Wednesday, May 9, 2012

Msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi




Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa msimamo wa Tanzania kuhusu suala la Sahara Magharibi na Morocco, wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.  
 

Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa msimamo wa Tanzania kuhusu suala la Sahara Magharibi na Morocco, wakati akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB), akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Mambo ya Nje leo jijini Dar es Salaam.  Mwingine pichani ni Bw. Assah Mwambene, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali -Wizarani.
 
 
 
 
Msimamo wa Tanzania kuhusu Sahara Magharibi
 
Tanzania imesema haijabadili msimamo wake katika kuwaunga mkono Watu wa Sahara Magharibi kuhusu haki yao ya kujitawala kutoka mikononi mwa Morocco.

Hayo yalisemwa na Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati akiongea na Waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari leo jijini Dar es Salaam.

Aidha, Tanzania imeisihi Morocco irudi katika uanachama wa Umoja wa Afrika ili kuweza kuwa na mazungumzo ya pamoja baina yao, wananchi wa Sahara Magharibi na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kutafuta suluhu ya kudumu kuhusu mgogoro huo.

“Tatizo hilo limekuwa kidonda ndugu haliwezi kupona kesho, kwa hiyo msimamo wa Tanzania ni huo. Tunataka kuwe na uhuru wa Sahara Magharibi na tunaomba pande zote, pamoja na Umoja wa Mataifa wamalize kwa haraka sana tatizo hili ili kuwe na kura ya maoni ya wananchi wenyewe kuamua ama kujitawala au kuwa sehemu ya Morocco,” alisema Mhe. Membe.

Mhe. Membe aliongeza kuwa, Tanzania itaheshimu maamuzi yoyote ya wananchi wa Sahara Magharibi kwa vile “tunaamini wataamua kujitawala wenyewe na siyo kuwa kama kile Kisiwa cha Mayote nchini Comoro”.  Wananchi wa Kisiwa hicho waliamua kuwa sehemu ya nchi ya Ufaransa, ingawa kipo Afrika.

Kuhusu tatizo la kumpata Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mhe. Membe alisema Tanzania inaungana na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kumuunga mkono mgombea kutoka Afrika Kusini kwenye nafasi hiyo Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma dhidi ya mgombea anayetetea uenyekiti huo, Bw. Jean Ping.

Nchi Wanachama wa AU zinatarajiwa kupiga kura na hatimaye kumchagua Mwenyekiti wa Kamisheni hiyo mwezi wa Julai mwaka huu wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi mjini Lilongwe, nchini Malawi. 






Tuesday, May 8, 2012

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB), atafanya mazungumzo na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano Wizarani tarehe 09 Mei, 2012 kuanzia saa tano asubuhi.

Masuala atakayozungumzia ni pamoja na kampeni za mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Bi. Nkosazana Dlamini-Zuma, anayeungwa mkono na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Imetolewa na,

KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI,
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA,
DAR ES SALAAM.

08 MEI, 2012

Sunday, April 29, 2012

Wakuu wa Nchi wa EAC wasaini Itifaki ya Mkataba wa masuala ya Ulinzi



Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete (wa pili kushoto), akiwa na viongozi wenzake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakitia saini Mkataba wa makubaliano ya ushirikiano katika ulinzi.  Sherehe hiyo ilifanyika Ngurdoto Lodge tarehe 28 Aprili, 2012.  (picha na Ikulu)

