Monday, June 13, 2016

KATIBU MKUU AKIWA KWENYE SHEREHE ZA KUFUNGA MAFUNZO MAALUM YA JKT

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Aziz P. Mlima akikagua gwaride liliondaliwa wakati wa sherehe za kufunga mafunzo maalum ya JKT kwaajili ya watumishi 30 walioajiriwa hivi karibuni.
Mmoja wa wahitimu wa mafunzo maalum ya JKT akitoa salaam maalum ya kijeshi kwa Katibu Mkuu Dkt. Aziz P. Mlima
Katibu Mkuu  Dkt Aziz P. Mlima akimpongeza mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri zaidi wakati wa mafunzo maalum ya JKT

Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa Italia hapa nchini.

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), akimkabidhi zawadi Balozi wa Italia aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Luigi Scotto, katika hafla maalumu ya kumuaga iliyofanyika tarehe 10-06-2016, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), akimkabidhi zawadi Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa Papa hapa nchini, Balozi Francisco Montecillo Padilla. Balozi Francisco alipewa zawadi hiyo kwenye hafla maalumu ya kumuaga Balozi wa Italia hapa nchini, iliyofanyika tarehe 10-06-2016, katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

 Waziri Mahiga akifurahia jambo na Balozi Padilla na Balozi Scotto, mara tu baada ya kuwapa zawadi.

Saturday, June 11, 2016

Balozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia akutana na viongozi wakuu wa Kamisheni ya Utalii na Wanyamapori mjini Riyadh

Balozi Hemedi Iddi Mgaza akiwa Ofisini kwa Kiongozi Mkuu wa Kamisheni ya Utalii ya Saudi Arabia, Mwanamfalme HRH Sultan bin Salman bin Abdulazizi kwenye mazungumzo ya ushirikiano.

Friday, June 10, 2016

Waziri Mahiga ashiriki maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya Kimbari ya nchini Rwanda dhidi ya Watutsi


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, maadhimisho hayo yaliandaliwa na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania na kufanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Katika hotuba yake alitoa wito kwa mataifa yote kuweka mbele suala la amani ili kuepuka kupoteza maisha ya wananchi wasio na hatia ambao ni nguvu kazi ya Taifa katika kujiletea maendeleo.

Naibu Waziri Kigwangalla ashiriki Mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na  Watoto,  Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla ( Mb) akizungumza   kwa niaba ya serikali kuhusu  mafanikio na changamoto ambazo  serikali imekuwa ikikabiliana nazo  dhidi ya  ugonjwa wa UKIMWI  katika Mkutano wa ngazi ya juu  wa Baraza Kuu la  Umoja wa  Mataifa kuhusu UKIMWI unaoendelea Umoja wa Mataifa New York-Marekani.

Waziri Mahiga ampokea Mjumbe Maalum kutoka Eritrea

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga akipokea Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Eritrea, Mhe. Isaias Afwerki kwenda kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Ujumbe huo  uliwasilishwa na Mjumbe Maalum  ambaye pia ni Balozi wa Eritrea nchini mwenye makazi Nairobi, Kenya, Mhe. Beyene  Russom Habtai.

Balozi wa Tanzania nchini Kuwait amtembelea Mkuu wa Itifaki nchini humo

Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim, Balozi wa Tanzania nchini Kuwait akiwa katika mazungumzo  na Mkuu wa Itifaki wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait, Mhe. Balozi Dhari Ajran Al-Ajran alipomtembelea Ofisini kwake kwa ajili ya kumshukuru kwa mchango wake binafsi pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje ya Kuwait katika kufanikisha juhudi za Tanzania kufungua Ubalozi wake nchini humo. Kadhalika, Mhe. Maalim alimuhakikishia Mhe. Al-Ajran utayari wa Tanzania katika kuhakikisha mahusiano baina yake na Kuwait katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii yanasonga mbele zaidi.

Thursday, June 9, 2016

Wizara ya Mambo ya Nje yafanya mkutano na Vyombo vya Habari


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ambapo alizungumzia juu ya biashara haramu ya binadamu ambayo imekuwa ikiendendeshwa na mtandao wa watu wasiowaaminifu kwa kuwalaghai mabinti wa Kitanzania kwa kuwaahidi kuwapa ajira nje ya nchi.kwenye mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.

