Sunday, December 20, 2020
JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YAJIVUNIA MRADI WA UJENZI WA BWAWA LA KUZALISHA UMEME LA JULIUS NYERERE.
Saturday, December 19, 2020
Ujumbe wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki watembelea Mradi wa Ujenzi wa SGR
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote akitembea pembezoni mwa reli ambayo ipo katika hatua za mwisho za ujenzi. |
Friday, December 18, 2020
TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IORA
TANZANIA KUIMARISHA USHIRIKIANO NA IORA
Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano na Jumuiya ya Nchi zilizo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) katika kutekeleza mikakati ya uchumi wa bluu ambao unalenga kuimarisha sekta ya uvuvi hususan uvuvi wa bahari kuu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha amesema hayo aliposhiriki Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Nchi zilizopo kwenye Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA) uliofanyika tarehe 17 Disemba, 2020 kwa njia ya mtandao.
Amesema Tanzania itaboresha Sekta ya Uvuvi kwa kuimarisha kilimo cha mwani, utalii wa meli (cruise tourism), michezo ya baharini, utafutaji wa rasilimali za mafuta na gesi kwenye eneo la bahari, ujenzi wa bandari maalum za uvuvi, mafuta na gesi na masuala mengine muhimu ya kuimarisha uchumi na ustawi wa wananchi.
Mhe. Ole Nasha ametumia mkutano huo kuwakaribisha wenye nia ya kuwekeza nchini kuja kwa wingi ili kutumia rasilimali zilizopo kwa pamoja na kwa faida ya pande zote mbili.
Amesema Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia rasilimali zilizopo katika bahari ya Hindi na kuweka mazingira wezeshi ya uwekezaji ili kuwavutia na kuimarisha Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi.
Mkutano wa 20 wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo ya IORA umejadili masuala ya maendeleo katika eneo la Bahari ya Hindi ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa mpango kazi wa Jumuiya ya IORA wa mwaka 2017 – 2021. maandalizi ya mpango kazi mpya wa IORA wa mwaka 2022 – 2026; ushiriki na ushirikishwaji wa washirika wa mazungumzo katika masuala ya miradi na program za Jumuiya; masuala ya ulinzi na usalama wa bahari ya Hindi, mkakati wa kupambana na uhalifu, uharamia na biashara haramu ya binadamu katika eneo hilo la bahari.
Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri ulitanguliwa na Mkutano wa 22 wa Kamati ya Makatibu Wakuu/ Maafisa waandamizi wa Jumuiya ya IORA uliofanyika tarehe 15 – 17 Desemba, 2020.
Thursday, December 17, 2020
HABARI KTK PICHA ZIARA YA WAWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI NCHINI TANZANIA
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akielezea juu ya ziara
ya wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Uturuki katika studio za Radio Uhuru (Uhuru
FM) Leo Jijini Dar es Salaam |
Tuesday, December 15, 2020
WAWEKEZAJI KUTOKA UTURUKI WAWASILI TANZANIA KUWEKEZA
Wawekezaji kutoka nchini Uturuki wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji na biashara zilizopo nchini ili waweze kuwekeza na kukuza Diplomasia ya Uchumi baina ya mataifa hayo.
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo amethibisha kuwasili
kwa wawekezaji hao wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass
Partners" leo jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa wawekezaji watano kati
ya kumi wamefika nchini na kujumika na waturuki wengine wanaofanya biashara zao
hapa nchini.
"Wawekezaji
hawa kutoka Uturuki wamekuja na wamefungua taasisi yao inayojulikana kwa jina
la "Compass Partners" ili kuendeleza biashara na tunaamini kwa
kutekeleza biashara hii tunaenda kuendeleza uchumi wa Tanzania na kutengeneza
ajira kwa watanzania," Amesema Prof. Kiondo
Prof.
Kiondo ameongeza kuwa, hatua ya kwanza wawekezaji hao wameleta bidhaa mbalimbali
ili watanzania wazione, hatua ya pili itakuwa ni uwekezaji wa kiwanda hapa
nchini kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa bidhaa ambazo zitauzwa hapa nchini.
Aidha,
kwa upande wa bidha zinazozalishwa hapa nchini ambazo zina fursa ya kuuzwa
Uturuki ni pamoja na chai, pamba, tumbaku na kahawa bidhaa hizi zote zina soko
kubwa sana nchini Uturuki.