Na ROSEMARY MALALE, Arusha
28 Aprili, 2012
Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wameridhia na kusaini Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya Ushirikiano katika masuala ya Ulinzi na kuelekeza kuanza mara moja kwa  majadiliano ya pamoja yatakayopelekea kukamilika kwa Mkataba wa Pamoja katika masuala ya Ulinzi.
Aidha, mbali na kutia saini Itifaki hiyo Wakuu hao wa Nchi waliipokea ripoti iliyowasilishwa kwao na Baraza la Mawaziri na kuridhia masuala mbalimbali katika ripoti hiyo ikiwa ni pamoja na kumteua Bi. Jesca Eriyo, kutoka Uganda kuwa Naibu Katibu Mkuu mpya  kufuatia aliyekuwepo Bibi Beartice Kiraso kumaliza muda wake wa kazi katika Jumuiya.
Vilevile Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo waliridhia pendekezo la kumuongezea mkataba wa miaka  mingine mitatu  Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bw. Jean Clausde Nsengiyumva kutoka Burundi.
Kuhusu maombi ya Sudan Kusini ya kuwa Mwanachama wa Jumuiya hiyo, wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubali mapendekezo ya Baraza la Mawaziri ya kuundwa kwa Timu ya Uhakiki itakayohusisha wataalam watatu kutoka kila nchi mwanachama na Wataalam watatu kutoka katika Sekretarieti ya Jumuiya hiyo kwa ajili ya kuwezesha zoezi hilo.
Timu hiyo ya uhakiki, pamoja na mambo mengine itapitia maombi ya nchi hiyo na kuona kama yanakidhi Vigezo vya Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki ili kuwa mwanachama. Vigezo hivyo ni pamoja na masuala ya kijiografia yaani kama nchi ya Sudan Kusini inapakana au ipo karibu na mojawapo ya nchi mwanachama wa jumuiya hiyo;   nchi kuzingatia kanuni na misingi ya kimataifa ya demokrasia, utawala wa sheria, kuheshimu haki za binadamu, utawala bora na mchango wan chi katika kuimarisha ushirikiano ndani ya Jumuiya.
Wakuu hao wan chi pia walizungumzia masuala ya usalama katika kanda ya Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na mgogoro unaoendelea baina ya Sudan na Sudan Kusini na kuzitaka nchi hizo kurudi kwenye meza ya mazungumzo kumaliza tofauti zao.
Awali akifungua mkutano huo, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Tanzania na mwenyeji wa mkutano aliwakaribisha nchini marais na viongozi mbalimbali kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kueleza kuwa ni imani yake kuwa mkutano huo utakuwa ni wa mafanikio makubwa kwa manufaa ya wananchi wa Afrika Mashariki kwa ujumla.
“Sitapenda kuchukua muda mwingi kuzungumza siku ya leo bali nawakaribisha sana Tanzania na hasa hapa Arusha na ni imani yangu kuwa mkutano huu utakuwa wa mafanikio na manufaa kwa wananchi wa Jumuiya hii,” alisema Mhe. Kikwete.
Aidha, katika hotuba yake Mhe. Mwai Kibaki, Rais wa Kenya  ambaye pia ni Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo alieleza kuwa kuna umuhimu kwa nchi wanachama kuimarisha na kuwa na mtandao wa pamoja  wa miundombinu ili kukuza biashara na uchumi kwa ujumla.
Mkutano huo Maalum wa 10 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifanyika mjini Arusha tarehe 28 Aprili, 2012 na kuhudhuriwa na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Tanzania, Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Uganda, Mhe. Mwai Kibaki, Rais wa Kenya na Mhe. Paul Kagame, Rais wa Rwanda.
Wengine ni Mhe. Therence Sinunguruza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mawaziri, Makatibu Wakuu, Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini na wadau mbalimbali.

-Mwisho-

Saturday, April 28, 2012

World Leaders congratulate President Kikwete


Leaders from different parts of the world have continued to congratulate H.E. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania upon marking 48th Anniversary of the Union between Tanganyika and Zanzibar on April 26, 2012.

H.E. Kim Yong Nam, the President of the Presidium of the Supreme People’s Assembly of the Democratic People’s Republic of Korea said the government and people of Tanzania have achieved a greater success in the work for national unity and economic development.

"I take this opportunity to wish you greater success in your and your people’s efforts for development and prosperity of the country,” he said.

On his part, the President of the French Republic, Mr. Nicolas Sarkozy said his country shares the international commitment of Tanzania in favor of democracy, good governance and development, and appreciates Tanzania contribution to the peace and strengthening regional integration in Africa.

"I am delighted about the presence of the United Republic of Tanzania in the Peace and Security Council of the African Union, and tanzania's readness in furthering dialogue on regional security issues between our two countries.”

The President of the Republic of Turkey, H.E. Abdullah Gϋl, told the Tanzanian President that his country cherishes the achievement attained so far saying he was confident that Tanzania will remain determined to stay the course for development and enhancing bilateral ties between the two countries.”

H.E. Mr. Truong Tan Sang, the President of Vietnam said Tanzanians under the able leadership of President Kikwete have managed to attain a tremendous achievements while maintaining peace and unity of its people.

President of the Islamic Republic of Pakistan, H.E. Mr. Asif Ali Zardari, said Pakistan and Tanzania have historically maintained and nurtured very close, cordial and cooperation relations in diverse fields and called for a sustained and continued progress of the people and economic development of Tanzania.