Tuesday, June 7, 2016

JK ataka vijana waaminiwe na kuwezeshwa

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (awamu ya nne) Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete jana jumanne alitoa mhadhara wa 13 wa Kumbukumbu ya Rafael M. Salas ulioandaliwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu ( UNFPA), mhadhara huo ulikuwa ni sehemu ya vikao vya mwaka vya Bodi na Mifuko ya Umoja wa Mataifa vinavyoendelea katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Pamoja naye Meza Kuu ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Jan Elliason, Rais wa Bodi, na Balozi Carmelita R. Salas, mjane wa Bw. Rafael M. Salas

Benki ya Exim ya China kushirikiana na Tanzania katika sekta ya viwanda

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Aziz Mlima akiwa katika mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Exim ya China, Bi. Zhang Shuo alipofika Wizarani kwa mazungumzo. Katika mazungumzo yao Bi. Zhang alieleza nia ya Benki yake kuendelea kushirikiana na Tanzania katika Sekta ya Viwanda. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 07 Juni, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki atembelea Wizara ya Mambo ya Nje.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, Bi. Lilian Awinja. Bi. Awinja alionana na Katibu Mkuu kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Monday, June 6, 2016

Waziri Mahiga ampokea Naibu Waziri Mkuu wa Ubelgiji Mjini Dodoma

Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa na mgeni wake Mhe. 

Didier Reynders, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji mara baada ya kuwasili Mjini Dodoma kwa mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Serikali leo tarehe 6 Juni 2016.

Watafiti kuhusu masuala ya uchaguzi kutoka SADC wawasili nchini

Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Innocent Shiyo kulia akizungumza na Mtafiti kutoka SADC Bi. Patience Zonge raia wa Jamhuri ya Zimbabwe, ambaye  alitembelea katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujitambulisha kabla ya kuanza rasmi tathmini ya shughuli za Baraza la Ushauri kuhusu masuala ya Uchaguzi la SADC. Tathmini hiyo inafanyika kufuatia agizo la Kamati ya Mawaziri lililotolewa katika kikao cha 17 kilichofanyika tarehe 20 hadi 21 Julai, 2015 ambapo nchini Tanzania tathmini hiyo itafanyika kati ya tarehe 6-7 Juni, 2016.
Sehemu ya wajumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea, kutoka kushoto ni Bw. Revocatus L. Ouko na Bw.Mohamed Kamal Mohamed.

Saturday, June 4, 2016

Mkoa wa Dar es Salaam wasaini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Jimbo la JiangSu la nchini China


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akiwa katika mazungumzo na Katibu wa Chama Tawala cha China Communist Party of China (CPC) Mhe. Luo Zhijun, ambaye jana alitembelea katika ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kuwekeana saini ya makubaliano ya ushirikiano kati ya Mkoa huo na Jimbo la Jiangsu la nchini China 

Waziri Mahiga ashiriki hafla ya kumuaga Balozi wa Oman

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akiwa katika picha ya pamoja  na Balozi wa Oman nchini Mhe. Soud Al-Mohammed Al-Ruqaishi (kulia) wakati wa hafla ya kumuaga Balozi huyo baada ya kumaliza muda wake wa kazi nchini. Hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Hotel ya Hyatt Jijini Dar es Salaaam iliandaliwa na Mhe. Jasem Ibrahim Al-Najem (kushoto), Balozi wa Kuwait nchini. 

Friday, June 3, 2016

Tanzania kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi za Ghuba

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akimkaribisha leo katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, Balozi wa Oman hapa nchini Mhe. Saud Ali Mohamed Al-ruqaishi alipokuja kuaga baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini.

 Katika mazungumzo yao Waziri Mahiga alimshukuru Balozi kwa kuendeleza ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Oman, vilevile aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano hata kwa Balozi atakaye teuliwa kuja kuiwakilisha nchi ya Oman. kwa upande wa Balozi Al-raqaishi alitumia fursa hiyo kumshukuru Waziri Mahiga na uongozi wote wa Wizara kwa ujumla kwa ushirikiano aliokuwa akipewa kwa kipindi chote cha uwakilishi wa Taifa lake hapa nchini. 
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Tahir Bakari, kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Al-ruqaishi.
Waziri Mahiga na Balozi Al-ruqaishi wakiwa katika picha ya pamoja.
       ===Wakati huo huo Waziri Mahiga alizungumza na Balozi wa Nchi za Falme za Kiarabu===

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Falme za Kiarabu (U.A.E) nchini Mhe. Abdulla Ibrahim Ghanim Al suwaidi alipokuja kumtembelea wizarani, na kufanya naye mazungumzo  yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Falme za Kiarabu katika nyanja mbalimbali zikiwemo:  Afya, Elimu, Biashara na Uchumi, pia Balozi wa Al suwaidi alimpongeza Waziri Mahiga kwa Hotuba ya Bajeti ya 2016/2017 iliyopitishwa na Bunge. 
Waziri Mahiga na Balozi Al suwaidi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza mazungumzo
                      === Pia Dkt. Mahiga alikutana kwa mazungumzo na Balozi wa Kuwait  ====

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.), akisaliamiana na Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem alipomtembelea Wizarani mapema leo asubuhi na kufanya naye mazungumzo yaliyojikita katika kuboresha na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Kuwait.
Dkt. Mahiga akimweleza jambo Balozi Al Najem
Balozi Al Najem akimwelezea jambo Waziri Mahiga mara baada ya kuzindua Tovuti ya Ubalozi wao, huku Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya kati Balozi Abdallah Kilima (wa Tatu kutoka kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje wakishuhudia.  
Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Al Najem mara baada ya kumaliza mazungumzo yao.

