Saturday, June 10, 2023

WAZIRI TAX AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IFAD

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario walipokuna kwa mazungumzo katika makao makuu wa Shirika hilo jijini Roma, Italia.

Waziri mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax amekutana na kuzungumza na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario jijini Roma na kubadilishana mawazo juu ya njia za kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na IFAD ili kuweza kunufaika na miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendeshwa na shirika hilo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Rais wa IFAD Dkt. Alvaro Lario katika picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Rais wa IFAD Dkt. Alvaro Lario wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika jijini Roma, Italia

Mazungumzo yakiendelea


DKT TAX AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA FAO

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax akisalimiana na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Dr. Qu Dongyu jijini Roma nchini Italia tarehe 09 Juni, 2023.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax akiwa  na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Dr. Qu Dongyu walipokutana jijini Roma nchini Italia tarehe 09 Juni, 2023.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax na  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Dr. Qu Dongyu wakizungumza walipokutana jijini Roma nchini Italia tarehe 09 juni, 2023.

mazungumzo yakiendelea na kushuhudiwa na wajumbe wa pande mbili.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Dr. Qu Dongyu katika picha ya pamoja na wajumbe wao walipokutana jijini Roma nchini Italia tarehe 09 Juni, 2023.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax amekutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO) Dr. Qu Dongyu jijini Roma. 

Katika mazungumzo yao Dkt. Tax ameipongeza FAO kwa jitihada za kukusanya rasilimali kwa ajili ya jamii mbalimbali kunufaika na miradi ya maendeleo ya Shirika hilo ambazo pia Watanzania wengi  wanazitegemea na kunufaika nazo.

 

Friday, June 9, 2023

DKT. TAX AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA IFAD JIJINI ROMA

 

Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario akimpokea na kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax akisalimiana na walipokutana jijini Roma nchini Italia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax katika picha na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario walipokutana jijini Roma nchini Italia. 

 

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax akizungumza na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario walipokutana jijini Roma nchini Italia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax katika picha na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario baada ya kumaliza mazungumzo yao

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Tax amekutana na kuzungumza na Rais wa Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) Dkt. Alvaro Lario jijini Roma. 









Katika mazungumzo yao viongozi hao wamejadiliana jinsi Tanzania inavyoweza kunufaika na miradi mbalimbali inayoendeshwa na Shirika hilo katika sekta ya kilimo.

 

KAMPUNI YA TULLY’S YA JAPAN YAZINDUA UUZAJI WA KAHAWA YA TANZANIA KATIKA MIGAHAWA YAO


Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda (kulia) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mauzo wa Kampuni ya Tully’s inayomiliki migahawa maarufu ya Tully's nchini Japan, Bw. Daisuke Shindo wakati wa uzinduzi wa uuzaji rasmi wa kahawa ya Tanzania kwenye migahawa hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Tokyo tarehe 9 Juni 2023

Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda (katikati) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mauzo wa Kampuni ya Tully’s inayomiliki migahawa maarufu ya Tully's nchini Japan, Bw. Daisuke Shindo (kulia) pamoja na Meneja Mkuu wa Idara ya Bidhaa za Vinywaji wa Kampuni ya Marubeni ambayo ni mbia wa Tully’s na miongoni mwa kampuni zinazosafirisha kwa wingi kahawa kutoka Tanzania kuingia nchini Japan, Bw. Masahiko Yoshimura (kushoto) wakati wa uzinduzi wa uuzaji rasmi wa kahawa ya Tanzania kwenye migahawa hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Tokyo tarehe 9 Juni 2023

Mhe. Balozi Luvanda (wa tatu kulia) akiwa na Bw. Shindo ( wa tatu kushoto) na wadau wengine wa Japan wakati wa zoezi la uonjaji wa kahawa ya Tanzania

Wadau mbalimbali wa Japan wakishiriki hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa kahawa ya Tanzania kwenye migahawa ya Tully's ya nchini Japan

Mhe. Balozi Luvanda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Bw. Shindo (wa tatu kulia)  na Bw. Yoshimura (wa tatu kushoto) na Maafisa kutoka Ubalozi wa Tanzania nchini Japan na wadau wengine wakati wa uzinduzi wa uuzaji wa kahawa ya Tanzania kwenye migahawa ya Tully's iliyopo Japan

Balozi Luvanda akiwa katika picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Mauzo wa Kampuni ya Tully’s inayomiliki migahawa maarufu ya Tully's nchini Japan, Bw. Daisuke Shindo

Mhe. Balozi Luvanda akionesha baadhi ya kahawa za Tanzania zinazouzwa nchini Japan

Mhe. Balozi Luvanda akihojiwa na Mtangazaji kutoka Shirika la Utangazaji la Japan-NHK, Idhaa ya Kiswahili kuhusu jitihada za Ubalozi zilivyofanikisha uuzaji wa kahawa ya Tanzania kwenye migahawa maarufu ya Tully's ya nchini Japan.