President Kikwete also received the goodwill messages from Sultan of Oman, the Republic of Benin, Mexico and Hellenic Republic of Greece.

Issued by:

THE MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION,

DAR ES SALAAM

APRIL 28, 2012

Friday, April 27, 2012

Rais Kibaki ahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa EAC




Rais wa Kenya, Mhe. Mwai Kibaki, akipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB), mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mjini Arusha jana.  Rais Kibaki anahudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika leo tarehe 28 Aprili 2012.



Rais Kibaki wa Kenya, akitumbuizwa na burudani ya ngoma mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) jana mjini Arusha.


Rais Kibaki wa Kenya (katikati), akiwa na wenyeji wake Mhe. Membe (kulia) na Mhe. Samuel Sitta (kushoto), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mara baada ya kuwasili jana mjini Arusha.



Thursday, April 26, 2012

MKUTANO WA BARAZA LA MAWAZIRI WA EAC


Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (wa katikati mstari wa mbele) akiwa na Mhe. Hussein Mwinyi (Mb.), Waziri wa Ulinzi pamoja na Mhe. Harrison Mwakyembe (Mb.), Naibu Waziri wa Ujenzi kwenye moja ya vikao vya majadiliano vya ujumbe wa Tanzania kabla ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Arusha tarehe 25 Aprili, 2012. (Picha na Wizara ya Mambo ya Nje).


Mabalozi wa Tanzania katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika moja ya vikao vya majadiliano wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana mjini Arusha. Kutoka kushoto ni Dkt. Batilda Buriani, Balozi wa Tanzania, Kenya, Mhe. Marwa Matiko, Balozi wa Tanzania, Rwanda, Mhe. James Nzagi, Balozi wa Tanzania, burundi na Mhe. Dkt. Ladislaus Komba, Balozi wa Tanzania, Uganda.


Mhe. Samwel Sitta, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara yake, Dkt. Stergomena Tax-Bamwenda akiongoza moja ya vikao vya majadiliano vya ujumbe wa Tanzania (haupo pichani) kabla ya Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika Arusha tarehe 25 Aprili, 2012.


Bw. John Haule, Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akibadilishana mawazo na Bw. George Masaju, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki jana mjini Arusha.


Mhe. Samwel Sitta, Waziri wa Afrika Mashariki, akiwa na baadhi ya Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakisaini Ripoti  baada ya kufikia makubaliano katika mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya hiyo uliofanyika jana mjini Arusha. 

26 Aprili, 2012
Na ROSEMARY MALALE, ARUSHA
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika mjini Arusha jana kujadili na kukubaliana agenda mbalimbali zitakazowasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya hiyo tarehe 28 Aprili, 2012.

Miongoni mwa agenda muhimu zilizojadiliwa na Mawaziri hao ni pamoja na mapendekezo ya kuteua Naibu Katibu Mkuu  mpya kutoka Uganda kufuatia aliyekuwepo Bibi Beartice Kiraso kumaliza muda wake; kuongeza mkataba wa miaka mitatu kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Bw. Jean Claude Nsengiyumva kutoka Burundi; kupitia ripoti kuhusu maombi ya Jamhuri ya Sudan Kusini ya kuwa mwanachama wa Jumuiya na kupitia Mswada wa sheria ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu uangalizi wa uzito wa mizigo inayobebwa na magari ili kulinda barabara za nchi wanachama zisiharibiwe.
Masuala mengine yaliyojadiliwa ni Rasimu ya Itifaki ya Kupambana na Rushwa kwa nchi wanachama; Rasimu ya Itifaki ya Ushirikiano katika masuala ya Ulinzi na ripoti ya Kamati ya Fedha na Utawala.
Awali akifungua Mkutano huo wa Baraza la Mawaziri, Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt. Richard Sezibera aliwaomba Mawaziri watoe maoni yao kuhusu agenda hizo ili baadae zifikishwe na kuridhiwa na Wakuu wa Nchi.
Mkutano huo wa Mawaziri ulitanguliwa na vikao vya Maafisa Waandamizi kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 20-22 Aprili kikifuatiwa na kikao cha Kamati ya Uratibu chini ya Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama kilichofanyika tarehe 23 na 24 Aprili, 2012.
Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo  uliongozwa na Mhe. Samwel Sitta (Mb), Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki na kuwahusisha pia Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb), Waziri wa Ulinzi, Mhe. Perreira Ame Silima (Mb), Naibu Waziri wa Fedha na Mhe. Harrison Mwakyembe (Mb), Naibu Waziri wa Ujenzi.
Wengine ni Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. George Masaju, Dkt. Stergomena Tax-Bamwenda, Katibu Mkuu wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Mambo ya  Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Herbert Mrango, Katibu Mkuu wa Ujenzi, Bw. Job Masima, Katibu Mkuu wa Ulinzi, Mabalozi wa Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi na Maafisa Waandamizi  kutoka Serikalini.
Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki utafanyika mjini hapa tarehe 28 Aprili, 2012.