==== Vilevile Balozi  Mahiga alikutana kwa mazungumzo na  Balozi wa Qatar ====
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Kulia) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Mhe. Abdulla Jassim Al Maadad alipokuja kumtembelea Wizarani, mazungumzo hayo yaliyojikita katika kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Qatar katika nyanja mbalimbali zikiwemo za Elimu, Biashara na Uchumi.
Balozi Al Maadadi naye pia alimweleza Waziri Mahiga atahakikisha kuwa anaendeleza mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na nchi yake, sambamba na kuhakikisha Serikali nchini Qatar inaisaidia Tanzania hasa katika sekta ya elimu, biashara na uchumi ambazo Qatar imekuwa ikifanya vizuri.
Mazungumzo yakiendelea
Waziri Mahiga akiagana na Balozi Al maadadi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao. 

==== Mwisho Mhe. Waziri alikutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia  ====

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Wajih Alotaabi alipokuja kumtembelea katika ofisi za Wizara  na kufanya naye  mazungumzo, ambapo katika mazungumzo yao Dkt. Mahiga ameshukuru Taifa la Saudi Arabia kwa kuwa na Mahusiano Mazuri na nchi ya Tanzania, pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Mhe. Alotaabi, kwa kufanikisha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje Mhe. Ade Al Jubair alipokuja kwa ziara ya kikazi nchini na kuweka saini ya Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi na Uwekezaji.  
Mhe. Wajih Alotaabi naye alitoa shukrani kwa ushirikiano ambao amekuwa akipewa na Wizara na Serikali kwa ujumla katika utekelezaji wa majukumu yake.
Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati Balozi Abdallah Kilima (wa kwanza kushoto), Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga pamoja na Afisa Mambo ya Nje Bw. Tahiri Bakari, kwa pamoja wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Kaimu Balozi wa Saudi Arabia Mhe. Wajih Alotaabi
Waziri Mahiga akifurahia jambo na Mhe. Wajih Alotaabi mara baada ya kumaliza mazungumzo 
Waziri mahiga katika Picha ya pamoja na Mhe. Alotaabi
Picha ya Pamoja


Wanachuo wa Royal Diffence College watembelea Wizara ya Mambo ya Nje.

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Edward Sokoine, akitoa maelezo ya awali wakati wa kuanza kwa mkutano na wanafunzi wa chuo cha Ulinzi cha Royal College of Diffence Studies kilichopo nchini Uingereza (hawapo pichani), ambao wapo kwenye ziara ya mafunzo katika nchi za Tanzania, Ethiopia na Malawi kwa ajili ya kubadilishana mawazo namna masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa yanayoibuka hivi sasa yanavyoathiri utulivu, usalama na ustawi wa nchi, kanda na dunia kwa ujumla. Mwingine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Samuel Shelukindo.
Baadhi ya wanachuo hao wakisikiliza maelezo kutoka kwa mzungumzaji meza kuu (hayupo pichani). Masuala mbalimbali yalijadiliwa ikiwa ni pamoja na hali ya usalama katika eneo la nchi za maziwa makuu, nafasi ya wakuu wa nchi za Afrika katika utatuzi wa migogoro, uhusiano wa Tanzania na nchi jirani na mikakati ya kukabiliana na ugaidi katika kanda na dunia kwa ujumla.
Baadhi ya wanachuo pamoja na Askari wa JWTZ (waliovaa sare), wakisikiliza maelezo kutoka kwa mzungumzaji meza kuu (hayupo pichani).
 
Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia kwa makini mazungumzo.Wa kwanza kutoka kulia ni Bi. Olivia Maboko, Bi. Lilian Kimaro na Bi. Mona Mahecha
Mmoja wa wanachuo hao akiuliza swali.

Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Samuel Shelukindo akiendelea kufafanua jambo katika mkutano huo.
 
Kikao kikiendelea...
 Balozi Sokoine, akifafanua jambo.
Kikao kikiendelea.
======================
PICHA NA: REUBEN MCHOME.