Tunazalisha
tani 350,000 za pamba lakini tunaweza kuchakata asilimia 15 tu, hivyo tumepata
tayari mwekezaji ambaye atawekeza katika kiwanda cha nguo mkonani simiyu ili
kuongeza thamani ya bidhaa ya pamba hapa nchini.
Balozi,
Prof. Kiondo ametoa wito kwa Watanzania kuanza kuchangamkia fursa hizo za
biashara ili waweze kuongeza kipato na kuongeza biashara zao.
Kwa
upande wake, Kaimu Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah amesema kuwa biashara
kati ya Tanzania na Uturiki imekuwa ikiimarika kila wakati kwani Tanzania ni
sehemu salama ya kuwekeza na kufanya biashara.
"Kupitia
uwekezaji katika sekta mbalimbali ni imani yangu kuwa tutaendelea kukuza na
kuimarisha uhusiano wetu wa kidiplomasia," Amesema Mhe. Yah
Aidha,
amewataka Waturuki na Watanzania kutumia fursa za biashara zinazopatikana baina
ya mataifa hayo ili kufanya biashara na kukuza uchumi wao.
Ushirikiano
wa Tanzania na Uturuki ni wa muda mrefu, pamoja na mambo mengine uhusiano huo
umekuwa ukijikita zaidi katika kuendeleza uwekezaji wa viwanda, elimu na utalii
hasa katika kutangaza vivutio vya utalii vya Tanzania nchini Uturuki.
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akiongea na wanahabari
(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass
Partners" leo jijini Dar es Salaam
Kaimu
Balozi wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah akiongea na wanahabari (hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa Taasisi ya Waturiki "Compass Partners"
leo jijini Dar es Salaam
Balozi
wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo pamoja na Kaimu Balozi
wa Uturiki hapa Nchini, Mhe. Onur Yah wakikata utepe wakati wa uzinduzi wa
Taasisi ya Waturiki "Compass Partners" leo jijini Dar es Salaam
WAZIRI KABUDI AHIMIZA USHIRIKIANO MIONGONI MWA NCHI ZA OACPS
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Makutano wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Caribbean na Pacific (OACPS). |
Monday, December 14, 2020
UBALOZI WA TANZANIA NCHINI QATAR WAANZISHA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WATANZANIA WANAOAJIRIWA NCHINI HUMO
Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar umeanzisha rasmi programu ya mafunzo kwa waajiriwa wapya kutoka Tanzania wanaokwenda kufanya kazi nchini humo.
Mafunzo yakiendelea kwa Mabinti hao |
Mabinti tisa kutoka Tanzania walioshirki mafunzo ya kuwajengea uwezo yaliyoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini Qatar |
Saturday, December 12, 2020
TANZANIA, PAKISTAN ZASAINI MIKATABA YA MAKUBALIANO YA KIDIPLOMASIA
Tanzania
na Pakistan zimetiliana saini mikataba miwili ya makubaliano ambayo ni mkataba
wa mashaurino ya kidiplomasia pamoja na mkataba wa kuanzisha tume ya pamoja ya
ushirikiano wa kiuchumi.
Mikataba
hiyo imesainiwa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri wa mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi pamoja na Balozi
wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem.
Waziri
wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) amesema kuwa makubaliano hayo yanatoa fursa nyingi zilizopo za
kuongeza na kukuza biashara kati ya Tanzania na Pakistan hasa katika sekta ya
kilimo ikiwemo chai, pamba, korosho, mbegu za mafuta, Madini ya Tanzanite,
pamoja na uwekezaji.
"Tanzania
na Pakistan zina uhusiano wa muda mrefu na katika mazungumzo yetu ya leo,
Balozi wa Pakistan ameeleza fursa zilizopo Pakistan ambapo fursa hizo
zikitumiwa vizuri zitanufaisha mataifa yote mawili," Amesema Prof. Kabudi
Prof.
Kabudi ameongeza kuwa makubaliano hayo ni kielelezo kingine cha uhusiano mzuri
uliopo baina ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Pakistan na kwamba fursa
hizo zitaendelea kuongeze ushirikiano wa diplomasia ya uchumi baina ya Tanzania
na Pakistan.
Kwa
Upande wake Balozi wa Pakistani hapa nchini, Mhe. Mohammad Saleem amesema kuwa
kusainiwa kwa mikataba hiyo muhimu itasaidia kukuza na kuendeleza diplomasia ya
Uchumi baina ya Tanzania na Pakistan.