Tuesday, April 24, 2012

Balozi Mteule wa Rwanda awasilisha Nakala za Hati za Utambulisho


Balozi Mteule wa Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi, akimkabidhi nakala za hati za utambulisho Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB), leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam. (Picha na Tagie Daisy Mwakawago).


Mhe. Membe akiongea na Mhe. Dkt. Rugangazi, Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini.


Mhe. Dkt. Benjamin M. Rugangazi, Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini akizungumza jambo baada ya kuwakilisha nakala za hati za utambulisho kwa Mhe. Bernard K. Membe (MB), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.




 
Na ROSEMARY MALALE

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (Mb) amemhakikishia ushirikiano Balozi Mteule wa Rwanda hapa nchini, Dkt. Benjamin Rugangazi alipofika ofisini kwake kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho leo.

Akizungumza na Balozi huyo, Mhe. Membe alimkaribisha nchini na kusema kuwa Tanzania na Rwanda zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na kwamba anafurahi na anamkaribisha wakati wowote ofisini kwake kwa majadiliano kuhusu kuimarisha na kukuza ushirikiano huo.

“Nimefurahi Balozi upo hapa nchini tayari, Tanzania ni nchi nzuri ya kirafiki na utafurahia kuwa Tanzania. Ninakukaribisha wakati wowote utakapohitaji kuwasiliana na na mimi kwa mashauriano,” alisema Mhe. Membe.

Kwa upande wake Balozi huyo Mteule alimshukuru Mhe. Membe na kueleza kuwa Rwanda na Tanzania zimeendelea kushirikiana kama ndugu kwa muda mrefu na kwamba atashirikiana na Wizara na Watumishi kwa ujumla kwa karibu.






Rais Kikwete ahudhuria mazishi ya Rais Bingu wa Mutharika nchini Malawi



 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za rambirambi kwenye kaburi la aliyekuwa Rais wa Malawi, Prof. Bingu wa Mutharika


 




Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa aliyekuwa Rais wa Malawi marehemu Prof. Bingu wa Mutharika, kijijini Ndata, wilayani Thyolo, nje ya jiji la Blantyre, nchini Malawi jana.  Pembeni yake ni Mhe. Waziri Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mjane wa aliyekuwa Rais wa Malawi, marehemu Bingu wa Mutharika, Bi. Calista Mutharika wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika kijijini Ndata, katika mji wa Blantyre, Malawi tarehe 23 Aprili, 2012.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionge na Rais wa Malawi, Bi. Joyce Banda, wakati wa mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Prof. Bingu wa Mutharika aliyefarika April 6 mwaka huu.  Mazishi hayo yalifanyika tarehe 23 Aprili, 2012 kijijini Ndata, wilayani Thyolo, katika mji wa Blantyre, Malawi.

Picha zote na:  FREDDY MARO, IKULU

Thursday, April 19, 2012

Relief food to Somalia to be shipped soon, says minister

About 3000 tonnes of relief food to hunger-stricken Horn of Africa will be dispatched on the designated place as soon as the South African ship under SADC flag docks at the Dar es Salaam Harbour.

Foreign Affairs and International Cooperation Minister Bernard Membe told the National Assembly in Dodoma yesterday that the vessel would deliver all consignments of relief food pledged by the members of the SOuthern African Development Cooperation.

"The ship is expected in Dar es Salaam anytime now," said the minister, attributing the delay in shipment to, insecurity off the Somalia Coast in the Indian Ocean.

He ruled out any further delay as security situation in the region had improved tremendeously of late.  He added that the government also pledged 200,000 US Dollars to the war and hunger ravaged Somalia.