Kahawa ya Tanzania kama inavyoonekana pichani

==========================================================

Kampuni ya Tully’s inayomiliki migahawa maarufu ya TULLY’s imezindua rasmi uuzaji wa kahawa ya Tanzania katika migahawa yao yote 700 iliyoko nchini Japan  katika hafla iliyofanyika jijini Tokyo tarehe 9 Juni 2023.


Uzinduzi huo ambao ulienda sambamba na zoezi la uonjaji wa kahawa ya Tanzania, ulishuhudiwa na Balozi wa Tanzania nchini Japan, Mhe. Baraka Luvanda;  Mkurugenzi Mtendaji wa Mauzo wa Tully’s; Bw. Daisuke Shindo pamoja na Meneja Mkuu wa Idara ya Bidhaa za Vinywaji wa Kampuni ya Marubeni ambayo ni mbia wa Tully’s na miongoni mwa kampuni zinazosafirisha kwa wingi kahawa kutoka Tanzania kuingia nchini Japan, Bw. Masahiko Yoshimura.


Akitoa hotuba yake katika uzinduzi huo, Balozi Luvanda alizihakikishia kampuni za Japan, uwepo wa mazingira wezeshi ya biashara na hata uwekezaji wanapoamua kuwekeza katika kilimo au sekta nyingine za Tanzania.

 

Aidha, amelitaja kuwa zao la kahawa ni miongoni mwa mazao ya kimkakati nchini ambalo linatumika kibiashara kwa kulipatia Taifa pato kubwa kwa mauzo mengi ya kigeni. Akitolea mfano wa Japan, alieleza kuwa kwa mwaka, Tanzania inauza kahawa yake Japan, kwa wastani wa asilimia 33 ya kahawa inayolimwa nchini, ambayo ni sawa na wastani wa kilogramu million 15 (tani 15,000) ya kahawa yote ya Tanzania inayouzwa nchini Japan.


Balozi Luvanda alieleza kuwa, soko la kahawa nchini Japan bado ni kubwa, ikilinganishwa na matumizi na uhitaji wa Japan ambapo, Japan inahitaji wastani wa kilogramu milioni 453 (tani 453,000) za kahawa kwa mwaka na kutoa rai kwa watanzania hususan, wakulima wa zao la kahawa, watayarishaji, wasafirishaji na wafanyabiashara wa zao hili kuchangamkia fursa ya soko kubwa la Japan ambalo linakua siku hadi siku.


“Napenda kutoa wito kwa watanzania wenzangu kuzingatia ubora wa viwango kwa mazao tunayolima nchini kwani nchi nyingi tunazouza bidhaa zetu hususan, hapa Japan wanazingatia sana viwango. Hivyo, ili kulikamata soko hili la Japan ipasavyo, inatupasa kwenda sambamba na mahitaji ya kidunia ikiwemo, uzalishaji kwa viwango bora” alieleza Balozi Luvanda.

 

Vilevile, Balozi Luvanda alieleza juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan,  kuwa imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya kilimo kwa kuwekeza katika miradi ya muda mrefu na mifupi pamoja na maeneo ya msingi ya kutatua changamoto za kilimo kuanzia shambani hadi sokoni ili kujihakikishia uhakika wa chakula, kulisha wengine kibiashara duniani, na pia wakulima kujipatia kipato cha kutosha ili kupunguza umaskini.

 

“Serikali ya Tanzania kwa kasi kubwa imewekeza kwenye rasilimali fedha na watu pamoja na uhamasishaji wa sekta binafsi kuwekeza na kukifanya kilimo kuanza kutoa ajira zenye staha hususan, kwa vijana na wanawake, ikiwa ni pamoja na hatua ya kuongeza bajeti ya Wizara ya Kilimo na kujenga msingi imara wa utekelezaji wa mipango ya kilimo yenye kutazama Tanzania ifikapo mwaka 2050”, alieleza.

 

Alihitimisha hotuba yake kwa kuelezea jitihada za ubalozi za kufanikisha azma ya Serikali ya Tanzania katika mageuzi ya sekta ya kilimo ya kukifanya kuwa biashara. “Ubalozi unatekeleza jukumu kubwa la kuendelea kutafuta masoko ya bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini ikiwemo, mazao ya kilimo kama kahawa, kwa kuzitangaza bidhaa hizo na kutafuta wawekezaji wa kuendeleza sekta mbalimbali kama vile sekta ya kilimo hususan, kilimo cha biashara kwa mazao ya kimkakati”, alihitimisha.