"Ni
imani yangu kuwa kusainiwa kwa mikataba hii miwili ya makubaliano baina ya
Serikali ya Tanzania na Pakistan kutasaidia kudumisha na kukuza uchumi kati ya
mataifa yetu," Amesema Balozi Saleem
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi akiangalia baadhi ya nyaraka alizokabidhiwa na Balozi wa Pakistani
nchini, Mhe. Mohammad Saleem katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi pamoja na Balozi wa Pakistani nchini, Mhe. Mohammad Saleem wakisaini
mikataba ya makubaliano katika Ofisi ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Friday, December 11, 2020
TZ YAHIMIZA MATAIFA MAKUBWA KUENDELEA KUZIFUTIA MADENI NCHI ZA OACPS
Tanzania imeendelea
kuhimiza umuhimu wa mataifa makubwa kuzifutia madeni nchi za Jumuiya ya nchi za
Afrika, Caribbean na Pasifiki (OACPS) zilizoathiri na janga la COVID-19 pamoja
na kuyataka mataifa hayo kuhakikisha kwamba chanjo ya COVID-19 itakayopatikana
inazifikia nchi zote za Jumuiya hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) ambaye pia ni Rais wa Baraza la Mawaziri la OACPS wakati
alipokuwa anawasilisha hotuba yake katika Mkutano wa 39 wa Bunge la pamoja
baina ya nchi za ACP na EU na Mkutano wa 111 wa Baraza la Mawaziri kutoka nchi
za Jumuiya ya OACPS uliofanyika jana kwa njia ya Mtandao (Video Conference) jijini
Dar es Salaam.
"Kutokana na jukumu
langu kama Rais wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya OACPS nimehutubia kwa njia
ya video Bunge la pamoja la Ulaya na ACP (ACP-EU Joint Parliamentary Assembly).
Katika hotuba yangu nimehimiza umuhimu wa mataifa makubwa kuendelea kuzifutia
madeni nchi za OACPS zilizoathiri na janga la COVID-19, pamoja na kuyataka
mataifa hayo kuhakikisha kwamba chanjo ya COVID-19 itakayopatikana inazifikia
nchi zote za Jumuiya yetu ya OACPS," Amesema Prof. Kabudi
Halikadhalika, Prof. Kabudi
ameelezea hatua iliyofikiwa na nchi za OACPS ikiwemo Tanzania katika kujenga
democrasia, uchumi, biashara na maendeleo ya watu ikiwemo suala la kulinda na
kuheshimu haki za binadamu. Aidha, aliwajulisha juu ya changamoto zinazozikabili nchi za OACPS katika
kutimiza adhma yao ya maendeleo, ikiwemo janga la ugonjwa wa COVID -19,
mabadiliko ya tabia nchi, ugumu wa kuyafikia masoko ya ulaya, masuala ya amani
na usalama ikiwemo suala la wakimbizi.
Kwa upande wake Waziri wa
Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani, Dkt. Gerd Muller, ambaye pia ni Raisi wa
Baraza la Mawaziri la Umoja wa Ulaya alimhakikishia
Prof. Kabudi kuwa Umoja wa Ulaya (EU) utaendeleza ushirikiano wake na nchi za
OACPS katika kuhakikisha kuwa uchumi wa Jumuiya hiyo unazidi kuimarika.
"Naomba kutumia fursa
hii kukuhakikishia kuwa sisi ka EU tupo tayari kushikamana na Jumuiya ya OACPS
kuimarisha uhusiano wetu kiuchumi, kisiasa, kidiplomasia lakini pia kulinda na
kuapa kipaumbele masuala yote yanayohusu haki za binadamu," Amesema Dkt.
Muller.
Mbali na Dkt. Muller
wengine waliohutubia katika mkutano huo ni pamoja na Jutta Urpilanen, Kamishna
wa Ubia wa Kimataifa kutoka EU ambaye nae pia alisisitiza kuendeleza mshikamano
baina ya nchi za EU na OACPS.
Katika hatua nyigine, Prof.
Kabudi ameeleza kuwa kumalizika kwa mkutano wa 39 wa Bunge la pamoja baina ya
nchi za ACP na EU kumetoa fursa ya kufanyika kwa mkutano wa wa Baraza la
Mawaziri wa nchi za OACPS unaotegemewa kuanza kufanyika kwa njia ya mtandao
(Video Conference) kuanzia tarehe 13 hadi 17.