The minister was reacting to Chambani Member of Parliament (CUF) Salim Hemed Khamis who had sought to know how the government was living up to the Africa Union's slogan "One Africa One Vote Against Hunger" adopted last year, requiring African countries to come to the rescue of the troubled region.

The AU had observed that food insecurity remained at emergency levels across parts of the Horn of Africa, with famine declared in two regions of Southern Somalia and humanitarian organizations struggled to cope with the influx of Somalia refugees in Ethiopia and Kenya.

Mr. Membe said the AU members during their special meeting in Addis Ababa, Ethiopia last August pledged 350m US Dollars for the cause.

He however, observed that as of February of this year, it emerged that some 1 bn US Dollars was needed to address the situation.

Quoting United Nations statistics, the minister said the disaster affected more than 12 million people, and deaths associated with famine reached an average of six people (five children and one adult) daily last year.

Source:  Daily News, Tanzania

Wednesday, April 18, 2012

Rais Kikwete akiwa katika ziara ya kikazi ya siku tano nchini Brazil

   


Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia katika mkutano wa Open Government Partnership, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil tarehe 17 Aprili 2012.  


  
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Waziri Mkuu wa Georgie Mh Nika Gilauri katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,baada ya kuhudhuria mkutano wa Open Government Partnership.  Wengine kwenye picha ni Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb) (wa tatu kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.



Ujumbe wa Tanzania ukibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil.  Kutoka kushoto ni Waziri katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Mathias Chikawe, Waziri wa Kazi na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika wa Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Mahadhi Juma Maalim na Mshauri wa Rais (Masuala ya Siasa) Dkt Laurian Ndumbaro.



Ujumbe wa Tanzania, akiwemo Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Mshauri Mkuu Mwandamizi wa Rais katika masuala ya kidiplomasia, wakiwa kwenye mkutano wa Open Government Partnership katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil. 



Wajumbe wa Tanzania, akiwemo Bi. Grace Shangali (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Europe na America kwenye Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pamoja na Wajumbe wengine kutoka taasisi mbalimbali za kiraia na serikali wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Brasilia Convention Centre jijini Brasilia, Brazil,wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Open Government Partnership.


Picha zote na maelezo -   http://www.ikulublog.com/



Monday, April 16, 2012

Mhe. Membe aongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa CMAG mjini London




Mhe. Bernard K. Membe (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiongea jambo na Mhe. Surujrattan Rambachan (katikati), Waziri wa Mambo ya Nje wa Trinidad and Tobago ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mkutano wa Kikosi Kazi cha Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Ministerial Action Group - CMAG), na Mhe. Bob Carr, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CMAG.  Mkutano huo ulifanyika katika Malborough House, mjini London tarehe 16 April, 2012.


Mhe. Membe, ambaye aliongoza Ujumbe wa Tanzania, akiwa katika Chumba cha Mkutano wa CMAG.  Wengineo katika picha ni wajumbe kutoka Tanzania, akiwemo Bi. Dora Msechu (wa pili kulia), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.  Tanzania ni mojawapo ya nchi mwanachama wa CMAG, zikiwemo nchi za Australia, Bangladesh, Canada, Jamaica, Maldives, Sierra Leone, Trinidad and Tobago na Vanuatu.



Mhe. Membe akiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Bob Carr, Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CMAG.

Saturday, April 14, 2012

President Kikwete sends a Condolence Message to the President of Algeria

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, the President of the United Republic of Tanzania sends a condolence message to H.E. Abdelaziz Bouteflika, the President of the People’s Democratic Republic of Algeria following the death of H.E Ahmed Ben Bella, First President of the People’s Democratic Republic of Algeria.  The message reads as follows:   

“H. E. Abdelaziz Bouteflika 
President of the People’s Democratic Republic of Algeria
ALGIERS

Your Excellency and Dear Brother,

I am deeply saddened by the sad news of the untimely death of the founding Father of your great Nation that took place on 11th April, 2012.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, and indeed on my own behalf, I wish to convey our deepest sympathies and condolences to Your Excellency and, through you, to the bereaved family and relatives as well as the Government and the entire brotherly People of Algeria for this untimely death.

Tanzania will always remember the late Ahmed Ben Bella for the important role he played in cementing the relations between our two countries that so happily exists to-date.

