Na Mwandishi wetu, Dar
Kampuni
ya Madini ya Anglogold Ashanti ya Afrika Kusini imeahidi kuendeleza ushirikiano
na Serikali ya Tanzania katika sekta ya madini na kuhakikisha kuwa sekta hiyo
inakuwa mstari wa mbele kuchangia uchumi.
Ahadi
hiyo imetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti – Afrika, Bw. Sicelo
Ntuli wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) leo Jijini
Dar es Salaam.
Akiongea
mara baada ya mazungumzo hayo Balozi Mulamula amesema kuwa, Anglogold Ashanti
ni wadau wakubwa katika sekta ya madini na wameonesha utayari wao wa kushirikiana
kwa karibu na Serikali katika kukuza na kuendeleza sekta ya madini.
“Leo
hii nimekutana na uongozi wa Kampuni ya Madini ya Angogold Ashanti na
tumejadili pamoja na mambo mengine, utayari wa Kampuni hiyo kushirikiana na
Serikali katika kukuza sekta ya madini hapa nchini,” Amesema Balozi Mulamula
Balozi
Mulamula ameongeza kuwa kitendo cha kukutana na wadau wa madini kama Anglogold
Ashanti na kujadiliana nao masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kukuza sekta ya
madini ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi.
Kwa
Upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti Bw. Ntuli amesema kuwa
uongozi wa Anglogold umefarijika kukutana na Mhe. Waziri wa Mambo ya Nje na
kuweza kujadiliana nae mambo mbalimbali ikiwemo suala la kukuza ushirikiano
baina ya Kampuni hiyo na Serikali ya Tanzania.
“Sisi
kama Anglogold tumefarijika kuona Serikali ya Tanzania ipo tayari kuendeleza
ushirikiano na Sisi…….tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu kwa maslahi mapana
ya pande zote mbili,” Amesema Bw. Ntuli
Aprili 16, 2021 Kampuni ya Anglogold Ashanti iliingia ubia na Kampuni ya BG Umoja ya nchini Tanzania kwa ajili ya kuchimba madini katika miradi ya Nyankanga na Geita Hill. Anglogold ni Kampuni mama ya Geita Gold Mine (GGML) imeipatia BG Umoja mkataba wenye thamani ya Dola za Marekani Milioni 186 kwa miaka miwili.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akizungumza na Afisa Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti – Afrika,
Bw. Sicelo Ntuli wakati walipokutana kwa mazungumzo leo jijini Dar es Salaam
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Anglogold Ashanti – Afrika, Bw. Sicelo Ntuli akimueleza jambo Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika leo jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata
Mulamula (Mb) akiongoza kikao chake na Kampuni ya Madini ya Anglogold Ashanti
ya Afrika Kusini kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.