Prof. Kabudi ameongeza kuwa
katika mkutano huo, masuala muhimu yatakayo jadiliwa ni pamoja na Mapambano
dhidi ya ugonjwa Corona, majadiliano ya mkataba mpya wa ubia mpya baina ya nchi
za OACPS na Umoja wa Ulaya, Mageuzi (reforms) ndani ya Sekretariati ya OACPS, kusimamia
kusainiwa kwa Mkataba ulioboreshwa wa Georgetown (the Revised Georgetown
Agreement) na nchi za OACPS pamoja na Mikakati ya kufanya shughuli za Jumuiya
ziguse zaidi Maisha ya wananchi.
Itakumbukwa kuwa Agosti 1,
2020 Tanzania ilikabidhiwa jukumu la kuongoza Jumuiya ya nchi za Afrika,
Caribbean na Pasifiki (OACPS) kwa ngazi ya Mawaziri na kwa ngazi ya balozi
Brussels.
Jukumu hilo ni heshima
kubwa kwa Tanzania na ni ishara ya wazi ya jumuiya ya kimataifa kutambua kazi
kubwa anayofanya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli ndani ya nchi na hivyo kutamani pia ushawishi wake huo uwe katika
ngazi ya kimataifa hususan katika jumuiyan hii ya OACPS.
Hii ni mara ya tatu
Tanzania kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa
Jumuiya hii tangu ilipoanzishwa mwaka 1975. Tanzania ilikuwa Mwenyekiti mwaka
1992 na mwaka 2014. Chini ya Uongozi wa Tanzania vipaumbele vikuu ni pamoja na
kupambana na ugonjwa wa corona na athari zake, kusimamia kukamilishaji wa
majadiliano ya mkataba mpya wa ubia kati yan chi za OACPS na Umoja wa
Ulaya, kusimamia mageuzi makubwa ndani
ya Jumuiya ya OACPS ili iendane na wakati na kuelekeza rasilimali zake kwenye
maeneo muhimu yenye tija kwa wanachama.
Aidha, Tanzania pia imelenga kuimarishaji
ushiriano miaongoni mwa nchi za OACPS (Connectivity) na kufanya mashauriano na
wabia wetu wengine wa maendeleo ukiwemo Umoja wa Ulaya katika kuweka mifumo
mizuri zaidi ya kuimarisha biashara, ongezeko la thamani ya mazao ya kilimo,
matumizi ya digitali na fursa zaidi za masoko.
Thursday, December 10, 2020
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE ALA KIAPO CHA UTII BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI
Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Tate Olenasha, ameapa kiapo cha Utii cha Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki
Mhe. Olenasha
ameapa kiapo hicho na kushuhudiwa na Spika wa Bunge la Jumuiya ya Afrika
Mashariki, Mhe. Martin Ngoga pamoja na wabunge wengine wanaounda Bunge hilo ili
kumwezesha kushiriki kwenye Bunge hilo kama Naibu Waziri anayeshughulikia
masuala ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe. Olenasha
ameapa kiapo hicho akiwa katika Ofisi za Wizara zilizopo kwenye Mji wa
Serikali, Mtumba jijini Dodoma wakati wa kikao kilichofanyika kwa njia ya
mtandao tarehe 10 Desemba 2020.
Aidha, kikao
hicho kimehudhuriwa na Wabunge wa Bunge hilo ambao wengi wameshiriki kutokea
kwenye nchi zao wakati Mhe. Spika akiwa Makao Makuu ya Bunge hilo jijini
Arusha.
Kikao hicho,
pamoja na mambo mengine kimejadili Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge la
Afrika Mashariki ya Masuala Mtambuka
Mbunge wa
Bunge la Afrika Mashariki kutoka Tanzania, Mhe. Josephine Sebastian Lemoyan
akimtambulisha Mhe. Olenasha kwenye Bunge hilo kama Mjumbe mpya |
Mhe. Olenasha
akisaini Hati ya Kiapo baada ya kula kiapo cha utaii cha kushiriki Bunge la
Afrika Mashariki |
Mhe. Olenasha
kwa pamoja na Mhe. Josephine wakifuatilia mjadala uliokuwa ukiendelea wakati wa
kikao cha Bunge la EALA |
Naibu Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Olenasha akichangia
jambo wakati wa kikao
|