 He will also be remembered as a truly son of Africa who stood for unity and dignity of the African people. Africa has indeed lost one of the charismatic and revolutionary leaders who dedicated his life not only for the struggle for the independence of Algeria but also for the other African countries that were still suffering under colonialism.  He also contributed positively to the peace and stability of Africa in his capacity as the Chairperson of the Panel of the Wise of the African Union. 

At this difficult moment of agony and distress, we share your grief and pray to the Almighty God to give the bereaved family, relatives and all the people of Algeria strength and courage to endure the agony resulting from this great loss.  May the Almighty God rest the soul of the deceased in eternal peace. 

Please accept, Your Excellency and Dear Brother, the assurances of my highest consideration.

Jakaya Mrisho Kikwete
President of the United Republic of Tanzania



Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation

DAR ES SALAAM
14th April, 2012

Wednesday, April 11, 2012

UTEUZI WA MKUU WA CHUO NA MWENYEKITI WA TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA YA NELSON MANDELA‏



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS


Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal kuwa Mkuu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela.
Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam leo, Jumatano, Aprili 11, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue imesema Rais Kikwete pia amemteua Profesa David Homeli Mwakyusa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo cha chuo hicho cha Nelson Mandela.
Taarifa imesema kuwa uteuzi wa Dkt. Bilal ambaye ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Profesa Mwakyusa aliyepata kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii katika Serikali ya Rais Kikwete ulianza Alhamisi iliyopita, Aprili 5, 2012.
Chuo cha Nelson Mandela ambacho kiko Arusha ni moja ya vyuo vikuu vinne vinavyolenga kuendeleza sayansi na teknolojia katika Bara la Afrika.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
11 Aprili, 2012

Sunday, April 8, 2012

Mhe. Membe mgeni rasmi Tamasha la Pasaka

View FOTO1.JPG in slide show

Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akihutubia umati wa watu uliofika kwenye Tamasha la Pasaka lililofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Kushoto kwa Mhe. Waziri ni Mke wake Mama Dorcas Membe.


View FOTO2.JPG in slide show

Mhe. Membe (wa pili kutoka kushoto) akiwa na viongozi wa dini waliohudhuria Tamasha la Pasaka. Kutoka kushoto ni Askofu Sylivester Gamanywa wa WAPO Missions akifuatiwa na Mtume Fernandes wa Agape Missions na mwisho ni Mama Membe.
View FOTO3.JPG in slide show

Mhe. Waziri Membe akizindua albamu mpya ya nyimbo za injili iitwayo Kwa Utukufu wa Mungu ya mwimbaji wa nyimbo za injili Solomon Mukubwa kutoka Kenya wakati wa Tamasha la Pasaka.


View FOTO4.JPG in slide show

Mhe. Membe kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa na waimbaji wa nyimbo za injili waliohudhuria Tamasha la Pasaka.

View FOTO5.JPG in slide show

Mhe. Membe na Mkewe (kulia) wakiwa na Rebecca Malope mwimbaji mashuhuri wa nyimbo za injili kutoka Afrika Kusini wakati wa Tamasha la Pasaka.


View FOTO6.JPG in slide show

Baadhi ya Wabunge na Balozi Liberata Mulamula kwenye Tamasha la Pasaka.

Saturday, April 7, 2012

Kumbukumbu za Mauaji ya Kimbari ya Rwanda‏


View FOT01.JPG in slide show

Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akitoa hotuba wakati wa Maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 18 ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yaliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City.
 
View FOTO2.JPG in slide show

Mhe. Naibu Waziri akiwasha mshumaa kama ishara ya kuwakumbuka mamia ya watu waliouawa nchini Rwanda mwaka 1994.


View FOTO3.JPG in slide show

Mhe. Naibu Waziri (wa pili kutoka kushoto) akiwa pamoja na wawakilishi mbalimbali wakati wa kumbukumbu hizo. Kutoka kushoto kwa Naibu Waziri ni Bw. Alexio Musindo, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) hapa nchini anayefuata ni Bw.Lambert Sano, Kaimu Balozi wa Rwanda hapa nchini na mwisho ni Bw. Roland Amoussouga, Msemaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda (ICTR) iliyopo Arusha.


Wizara yamuaga Balozi wa Ireland nchini


View FOTO1.JPG in slide show

Mhe. Balozi Liberatta Mulamula, Msaidizi Mwandamizi wa Rais katika Masuala Diplomasia akitoa hotuba kwa niaba ya Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, wakati wa hafla fupi ya chakula cha mchana kilichoandaliwa maalum kwa ajili ya kumuaga Mhe. Lorcan Fullam, Balozi wa Ireland aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika Hoteli ya Double Tree.