 

Kadhalika,  Balozi Luvanda alihamasisha ushiriki wa wadau wa kahawa nchini katika Maonesho ya Kimataifa ya Kahawa ya Mwaka 2023 (World Specialty Coffee Conference and Exhibition 2023) yatakayofanyika jijini Tokyo kuanzia tarehe 27  hadi  29 Septemba 2023, ambayo yanaratibiwa na Ubalozi kwa kushirikiana na Bodi ya Kahawa Tanzania. Tanzania ilishiriki kikamilifu katika Maonesho hayo kwa mwaka 2023 na manufaa yake yameonekana.


Tully’s Co. Ltd., inamiliki migahawa takribani 700 nchini Japan na imejipatia umaarufu mkubwa katika biashara ya uuzaji wa kahawa za aina mbalimbali duniani. Kahawa ya Tanzania iliyozinduliwa ni kutoka Mashamba ya Kahawa ya GDM (GDM Farms) yaliyoko Mbozi mkoani Mbeya.


Kuzinduliwa kwa kahawa ya GDM nchini Japan kunapandisha zaidi uhakika wa soko la kahawa ya Tanzania nchini Japan ambayo imejizolea umaarufu mkubwa kwa ubora na radha ya aina yake na kupelekea kupewa jina maarufu la kibiashara la Kilimanjaro Coffee. Jina hili hutumika nchini Japan, kwa kahawa zinazozalishwa Tanzania pekee, kwa kutambua kivutio kikubwa cha Mlima Kilimanjaro uliopo nchini Tanzania.

 

Tanzania inasifika Japan kwa kutoa kahawa bora aina ya Arabica (Arabica laini - full washed na Arabica ngumu - natural) inayolimwa katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mara, Tanga, Morogoro, Njombe, Iringa, Katavi, Rukwa, Ruvuma, Kigoma, Songwe na Mbeya; na kahawa ya Robusta inayolimwa mkoani Kagera.

 

IMETOLEWA NA UBALOZI WA TANZANIA NCHINI JAPAN

TAREHE 9 JUNI 2023

 








 

DKT. TAX AZUNGUMZA NA NAIBU WAZIRI MKUU NA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA WA ITALIA JIJINI ROMA


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisalimiana na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani walipokutana kwa mazungumzo yaliyofanyika ofisini kwake jijini Roma, Italia tarehe 9 Juni, 2023.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Roma, Italia. Akishuhudia nyuma yao ni Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahamoud Thabit Kombo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akizungumza na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani walipokutana kwa mazungumzo ofisini kwake jijini Roma, Italia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na ujumbe wake upande wa kulia wakizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani na ujumbe wake walipokutana kwa mazungumzo Ofisini kwake jijini Roma, Italia.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax (Mb) amekutana na kuzungumza na Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Antonio Tajani ofisini kwake jijini Rome nchini Italia tarehe 9 Juni,2023 

Akizungumza na mwenyeji wake Mhe. Dkt. Tax ameelezea kuridhishwa na uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Italia na kuishukuru Serikali ya Italia kwa kuendelea kuiunga mkono Serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo kupitia maeneo ya elimu, afya, kilimo, mabadiliko ya hali ya hewa na uchumi wa buluu.

Mhe. Dkt. Tax ameihakikishia Italia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Tanzania na kuhakikisha uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Italia unakuwa na kufikia ngazi ya juu.

Dkt. Tax amependekeza kuanzishwa kwa mfumo wa majadiliano ya kisiasa kati ya Tanzania na Italia ambao utatumika kama jukwaa la kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo kwa maslahi mapana ya pande zote.

“Nafahamu kuwa nchi zetu hazina mfumo wa majadiliano wa kisiasa na kidiplomasia licha ya kuwa na uhusiano mzuri wa siku nyingi, napendekeza tuanzishe mfumo wa majadiliano ya kisiasa kati ya nchi zetu, mfumo ambao utatumika kama jukwaa la kuimarisha zaidi ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizi kwa maslahi ya pande zote,” alisema Dkt. Tax.

Dkt. Tax ameipongeza Serikali ya Italia kwa kuendelea kuwa mdau mkubwa wa mpango mkakati wa maendeleo na sera za taifa na kuishukuru kwa mikopo ya masharti nafuu wenye nia ya kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mafunzo ya ufundi na kuwezesha vijana kujiajiri katika mikoa ya Mbeya, Arusha, Mwanza, Songwe, Zanzibar na Dar es Salaam. 

Pia ameelezea shukurani za Serikali ya Tanzania kwa Serikali ya Italia kwa mkopo wa masharti nafuu kwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) na Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambao utawezesha utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usajili wa Taarifa muhimu kwa Tanzania Bara ambapo watoto chini ya miaka MITANO watasajiliwa.

Akizungumza katika kikao hicho Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikino wa Kimataifa Mhe. Anthonio Tajan amesema Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania kama mdau mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi na kuahidi kuwa Serikali ya Italia itaandaa kongamano la wafanyabiashara ili kuwawezesha wafanyabiashara wa Nchi hizo mbili kufahamiana na kupata fursa za kufanya kazi kwa pamoja. 

