Saturday, July 21, 2012

Rais Kikwete ampokea Mhe. Barroso, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU)


Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akimkaribisha Mhe. Jose Manuel Barroso, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EU) mara baada ya kuwasili Ikulu leo tarehe 21 Julai, 2012.


Mhe. Rais Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mhe. Barroso mara bada ya kumpokea Ikulu leo.


Mhe. Rais Kikwete na Mhe. Barroso wakiwashuhudia Mhe. Dkt. William Mgimwa, Waziri wa Fedha wa Tanzania na Bw. Andris Piebalgs, Kamishna wa Maendeleo wa Umoja wa Ulaya wakisaini mikataba ya  ushirikiano katika sekta mbalimbali baina ya Tanzania na Umoja huo,  Ikulu jijini Dar es Salaam tarehe 21 Julai, 2012.


Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa pamoja na Bw. Ramadhan Kijjah (wa kwanza kulia), Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na mjumbe kutoka Wizara hiyo wakati mikataba ya ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya ikisainiwa Ikulu, Dar es Salaam leo.

Mhe. Rais Kikwete akifafanua jambo kwa Mhe. Barroso mara baada ya mazungumzo yao Ikulu leo.


Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Dkt. Mgimwa, Bw. Kijjah, Balozi Irene Kasyanju, Balozi Dorah Msechu na wadau wengine kutoka Serikalini mara baada ya kusaini mikataba na Umoja wa Ulaya, Ikulu leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.