenye Chuo cha Kilimo na Ufugaji wa Mifugo Kilacha, Mkoani Kilimanjaro kwa kusaini Makubaliano ya Ushirikiano, na ukawa ndio mwanzo wa ushirikiano wa miaka 3 kati ya makampuni hayo 7, Serikali ya Uholanzi na wadau wazawa wa Tanzania. Chuo cha Kilimo na Ufugaji wa Mifugo cha Kilacha kinasimamiwa na Kituo cha Uzalishaji na Mafunzo kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Mkoani humo.
Mgeni rasmi wakati wa sherehe za uzinduzi huo alikuwa Mhe. Anna Mgwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju, Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Bibi Lianne Houben, na Mkurugenzi wa Biashara na Kilimo wa NABC, Bw. Mackenzie Masaki.

Makampuni hayo kutoka Uholanzi ni pamoja na: Aeres University of Applied Sciences; Ebit+/I Grow Chicken; GD Animal Health; Impex; Hendrix Genetics; Koudijs de Heus; na Vencomatic Group.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Dkt. Anna Mngwira ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Mradi wa Kukua na Kuku akitoa neno katika sherehe za uzinduzi wa Mradi huo. Kushoto kwake ni Padri Paul Huria, Msaidizi wa Meneja Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji na Mafunzo, Kilacha akimsikiliza kwa makini.
Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (pichani juu) na Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania, Bibi Lianne Houben (pichani chini) wakitoa hotuba fupi wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Kukua Na Kuku huko Kilacha, Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
Kutoka kulia ni Padri Landelimi Makiluli, Meneja Mkuu wa Kituo cha Uzalishaji na Mafunzo, Kilacha; Padri (Monsignor) Paul Huria, Msaidizi wa Meneja Mkuu wa Kituo; Mhe. Dkt. Anna Mgwira, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro; Bibi Lianne Houben, Kaimu Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania; na mwishoni kushoto ni Mhe. Irene Kasyanju, Balozi wa Tanzania nchini Uholanzi wakijiandaa na uzinduzi wa Mradi wa Kukua na Kuku
Wawakilishi wa Taasisi zenye ubia katika Mradi wa Kukua na Kuku wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro wakiweka saini Makubaliano ya Ushirikiano tayari kuanza utekelezaji wa Mradi huo huko Kilacha, Mkoani Kilimanjaro
Picha ya pamoja baada ya kusainiwa Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania, Serikali ya Uholanzi, Makampuni tajwa 7 yakiongozwa na Mkurugenzi wa Biashara na Kilimo kutoka NABC, Bw. Mackenzie Masaki (wa pili kutoka kushoto). Wa kwanza kushoto ni Bibi Theo Mutabingwa, Afisa Kilimo katika Ubalozi wa Uholanzi nchini Tanzania.
Balozi Irene Kasyanju akibadilishana mawazo na wawakilishi wa Kampuni ya Hendrix Genetics, Bw. Peter Arts (kushoto); na Ebit+/I Grow Chicken, Bw. Eric Mooiweer (kulia) mara baada ya uzinduzi wa Mradi wa Kukua na Kuku utakaoendeshwa na Makampuni tajwa 7 kutoka Uholanzi 









Saturday, May 18, 2019

Waziri wa Mambo ya Nje akutana na Jumuiya ya Mabohora.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.), akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora, Zainuddin Adamjee,katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam tarehe 18 Mei, 2019.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.), akiwa katika mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora, Zainuddin Adamjee,katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Ujumbe uliombatana na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora Zainuddin Adamjee wakimuonesha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki,Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.), kitabu chenye picha mbalimbali zilizopiga wakati wa mkutano wa jumuiya hiyo uliofanyika Jijini Dar es salaam na kuhudhuriwa na mabohora zaidi ya 30 elfu kutoka duniani kote ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alijumuika nao. 


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohora, Zainuddin Adamjee na ujumbe alioambatana nae mara baada ya mazungumzo,katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Jijini Dar es Salaam.

Friday, May 17, 2019

Fursa za ajira

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

NAFASI ZA AJIRA KATIKA SEKRETARIETI YA JUMUIYA YA MADOLA, LONDON, UINGEREZA.

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, inawahamasisha Watanzania wenye sifa kuomba nafasi ya ajira katika Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola, London, Uingereza.

Ajira hizo ni :-

Afisa Msaidizi Programu ya Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (Assistant Programmes Officer – Monitoring and Evaluation Unit) na

Meneja Utafiti wa masuala ya Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Research Manager-Economic, Youth and Sustainable Development).

Taarifa zote muhimu kuhusu fursa hizo za ajira zinapatikana kwa kupitia  tovuti  http://thecommonwealth.org.jobs.

Mwisho wa kutuma maombi ya nafasi hizo ni tarehe 23 Mei, 2019.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya Sarahawi awasilisha nakala za hati za utambulisho kwa Waziri Kabudi.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akipokea nakala za hati za utambulisho za Mhe. Mahayub Buyema Mahafud, Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu ya  Sarahawi nchini Tanzania.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika mazungumzo na Bwana. Mahayub Buyema Mahafud, Balozi mteule wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kiarabu Sarahawi.


Profesa Kabudi akutana na mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.)  akiwa katika mazungumzo na Mhe. Mikel Kafando ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Burkina Faso na Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Mikel Kafando ambaye ni Rais Mstaafu wa Burkina Faso na Mjumbe Maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Burundi.

Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (Afdb) aitembelea Tanzania




Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina alipokwenda kumpokea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.


Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia aitembelea Tanzania.

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akisalimiana na Mhe.Ivica Dacic,Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Mhe.Ivica Dacic,Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia na baadhi ya wajumbe aliombatana nao.


 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi akiwa katika mazungumzo na Mhe.Ivica Dacic, Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia.

 Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Kabudi (Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Mhe.Ivica Dacic,Naibu Waziri Mkuu wa Kwanza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Serbia,wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Kasidi Faraji Mnyepe. 










Job Announcement at the African Union Commission

Dodoma, 17 May 2019
PRESS RELEASE

Job Announcement at the African Union Commission
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received vacancy notification from the Commission of African Union inviting qualified Tanzanians to apply for the posts available at the Commission.

The vacant positions currently available in the commission are as follows:
Position
Department
location
Deadline
DESKTOP-PUBLISHER
DIRECTORATE OF Conference & Publication Management
Ethiopia
30/5/2019
DIRECTOR-INTER-AFRICAN BUREAU FOR ANIMAL RESOURCES ((IBAR)
Department of Rural Economy & Agriculture.
Kenya
27/5/2019
DIRECTOR-INTER-AFRICAN BUREAU FOR ANIMAL RESOURCES ((IBAR)
Department of Rural Economy & Agriculture
Kenya
30/5/2019

Details of the positions are available on the Union career website http://aucareers.org/.

Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,