Amemuhakikishia Mhe Waziri kuwa Serikali ya Italia imedhamiria kuendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania na nchi za Afrika kwa ujumla katika sekta mbalimbali. 

WAZIRI TAX: WATUMISHI TEKELEZENI DIPLOMASIA YA UCHUMI KWA BIDII


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akisaini kitabu cha wageni aliposili katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Italia

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.Dkt. Stergomena Tax amewataka watumishi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia kutekeleza Diplomasia ya Uchumi kwa bidii ili kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Akizungumza na watumishi hao katika Ofisi za Ubalozi huo Jijini Roma, Mhe. Dkt. Tax amesema Serikali inawategemea wao kama wadau wa kubwa katika kutekeleza diplomasia ya uchumi ili kuinufaisha nchi.

“Wizara inategemea Balozi katika kutekeleza diplomasia ya uchumi, kwa hiyo mna wajibu wa kuhakikisha mnafanya kazi hii kwa ukamilifu” alisema Dkt.Tax.

Aidha, Dkt. Tax ameupongeza Ubalozi huo kwa kuandaa mkakati wa kutekeleza diplomasia ya uchumi katika eneo lake la uwakilishi na kuzitaka Balozi nyingine za Tanzania kuiga mfano huo.

“Nimesikia hapa mmeandaa mpango mkakati wa kutekeleza Diplomasia ya Uchumi katika eneo lenu, hili ni jambo zuri niwapongeze kwa hilo na balozi zetu nyingine hazina budi kuiga mfano huu,” alisema Dkt. Tax

Aliongeza kuwa Wizara inatengeneza mkakati wa kitaifa wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi, tutawaletea muuone na mtoe maoni yenu ili kuuboresha zaidi.

Amesema anaamini kuwa kupitia mkakati huo Wizara itajifunza kitu na hivyo kuja na mkakati bora wa utekelezaji wa diplomasia ya uchumi.

Mhe.Waziri amewasihi watendaji wa ubalozi kuhakikisha wana shirikisha sekta binafsi katika kutekeleza kazi zao kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondoa uwiano mdogo wa kibiashara uliopo kati ya Tanzania na Italia.

Awali akizungumza katika kikao hicho Balozi wa Tanzania nchini Italia, Mhe. Mahmoud Thabit Kombo alisema ubalozi unaendelea kusimamia na kutekeleza diplomasia ya uchumi kupitia utalii,kilimo,uwekezaji, biashara na masoko ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na nchini inazowakilisha.

Alisema ubalozi pia unashirikisha Diaspora katika shughuli za maendeleo ya nchi na kupongeza mpango wa kusajili Diaspora wa Tanzania kwa njia ya Kidigitalia

Mhe. Dkt. Tax yuko nchini Italia kwa ziara ya kikazi ambapo anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Italia
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax akifuatilia taarifa iliyokuwa ikiwasilishwa na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Kombo wakati wa kikao kazi watumishi wa Ubalozi huo. Kushoto ni Mkurugezi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Swahiba Mndeme na kulia ni Mkuu wa Utawala Ubalozi wa Utalia Bi. Jubilata Shao
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Kombo wakiwa picha ya pamoja
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Stergomena Tax na Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud Kombo wakiwa picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi 

Balozi wa Tanzania nchini Italia Mhe. Mahmoud T. Kombo akielezea jambo kwa Waziri Tax alipokuwa akitembelea maeno ya Ubalozi

Tuesday, June 6, 2023

NAIBU WAZIRI, BALOZI MBAROUK AKAGUA MAENDELEO YA UJENZI WA JENGO LA OFISI YA WIZARA

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Fatma M. Rajab alipowasili eneo la Mtumba inapojengwa jengo la ofisi la Wizara hiyo kwa ajili ya kujionea maendeleo ya ujenzi.

Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Majengo katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhandisi John Kiswaga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma M. Rajab kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara katika eneo la Mtumba

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili eneo la Mtumba kujionea maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiangalia ngazi za kuingilia lango kuu la jengo la Ofisi ya Wizara linalojengwa Mtumba jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akiangalia maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Wizara eneo la Mtumba jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma M. Rajab wakiongea na wakandarasi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara katika eneo la Mtumba jijini Dodoma

Hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Wizara linalojengwa eneo la Mtumba jijini Dodoma. Jengo limefikia zaidi ya asilimia 70 ambayo ni hatua inayokwenda sambamba na Mkataba wa ujenzi 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara Mtumba jijini Dodoma

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb) na Naibu Katibu Mkuu, Balozi Fatma M. Rajab wakiongea na wakandarasi kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara katika eneo la Mtumba jijini Dodoma