View FOTO2.JPG in slide show

Balozi  Mulamula akiwa pamoja na Mhe. Fullam wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo.


View FOTO3.JPG in slide show 
  
Mhe. Lorcan Fullam, Balozi wa Ireland aliyemaliza muda wake wa kazi hapa nchini akizungumza machache wakati wa hafla ya kumuaga.
 
 
View FOTO4.JPG in slide show
 
Balozi Fullam akifurahia zawadi ya Picha ya Wanyama aliyokabidhiwa na Balozi Mulamula kama kumbukumbu ya Tanzania atakapoondoka.
 
 
View FOTO5.JPG in slide show
 
Baadhi ya Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa walioshiriki hafla ya kumuaga Balozi Fullam


Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi kwa Makamu wa Rais wa Malawi

 

RAIS KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI KWA SERIKALI YA MALAWI KUFUATIA KIFO CHA ALIYEKUWA RAIS WA NCHI HIYO HAYATI BINGU WA MUTHARIKA


Hayati Bingu wa Mutharika
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Makamu wa Rais wa Malawi, Mheshimiwa Joyce Banda kuomboleza kifo cha kiongozi wa nchi hiyo, Mheshimiwa Rais Bingu wa Mutharika.

Katika salamu zake hizo, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Banda kuwa Tanzania imepokea kwa mshtuko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha Rais Bingu wa Mutharika ambaye Rais Kikwete amemwelezea kama kiongozi wa karibu na rafiki mkubwa wa Tanzania.

Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo, “Sisi katika Tanzania tumepokea taarifa za kifo cha Rais Bingu wa Mutharika kwa mshtuko na majonzi. Alikuwa kiongozi na rafiki wa karibu wa Tanzania na rafiki yangu. Alikuwa kiongozi wa kutumainiwa miongoni mwa nchi wanachama wa Jumuia ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Bara la Afrika lote.”

Ameongeza Rais Kikwete: “ Kwa hakika, Afrika imempoteza kiongozi imara, aliyeamini katika maslahi ya Bara letu na watu wake. Siku zote tutamkumbuka kwa dhamira yake na moyo wake katika kupigania umoja, amani, utulivu na ustawi wa mataifa yetu mawili na Afrika nzima.”

Kwa niaba ya Serikali na Wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe, nakutumia wewe Mheshimiwa, familia ya marehemu na wananchi wote wa Malawi salamu za rambirambi za dhati ya mioyo yetu kufuatia kifo cha ghafla cha Mheshimiwa Rais Bingu wa Mutharika,” amesema Rais Kikwete katika salamu zake.

Mwisho.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

Tuesday, April 3, 2012

President Kikwete congratulates new President of the Republic of Senegal

Press Release

H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E.  Macky SALL, President of the Republic of Senegal, following the swearing in to the office that took place on 2nd April, 2012.  The message reads as follows:

“His Excellency Macky Sally
President of the Republic of Senegal
DAKAR

Your Excellency and Dear Brother,

I have received with great pleasure the news of your swearing in as the new President of the Republic of Senegal, following your landslide victory during  the  second  run-off  Presidential  election  that  was  held  on 25th March, 2012.

On behalf of the Government and People of the United Republic of Tanzania, I would like therefore to extend to Your Excellency our profound and heartfelt congratulations for being sworn into office to assume the Presidency of your great country.  This is a clear testimony of the confidence reposed in you and your party by the people of the Republic of Senegal.  Also, it is a clear testimony of the maturity of democracy by the people of the Republic of Senegal and thus making Senegal to be hailed as one of Africa’s model democracies.

As you embark upon your new responsibilities of that high office, I look forward to working closely with you and the Government of the Republic of Senegal to further promote the bilateral relations that so-happily exist between our two countries, for the mutual benefit of our people.

I also look forward to working closely with you in the framework of the African Union and the United Nations in our common endeavour towards achieving economic and social prosperity not only for the people of our two countries but also for the people of the continent, as a whole.

While wishing you continued good health and success in your new responsibilities, please accept, Your Excellency and Dear Brother, the assurances of my highest consideration”.

  
ISSUED BY: MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM

03RD APRIL, 2012