Monday, December 13, 2021

UZINDUZI WA MATANGAZO YA VIVUTIO VYA UTALII KATIKA MABASI NCHINI ISRAEL

Katika kuhitimisha maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Mhe. Job Daudi Masima, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Israel amezindua matangazo ya vivutio vya utalii katika mabasi ya abiria yanayofanya safari zake kati ya jiji la Tel Aviv na miji ya jirani, katika stendi kuu ya mabasi, katika kitongoji cha Petach Tikva. Matangazo hayo yamebandikwa kwenye mabasi yapatayo 125 kwa muda wa wiki tatu kuanzia tarehe  10 - 31 Disemba 2021. Matangazo hayo yanayoonesha Mlima Kilimanjaro; Wanyama katika hifadhi ya Serengeti; Ngorongoro na fukwe za Zanzibar yanatoa fursa kwa wakazi wa Israel kujionea vivutio hivyo na kuhamasika kutembelea Tanzania mara baada ya masharti ya UVIKO kulegezwa.
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima akikata  utepe kuashiria uzinduzi wa matangazo ya vivutio vya utalii vya Tanzania katika mabasi ya abiria nchini Israel.
Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima akionesha tangazo kwenye basi linalohusu fukwe za Zanzibar likisomeka "Zanzibar -  Splendid Unspoiled White Sand Beaches"
Tangazo kwenye basi linalohusu Mlima Kilimanjaro likisomeka "Glorious Mt. Kilimanjaro - The roof of Africa only in Tanzania"

Tangazo kwenye basi linalohusu Ngorongoro likisomeka "Magnificent Ngorongoro Crater- World's wildest Nature"
Tangazo kwenye basi linalohusu Serengeti likisomeka "Outstanding Serengeti Wildlife- The Largest Wild Migration in the World"

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.