Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Suzan Kolimba(Mb) akiwa katika mkutano na Naibu Mkurugenzi wa Kampuni ya simu ya Halotel nchini Bw. Pham Dinh Quan alipomtembelea Wizarani jana tarehe 31 Oktoba,2017, Dar es salaam.
Katika Mazungumzo yao Bw. Quan alisema kampuni ya halotel hadi sasa imewekeza katika eneo kubwa la Tanzania hasa vijijini, alisema hadi sasa Kampuni hiyo imewekeza asilimia 80 ya eneo la Tanzania na wana mpango wa kuongeza uwekezaji zaidi katika eneo ambalo halijafikiwa. Mhe. Dkt. Kolimba alipongeza kampuni ya Halotel kwa uwekezaji huo mkubwa ambao umesaidia kurahisisha mawasiliano nchini hasa Vijijini.
Mkutano huo ukieendelea.
Naibu Waziri Mhe.Dkt. Suzan Kolimba (Katikati), Naibu Mkurugenzi wa Halotel Bw. Pham Dinh Quan kushoto kwake na kulia ni Bw. Emmanuel Luangisa Afisa Mambo ya Nje wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano.